Mtei - Mbowe - BoT; Connecting the dots...

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,017
7,220
Mwenyekti wa kwanza wa CHADEMA, Mzee Edwin Mtei, alikuwa Gavana wa BoT.

Mwenyeti wa sasa wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, alikuwa mwajiriwa wa BoT.

Kabla ya kupata uenyeti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, alimuoa mtoto wa Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA, Mzee Edwin Mtei.

Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA, amekiri kwa maandishi kuwa anamiliki mabilioni ya shilingi pesa tasilimu na mali zisizohamishika yenye thamani ya mabilioni ya shilingi.

Hesabu za kiasi cha kodi alicholipa Mh. Freeman Mbowe kwa miaka kumi iliyopita hakiendani na utajiri huo mkubwa alio nao.

Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA Mzee Edwin Mtei, hupenda kujitambulisha kama mkulima. Hata hivyo, utajiri wake ni mkubwa sana kuliko kiasi cha uzalishaji wa shamba lake lililopo Tengeru, Arusha.

Mzee Mtei amekuwa akitumia pesa zake binafsi kuendesha shughuli zote za CHADEMA tangu ilipoanzishwa mpaka ilipofikia hatua ya kupata wabunge na ruzuku. Huu ni utajiri wa hali ya juu. Sio mbaya kuwa tajiri, lakini utajiri wa mtu ni lazima uendane na kiasi cha kodi anacholipa. Mtu akiwa tajiri sana lakini katika orodha ya walipa kodi haonekani, ni ishara ya ufisadi.

Ukwasi huu wa wanasiasa hawa wawili walioitumikia BoT na kuamua kuunganisha familia zao kwa njia ya ndoa ya binti wa mmoja wao unatokana na chanzo gani?

Je, kuunganisha familia hizi ni njia ya kuongeza uaminifu wa "ushirikiano" waliokuwa nao tangu BoT? Je, "ushirikiano" wao waliouanza BoT unaendelea ndani ya Chadema? Je, hii ndio sababu ya Mzee Mtei kulazimisha Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti na kukataza wagombea "who are from nowhere"?.

Je, biashara ya ukumbi wa muziki inamuwezesha mtu kumiliki mabilioni nje ya nchi? Kiingilio bilicanas ni shilingi ngapi kila mtu? Kwa siku wanaingia watu wangapi? Je, zinatosha kununua nyumba Uingereza, Marekani, Afrika Kusini na Dubai?

Its too early to go to bed, wake up. Connect the dots...

=================================
UFAFANUZI toka kwa Ndugu Edwin Mtei
=================================

Post # 1

Nalazimika kuandika kuelezea maisha na utumishi wangu kwa umma na taifa letu, kutokana na juhudi za wahasimu wangu ku-"connecting the dots...." kumfikia Mbowe.

Inavyofahamika, nilibahatika kuteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha 9 Septemba 19064. Binti yangu Lilian' ambaye alikuwa mtoto wetu wa pili, alizaliwa 29 Sept 1964 na ameolewa na Mbowe. Yeye Freeman alizaliwa 14 Sept., 1961 na wazazi wake walimpa jina hilo alipobatizwa siku yetu ya Uhuru, 9 Decemba, 1961.

Mwalimu Nyerere aliniteua kuanzisha sarafu yetu na Benki Kuu Octoba 1965 na shughuli za BoT zilianza rasmi tarehe 14 Juni, 1966. Niliachia u-Gavana Aprili 1974 nakawa Katibu Mkuu EAC (Phase I) Charles Nyirabu akinuridhi kama Gavana. Februari 1977 nikateuliwa Waziri wa Fedha ambapo kufuatia kutokubaliana na boss wangu kuhusu sera za fedha na uchumi, nilijiuzulu Novemba 1979 nikahamia Arusha kuwa mkulima wa kahawa 1980 mpaka leo.

Itaonekana ni upotoshaji usiopingika kwamba nikiwa Gavana 1965 hadi 1974, Freeman na Lilian walikuwa watoto wachanga wakisoma shule za chekechea na primari na wasioweza kuhusishwa na miradi.

