Mwenyekti wa kwanza wa CHADEMA, Mzee Edwin Mtei, alikuwa Gavana wa BoT.
Mwenyeti wa sasa wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, alikuwa mwajiriwa wa BoT.
Kabla ya kupata uenyeti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, alimuoa mtoto wa Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA, Mzee Edwin Mtei.
Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA, amekiri kwa maandishi kuwa anamiliki mabilioni ya shilingi pesa tasilimu na mali zisizohamishika yenye thamani ya mabilioni ya shilingi.
Hesabu za kiasi cha kodi alicholipa Mh. Freeman Mbowe kwa miaka kumi iliyopita hakiendani na utajiri huo mkubwa alio nao.
Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA Mzee Edwin Mtei, hupenda kujitambulisha kama mkulima. Hata hivyo, utajiri wake ni mkubwa sana kuliko kiasi cha uzalishaji wa shamba lake lililopo Tengeru, Arusha.
Mzee Mtei amekuwa akitumia pesa zake binafsi kuendesha shughuli zote za CHADEMA tangu ilipoanzishwa mpaka ilipofikia hatua ya kupata wabunge na ruzuku. Huu ni utajiri wa hali ya juu. Sio mbaya kuwa tajiri, lakini utajiri wa mtu ni lazima uendane na kiasi cha kodi anacholipa. Mtu akiwa tajiri sana lakini katika orodha ya walipa kodi haonekani, ni ishara ya ufisadi.
Ukwasi huu wa wanasiasa hawa wawili walioitumikia BoT na kuamua kuunganisha familia zao kwa njia ya ndoa ya binti wa mmoja wao unatokana na chanzo gani?
Je, kuunganisha familia hizi ni njia ya kuongeza uaminifu wa "ushirikiano" waliokuwa nao tangu BoT? Je, "ushirikiano" wao waliouanza BoT unaendelea ndani ya Chadema? Je, hii ndio sababu ya Mzee Mtei kulazimisha Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti na kukataza wagombea "who are from nowhere"?.
Je, biashara ya ukumbi wa muziki inamuwezesha mtu kumiliki mabilioni nje ya nchi? Kiingilio bilicanas ni shilingi ngapi kila mtu? Kwa siku wanaingia watu wangapi? Je, zinatosha kununua nyumba Uingereza, Marekani, Afrika Kusini na Dubai?
Its too early to go to bed, wake up. Connect the dots...
ZEMarcopolo,
Nimeeleza kwamba nikiwa Gavana BoT (1965-74), Freeman Mbowe na binti yangu Lillian walikuwa watoto wachanga, na singeweza kuwashirikisha katika miradi. Freeman alikuwa na miaka 4, na Lillian alikuwa na mwaka mmoja!!
Licha ya kwamba hizi zilikuwa enzi za Ujamaa, babake Freeman alikuwa mjasiriamali mzito, akimiliki Mbowe Hotels Dar es Salaam na Moshi, na ni wakati huu alijenga Aishi Hotel huko Machame. Nakumbuka nikihudhuria uzinduzi rasmi wa Aishi Hotel uliofanywa na Rais Mwalimu Nyerere aliyekuwa rafiki wa Aikaeli Mbowe. Wakati huu sikuwa mzazi mwenza na Freeman labda alikuwa shule ya sekondari.
Freeman Mbowe amerithi hii miradi baada ya kifo cha babake, na ameiendeleza na kuipanua kwa umahiri sana, e.g. kama kuongeza Club Billicanas huko Dar, na Conference Centre pale Aishi. Umahiri na umakini wa Freeman katika business na sawa na ule anaodhihirisha kama mwanasiasa.
Kuhusu mimi binafsi, umesema ukweli kwamba shamba langu la kahawa si kubwa. Gharama za uendeshaji ni kubwa. na mimi nasema nalima kahawa kama "hobby" tu. Ni wakulima wachache sana wanaopata faida kwa kulima kahawa. Soko lake linamilikiwa na wanywaji wa kahawa nchi za nje na hii ndiyo sababu ya kusuasua kwa zao hili hapa Tanzania.
Hata hivyo mara baada ya kununua hili shamba 1980, nilihamia Washington D.C. kama Executive Director wa IMF (end 1982) kwa kupendekezwa na Rais wangu, Mwalimu Nyerere. Nilibahatika kuhama na wanangu waliokwenda kumalizia shule za sekondari huko, pamoja na University kabla ya kurudi nyumbani. Binti yangu Lillian alirudi nyumbani baada ya High School na kujiunga na Muhimbili Medical, akawa daktari. Ni wakati huu walifahamiana na Freeman, wakaoana August 1991 kabla hata ya harakati za siasa ya vyama vingi.
Nimesema nilibahatika kuteuliwa IMF Executive Director 1982, na nilipofika huko nilijiunga na pension scheme ya IMF, ambapo mara baada ya kurudi nyumbani na kuwa na umri wa miaka 60, nikaanza kulipwa pension. Pamoja na savings zangu za huko Washington niliweza kukamilisha masomo ya wanangu na IMF sasa inanilipa pension ambayo ni kidogo kutokana na muda mfupi (miaka 4 tu) niliyotumikia shirika hili la kimataifa.
Kutokana na pension yangu na mapato mengine e.g. house rent tumeweza kuishi na kuendeleza maisha yetu bila kuwa ombaomba. Ukulima wetu sasa unabadilika taratibu kuwa pia na mahindi pamoja na kuongeza nyumba hapa shambani kadri kipato kinavyoruhusu au mikopo inavyopatikana.