Serikali ya Mwalimu iliniteuwa IMF Executive Director Novemba 1982, nikaweza kuhamia Washington D.C, na wanangu wakaweza kumalizia sekondari na university huko Merikani, isipokuwa Lilian ambaye baada ya sekondari aliamua kurudi Tanzania kusomea udaktari Muhimbili ambapo alifaulu vizuri sana. Nahisi ni wakati huu walifahamiana na Freeman, na wakaoana Augost 1991.

Harakati za siasa za vyama vingi zilishika kasi mwanzoni mwa 1992, Francis Nyalali alipokabidhi ripoti yake. Mimi binafsi nilijitwika mzigo wa kulea Chadema nilichoshiriki kuasisi. Nilihamia Dar es Salaam, hadi 1998, nikiishi kwa mapato yangu binafsi, nikitumia magari yangu na ya waasisi wenzangu na washaabiki wetu kuzuru na kutembelea kila wilaya Tanzania Bara isipokuwa Makete, Ngara na Ukerewe. Kila wilaya niliyozuru niliacha ofisi au tawi la Chadema. Mara nyingi nilikuwa mgeni wa wanachama wapya. Zanzibar nilizuru pia, lakini ungozi wa CDM huko ndio walisimika Chadema.

1998 niliachia uenyekiti kwa Bob Makani, ndipo nikaweza kurudia shamba na mashughuli yangu mengine. Inafahamika kwamba Freeman Mbowe aliongoza Vijana wa Chadema tangu mwanzo; na ameongoza chama kama Chairman tangu 1993, Makani alipoachia uenyekiti, na akishirikiana hasa na Dr. Willibrod Slaa wamesimika Chadema Tanzania. Najisikia raha sana na kuwa na matumaini kwamba ukombozi wetu u karibu, hasa nikiona jinsi vijana wenye uzalendo wa hali ya juu, wenye ujasiri na umakini wakimiminika kwa wingi kutuunga mkono. Kauli mbiu zetu za "Peoples' Power" na " Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke" zimenisisimua sana na kunipa matumaini ya Ushindi mapema.

Post # 2

ZEMarcopolo,

Nimeeleza kwamba nikiwa Gavana BoT (1965-74), Freeman Mbowe na binti yangu Lillian walikuwa watoto wachanga, na singeweza kuwashirikisha katika miradi. Freeman alikuwa na miaka 4, na Lillian alikuwa na mwaka mmoja!!

Licha ya kwamba hizi zilikuwa enzi za Ujamaa, babake Freeman alikuwa mjasiriamali mzito, akimiliki Mbowe Hotels Dar es Salaam na Moshi, na ni wakati huu alijenga Aishi Hotel huko Machame. Nakumbuka nikihudhuria uzinduzi rasmi wa Aishi Hotel uliofanywa na Rais Mwalimu Nyerere aliyekuwa rafiki wa Aikaeli Mbowe. Wakati huu sikuwa mzazi mwenza na Freeman labda alikuwa shule ya sekondari.

Freeman Mbowe amerithi hii miradi baada ya kifo cha babake, na ameiendeleza na kuipanua kwa umahiri sana, e.g. kama kuongeza Club Billicanas huko Dar, na Conference Centre pale Aishi. Umahiri na umakini wa Freeman katika business na sawa na ule anaodhihirisha kama mwanasiasa.

Kuhusu mimi binafsi, umesema ukweli kwamba shamba langu la kahawa si kubwa. Gharama za uendeshaji ni kubwa. na mimi nasema nalima kahawa kama "hobby" tu. Ni wakulima wachache sana wanaopata faida kwa kulima kahawa. Soko lake linamilikiwa na wanywaji wa kahawa nchi za nje na hii ndiyo sababu ya kusuasua kwa zao hili hapa Tanzania.

Hata hivyo mara baada ya kununua hili shamba 1980, nilihamia Washington D.C. kama Executive Director wa IMF (end 1982) kwa kupendekezwa na Rais wangu, Mwalimu Nyerere. Nilibahatika kuhama na wanangu waliokwenda kumalizia shule za sekondari huko, pamoja na University kabla ya kurudi nyumbani. Binti yangu Lillian alirudi nyumbani baada ya High School na kujiunga na Muhimbili Medical, akawa daktari. Ni wakati huu walifahamiana na Freeman, wakaoana August 1991 kabla hata ya harakati za siasa ya vyama vingi.

Nimesema nilibahatika kuteuliwa IMF Executive Director 1982, na nilipofika huko nilijiunga na pension scheme ya IMF, ambapo mara baada ya kurudi nyumbani na kuwa na umri wa miaka 60, nikaanza kulipwa pension. Pamoja na savings zangu za huko Washington niliweza kukamilisha masomo ya wanangu na IMF sasa inanilipa pension ambayo ni kidogo kutokana na muda mfupi (miaka 4 tu) niliyotumikia shirika hili la kimataifa.

Kutokana na pension yangu na mapato mengine e.g. house rent tumeweza kuishi na kuendeleza maisha yetu bila kuwa ombaomba. Ukulima wetu sasa unabadilika taratibu kuwa pia na mahindi pamoja na kuongeza nyumba hapa shambani kadri kipato kinavyoruhusu au mikopo inavyopatikana.
 
Balali na CCM wenyewe wanamiliki nini?

Mbowe si kila siku mnamponda hapa eti std seven alikuwa na cheo gani BOT hadi kuweza kuchota Pesa?
mbona Mwigulu aliajiriwa BOT naye ana mabilioni?

kuajiriwa BOT haikufanyi uwe na Mabilioni.
 
Hujawahi kutoa hoja yenye MASHIKO,shamba la mzee MTEI ni dogo kuliko langu lililopo Gomba estate lenye kahawa za kutosha,Napakana na NYAGA MAWALLA.arusha kumiliki ivi viploti ni kawaida but mtu ukiweka sokoni ama kuvuna kilichomo humo Utaitwa fisadi na AKILI NDOGO KAMA YAKO.Utatwanga maji ktk kinu na magamba yako.
 
Kwa akili yako Mbowe anamiliki biashara moja ya Ukumbi wa Burudani (Billicanas)?

Na kama hajalipa/ halipi kodi huoni kama huo ni udhaifu wa Serikali yetu ya CCM ktk kukusanya kodi?

Na kama, kwa namna yoyote ile walitumia nafasi zao vibaya kwa maslahi binafsi wakiwa watumishi wa UMMA kwa nini serikali haikuwachukulia hatua? Huoni kama huo nao ni udhaifu wa Serikali yetu sikivu ya Chama Cha Mapinduzi?
 
Kwa akili yako Mbowe anamiliki biashara moja ya Ukumbi wa Burudani (Billicanas)?

Na kama hajalipa/ halipi kodi huoni kama huo ni udhaifu wa Serikali yetu ya CCM ktk kukusanya kodi?

Na kama, kwa namna yoyote ile walitumia nafasi zao vibaya kwa maslahi binafsi wakiwa watumishi wa UMMA kwa nini serikali haikuwachukulia hatua? Huoni kama huo nao ni udhaifu wa Serikali yetu sikivu ya Chama Cha Mapinduzi?

Ndio fikra zinazorudisha nyuma maendeleo hizo. Unaiibia serikali halafu uansema ni makosa ya CCM!
 
Yaani we ze makopolo unataka kuhalalisha ufisdi unaofanywa na wanaccm wenzako kwa kulinganisha na umiliki wa nyumba alionao mbowe, kiukweli mnachokifanya sasa ni kuisafisha ccm kwa kinyesi hamtafika popote aise kumbe kuna haja cdm wachukue nchi, namshukuru mwita maranya alitahadhalisha khs mkakati wa kumchafua mbowe na chadema unakuja, binafsi kuanzia leo ctashabikia ccm tena.
 
Yaani we ze makopolo unataka kuhalalisha ufisdi unaofanywa na wanaccm wenzako kwa kulinganisha na umiliki wa nyumba alionao mbowe, kiukweli mnachokifanya sasa ni kuisafisha ccm kwa kinyesi hamtafika popote aise kumbe kuna haja cdm wachukue nchi, namshukuru mwita maranya alitahadhalisha khs mkakati wa kumchafua mbowe na chadema unakuja, binafsi kuanzia leo ctashabikia ccm tena.

Ukinionyesha sehemu nilipohalalisha ufisadi nitakulipa milioni 10.
 
Buku 7 team mna kazi ya ziada.
Kwa wale walioko Wilaya ya Hai wanafahamu ni kiasi gani mzee Aikael alivyojitosheleza kwa utajiri toka enzi hujazaliwa.
Kwanini bilicanaz ndo umeona mapato yake tu?
Vp kuhusu hotel za Aish Protea hazina mapato?
Je hana hisa ktk mashirika mbalimbali?
Ungetaja utajiri anaomiliki na kiasi cha fedha alichoachiwa na wazazi wake ili tumkosoe.

Ukimaliza tuchambulie na list of Shame.
 
Ukiona mtu mwerevu akikusanya umati wa watu kuwaeleza upuuzi huku akijua fika kwamba anachowaeleza ni upuuzi na kwamba wanatambua kuwa wanaambiwa upuuzi basi mtu huyo atakuwa amewapuuza wanaomsikiliza kwa kiwango kikuu! Sijui hizi attacks za wenye mtazamo hasi na sera za CCM mamboleo zitaisha lini!
 
Jamani msigombane jibuneni kwa hoja mbona pande zote mnatoka mapovu?tusio na vyama tunasubiri ukweli wa hao wote wenye mahela huko regardless ya upande anakotoka,tunataka hela zetu full stop ohh cdm mara ccm!ukweli uwekwe wazi
 
Hujakatazwa kuanzisha thread ya kujadili "ubilionea" wa Ridhiwani.

Hapa tunajadili Mtei - Mbowe - BoT connection...


tnakuwa mafukara nyie vibaraka wa mafisadi wa ccm mnatukebei na ktudhiaki, jaman ivi watoto pia wajukuu wetu urithi wao utakua ni upi?
angalia gesi ilivowakost wanamtwara just kugundulika tu miez 10 bomba lipo bagamoyo kwa kina ridhiwan, vp barabara 2mtwara 50 yr aijawai kuisha, angalieni masuala ya Epa, hujuma za bot, alex sterwat, mikataba ya madin i.e buzwagi nk, wiz bandalini nk, ivi vitu vnalidhohofisha taifa,

wewe unakuja na utani, ayo ayo masuala ya ela za uswiz, can u tel us why sinc then serikali imekua kimya? wanawajua wahun hao ambao weng ni makada wa ccm,

ebu tutumie bongo zetu vzr tnapojadili maslai ya taifa tuache utan o.wise tnataftiana ban pia kuharibiana siku
 
Jamani msigombane jibuneni kwa hoja mbona pande zote mnatoka mapovu?tusio na vyama tunasubiri ukweli wa hao wote wenye mahela huko regardless ya upande anakotoka,tunataka hela zetu full stop ohh cdm mara ccm!ukweli uwekwe wazi

Mkuu,

Ukweli uko wazi. Kinachotakiwa ni kuunganisha dots tu ili kuufikia ukweli.

Mzee Mtei alipobanwa kuhusu tenda ya magari ya M4C ya Chadema alijibu hivi:

niliachia ngazi Chadema 1998 na tangia hapo sishiriki ktk mambo ya uendeshaji wa Chama ambapo ningeweza kukujibu juu ya zabuni iliyohusu magari ya M4C.

Je, wewe phill unaamini kuwa Mzee Mtei hajui kuhusu manunuzi ya magari ya M4C. Hasahasa baada ya kusoma hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...m4c-na-pikipiki-kufisadi-ruzuku-ya-chama.html
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom