Mtei kasema UKWELI ULIOSHINDWA KUTAMKIKA, tuache unafiki!

Mtei kasema UKWELI ULIOSHINDWA KUTAMKIKA, tuache unafiki!

Tatizo kubwa la watawala hawapendi kuambiwa ukweli wao wanapenda kupambwa na sifa za kijinga kama serikali ya ccm ni sikivu kumbe wizi mtupu
 
Wengi tumejitenga na ukweli unaouzi. Katika kuunda tume ya katiba JK Ameshindwa kuepuka shinikizo la Redio Imani na Gazeti la al-nuur.

Ubaya tumefundishwa kuchukia DINI na si UDINI! MFANO chadema kinaitwa chama cha kikristu kwasababu tu uongozi wake wa juu unawakristo wengi.

Lakini CUF kimejaa waislamu wengi toka miaka ya tisini lakini JK hakukiusisha na udini! Unajua ni kwanini ni mpinga dini na si udini!

Tunataka kuaminishwa kuwa adui mkubwa wa mwislamu ni mkristo na adui mkubwa wa ukristo ni mwislamu. Tunasahau kuwa uislamu na ukristo asili yake ni moja Ibrahimu. Tunataka kuwasahau maadui tunaopambana nao ni walewale Ujinga, Umasiki, Maradhi na Rushwa.

Ubaya tumeitupa ELIMU tukaaminishwa UJINGA tukashindwa kuutambua ukweli. Majizi yanachangia makanisa na misikiti kwenye arambee tunayaona kama marafiki.

Mawazo ya Ar-nuur na Redio Imani ambayo ni msingi wa uteuzi wa tume;-
Tume iundwe na nusu ya wajumbe kutoka bara na nusu kutoka zanzibar(bila kujari ukubwa na idadi ya watu kutoka pande hizo). Na hili tundulisu alilipinga vikali akaonekana Mjinga.

Wajumbe kutoka zanzibar wawe waislamu wote sababu zanzibar ni nchi ya kiislamu na wajumbe kutoka bara wawe nusu wakristo nusu waislamu sababu ndio dini kuu kwa huku bara. Na kutowatambua kabisa wasio na dini.

Kwa mchanganuo huo maslai ya waislamu yataingia kwenye katiba mpya. Kwani 75% ya wajumbe watakuwa waislamu na25% tu ndio wawe wakristo. Ila moja ya dai kuu la waislamu ni nafasi sawa za uongozi, mahakama ya kadhi na kupinga mfumo kristo. Hawana habari juu ya ufisadi mfumo mbovu wa elimu, huduma duni za afya, rushwa na mfumuko wa bei.

Katika kuteua tume JK Kazingatia maoni ya media za kiislam. Je anaamini kama wao au ni kupunguza mashinikizo ya waislamu zidi yake.

Ata katika uteuzi wa majaji, wakuu wa mikoa na wilaya, mawaziri JK ujitaidi kuzingatia hili. Hii ni hatari! Tuzingatie uwezo tu.

Sioni tatizo atakama jk angeteua waislamu wote ila tu wawe na uwezo.
PILLI NATOARAI WATUMBE WA TUME WAANGALIE MASLAI YA TAIFA NA SIO DINI ZAO KWAN UMA HAUTAWEZA KUKAA KIMYA
Hii ilitakiwa iwekwe "sticky" kwa muda, very well said mkuu.
 
Mtei kasema kweli inakuwaje wakristo wakipigia kelele jambo la kutokuwa na usawa katika uwakili wa dini inaonekana ni udini na waislamu wakipiga kelele inaonekana ni haki? mfano Sumaye alipounda bodi ya parole wakrsto walikuwa wengi na waislamu walipiga kelele jambo lililofanya ikavunjwa hiyo bodi na kuundwa upya kwanini hapa kwenye katiba ionekane ni udini wakati ni haki?

Haiwezekeni Zanzibar wawe wote ni waislamu wakati kuna makanisa Kikwete kashindwa kuteua wakristo walioko Zanzibar? mbona Jaji Agustine Ramadhani au Issack Sepetu ni wakristo ambao asili yao ni Zanzibar wanopinga hoja wanataka kusema wakristo Zanzibar ni wawili tu Jaji Ramadhani na Sepetu? kama ni hivyo hayo makanisa yaliyoko Zanzibar wanaosali ni waislamu? kama sio waisilamu wanaosali sasa inakuwaje wakose hata wajumbe watatu wakristo toka Zanzibar?

Haya ndio mambo yaliyopo kwenye kamati kuu ya CCM pia ambayo ina wajumbe 32 kati ya hao wakristo ni 9 tu na 21 wote ni waislamu sababu ya 'Zanzibar equation" ndio maana napenda muungano uvunjike na ninamlaumu Nyerere kwa huu Muungano ingawa mimi ni mshabiki wake mkubwa maana muungano unawapa waislamu mamlaka makubwa wakati wao sio wengi kama wakristo Zanzibar isingekuwepo tungekuwa sawa kwa sawa angalia mfano wa Rais na Makamu wa Rais wao waislamu wanaweza kutoa Rais na makamu wote waislamu lakini wakristo hawawezi kufanya hivyo maana wakifanya hivyo tu tayari hoja ya udini inakuja
Another reason why this thread should be on "sticky" is this.
Again, very well said mkuu.
 
N
Nadhani Mtei hakutakiwa kutamka ile kauli.
Ikumbukwe hakuna sehemu yeyote iliyoandikwa kuwa idaidi ya viongozi waumini wa dini fulani iwe percent kadhaa na ya dini flani iwe percent kadhaa.
Ndio maana kwangu mimi malalamiko yeyote yale yanayohusu idadi flani ya viongozi wanaoamini dini flani kuwa ni kubwa kuliko wa dini fulani, nayaona ni ya kipuuzi.
Otherwise, iandikwe kwenye katiba ijulikane wazi kuwa mfano Rais akiwa mpagani, basi Makamo awe ni muumini wa Wachawi, Waziri wa fedha awe freemason, Waziri mkuu awe Mhindu n.k.
Kama hakuna makubaliano hayo then malalamiki yote yanayohusu mambo ya dini za viongozi, ni ujinga na upuuzi mtupu.

Ndibalema:
Umesomeka kiukweli kweli.
Tuwe wavumilivu tusubiri tuone, pengine Rais hakuchagua based on such claimed criteria; kumbe lengo ni kupata Katiba mpya inayo cover area zote of concern bila kujali huo udini; or rather ukristo na uislamu!

Sasa wale wahindu, freemasons, wapagani na waanga wasemeje? Kwani kama uislamu na ukristo ulikuwa kigezo, nao wapewe kanafasi angalau 2 out of 30 members

Tuwe waungwana kama ilivyo hulka yetu watz, naamini hakuna kitakachotutenganisha kamwe
 
Dr upo ?

Nilisikitika sana ulipoaga maana jukwaa lilipwaya sana natumai uko mzima. Hawa ndugu zetu wakristo washazoea waislamu ni wafagizi na wazibua vyoo na huo msemo wa mzee mtei amezungumza lililopo ndani moyo yake. Unakumbuka statement yake aliyomwambia Zitto kuwa hawezi kumpa chama mtu asiyemfahamu na asiyefahamika. Huo ni msemo wa wabaguzi wa kikristo ambao huchukulia waislamu ni waswahili na waswahili hawajasoma hivyo hawana maana yeyote. Kuna mtu mmoja toka kaskazini aliwahi kunifunulia anasema wachaga na wameru wanasema asili ya neno mswahili ni mtu asiye na maana katika jamii, mvivu na asiyestaarabika.

Zama zinabadilika sasa ni jino kwa jino. Waislamu wengi wamesoma na wanadeserve na haki yao kuwa na position nchini mwao instead of being treated as second class citizen nchini mwao. Failure to address this issue mwisho wa siku Tanzania itakuwa haikaliki kwani waislamu wameamka na hawatanii.

Baadhi ya wanasupport kauli ya Mtei na kundi lake wanafiki kwani kama tunadai uwiano tuanzie kwanza katika chadema almost 89% ya wagombea ubunge mwaka 2010 walikuwa wakristo waislamu walikuwa just a handful 11%, Tuende katika serikali ambapo tunaona viongozi wote wa juu serikalini almost 70% or more ni wakristo je nalo hilo mbona hamlisemi? Tuje katika wakurugenzi wa taasisi za serikali na wizara huko ndio balaa zaidi maana almost 80% or more ni wakristo mbona hamsemi???? Tukishuka chini zaidi katika mgawanyo wa rasilimali Taasisi za kikristo zinapata almost Bilioni 90 kila mwaka na walikuwa wakipata almost Trilioni 2 tangu wapitishe mkataba wao wa kifisadi (MOU kati ya makanisa na serikali) mbona hamsemi wakati waislamu hawapati chochote!!!! Tutafika tu pole pole
Mdondoaji, nini kilichobadilika hadi waislam wakapata elimu zaidi, hence nafasi zaidi?

Na ni nani alikuwa akiwazuia kupata elimu hadi wakawa wafagiaji?

Naomba ujibu hili tafadhali, kwasababu kuna a follow up question.
 
Kwa nini wabunge wa Chadema viti maalum wengi ni Wakirsto?

Kuna wabunge 25, Wakirsto ni 19 na Waislam ni 6 tu.

Mlitumia vigezo gani kuwapata hawa wabunge?

Hilo liko wazi sana Tanzania bara wakristo wengi kuliko waislam, pili ndo walienda shule mapema wakati waislam waking'ang'ania madrasa.

Naitamani Tanganyika yangu jamani, hawa jamaa wanaolazimisha muungano wanatunyima haki zetu.
 
Kuna kiongozi wa Chadema anajiita Rev Mzito k ni mtu hatari sana mdini number 1, na ndio namba 1 kwenye Anti Zitto Kabwe campaign. Sasa kwa Chama cha siasa kuwa na makada wa dizaini hii, its just a matter of time bomu linalipuka!
 
Rais ni Muislam, Makamu ni Muislam, Rais wa Zanzibar ni Muislam, Waziri wa fedha ni Muislam, Waziri wa Elimu Muislam, Waziri wa Afya Muisla,Waziri wa Ulinzi ni Muislam, Waziri wa Mambo ya ndani ni Muislam. Wizara nyeti zimewekwa waislam.Judge Mkuu Muislam, Judge Kiongozi Muislam, IGP Muislam. Wakristo hawalii lii udini. Leo Kikwete katumia upole na ukimya wa wakristo kuwadharau. Kajaza waislam kwenye tume ya katiba ili kuileta katiba ya Jamhuri ya waislam Tanzania.

Ndiyo sababu katika awamu yake nchi imekosa heshima, mwelekeo na maendeleo; hii ni kwa sababu majinga yameshikishwa usukani wakati hayana upeo kutokana na akili zilizoingia kutu ya imani yao.
 
CHADEMA kipo kwa maslahi ya wakristo hasa wa kaskazini, hii nadhani sio siri tena. Thanks Mzee Mtei!
 
Ulevi ni ulevi tu!!
Anaekunywa gongo na wiski wote kuyumba kwao ni kulekule!
Katika haya sihitajii kushangaa bali kusikitika kwa maana wako wanaojenga msingi wa nyumba zao katika vumbi badala ya kuujenga kwenye mwamba!!
Haya hayakuanza leo!
Wengi hatujui wala hatutafuti ujuzi bali tunakurupuka tu!!! kwa sababu imesemwa na fulani!!!
Vema ujumbe unafika na wenye fikra wanatambua kutofautisha pumba makapi na mchele
 
Ndiyo sababu katika awamu yake nchi imekosa heshima, mwelekeo na maendeleo; hii ni kwa sababu majinga yameshikishwa usukani wakati hayana upeo kutokana na akili zilizoingia kutu ya imani yao.
...Ilifika wakati mgumu wananchi tulifadhaika!!! hicho ni kipande cha wimbo ambacho kilistahili kuimbwa kwa usahihi kabisa kwa wakati nchi inatawaliwa na baba wa Taifa!!
Kweli Wananchi walifadhaika kwa sababu hakukuwa na usafiri, wala bidhaa ADIMU!! (mchele, dona, sukari n.k)
Kwa sababu hiyo hali ya uchumi ilikuwa ni 0.02% mpaka mwaka 1985 sasa hapo sielewi nini kipya katika nchi hii na watu hawataki kujiuliza ubovu uko katika dini au akili za watanzania!!!
 
Vita anatangaza amiri jeshi mkuu ambaye ni ustadh. kikwete
atasaidiwa na waziri wa ulinzi ambaye ni ustadh Hussen mwinyi
wengine watakaompa tafu ni waziri wa mambo ye ndani ambaye ni ustaadh Nahodha
Uhakika wa fedha utapatikana toka kwa waziri wa fedha ustaadh mkuro
ustadh Nundu
atarahisisha uchukuzi wa vifaa vya kijeshi na zana nyingine
ustaadh Dr. shein ataongoza kikosi kidogo KMKM tokea zanzibar
ustaadh makamu wa rais dr bilali atabakia ikulu kuangalia logistic ny
Mmeshikwa pabaya hamna pa kutokea

Umemsahau ustadh Mwema..
 
Mkuu nimependa hizo takwimu zako naona ni mzuri kwenye mambo ya takwimu naomba unasaidie na hizi takwimu.

Kwa nini wabunge wa Chadema viti maalum wengi ni Wakirsto?

Kuna wabunge 25, Wakirsto ni 19 na Waislam ni 6 tu.

Mlitumia vigezo gani kuwapata hawa wabunge?
Hapo mkuu hakuna majibu utakayopata!!!
 
Hilo liko wazi sana Tanzania bara wakristo wengi kuliko waislam, pili ndo walienda shule mapema wakati waislam waking'ang'ania madrasa.

Naitamani Tanganyika yangu jamani, hawa jamaa wanaolazimisha muungano wanatunyima haki zetu.

Mkuu kwani sifa za kuwa mbunge ni zipi? Halafu nipe takwimu za Wakirsto na Waislam na wale wasiokuwa na dini Tanzania...halafu tuendelee na mjadala.
 
Duh! Sasa mwabishana kitu gani ? Mi nadhani Mtei yuko right, na kwa vile mpo ktk process ya katiba mpya nadhani solution yake ni kuweka kifungu cha 50%-% ktk kada zooote hadi kwa wajumbe wa nyumba 10! Atakaebisha hili atakuwa mkorofi na mkorofi sio mwenzetu.
 
Duh! Sasa mwabishana kitu gani ? Mi nadhani Mtei yuko right, na kwa vile mpo ktk process ya katiba mpya nadhani solution yake ni kuweka kifungu cha 50%-50% ktk kada zooote hadi kwa wajumbe wa nyumba 10! Atakaebisha hili atakuwa mkorofi na mkorofi sio mwenzetu.
 
William mshumbusi,
Mkuu wangu katiba inapoundwa haijalishi Taifa hilo lina watu millioni 1 au millioni 50 maadam kinachotazamwa ni haki za watu wananchi wake..Hata kama wajumbe hawa wote wangekuwa wakristu kwa majina yao sidhani kama wangethubutu kuunda katiba inayowakandamiza Waislaam kwa kuwapendelea wakristu au kama ingekuwa na wanawake wengi basi haki za wanaume zingepunguzwa. Fikra hizi zinanifanya niamini kwamba hara rais kuwa muislaam ni issue kwa baadhi ya watu na tutayaona haya uchaguzi wa mwaka 2015 - Amini maneno yangu!

Kinachoendelea hapa JF ni fikra finyu sana, ni conspirancy theory kama mwandishi wa hadithi ya sinema au kitabu cha fiction maana sioni tatizo Zanzibar kuwa na wajumbe wengi kuliko bara ama bara kuliko wale wa Zanzibar na huo uuwiano wenu unaweza vipi kusaidia dini za watu kutumika ktk kuitunga katiba ya nchi. Wala sii kweli JK alishindwa kusema CUF ni chama cha kidini ikiwa chama hicho kimekwisha kisiwa hivyo kwa miaka 9 toka mwaka 2000 na kumalizwa kabla hata ya uchaguzi wa mwaka 2010. Jamani, Chadema ni miaka miwili tu tunaanza kuteteleka tunaweza kweli kusimama hadi 2015..

Tusitake sana kutafuta mchawi maana wachawi ni sisi wenyewe kiimani, na hakika kwa fikra kama hizi basi Tanzania bado tuna miaka 200 mingine ya kuwa na hata ustaraabu (civilization) maana unapofikiria mwenzako atafanya hivi kama ataachiwa nafasi basi vile vile kumbuka mwenzako naye hatakuwa na imani nawe na maadam hatuaminiani ina maana hatuna UTU. Na kama watawekwa watu kwa uuwiano wa dini basi bila shaka watavutana kwa maswala ya dini zao kwa maslahi ya dini zao - huu ndio Udini at the making.

Hili sio lengo la kuundwa kwa katiba mpya hata kidogo na kuendeleza hoja ya uuwiano ni kulikuza jambo hili makusudi kwa sababu JK ni muislaam, sioni sababu nyingine hata kidogo na kama angekuwa Mkapa ndio kachagua wajumbe hawa wala tusingefika hapa tulipofika maana miaka ya nyuma Nyerere aliwashirikisha Wazanzibar nusu ktk kuunda Muungano, Azimio la Arusha na hata katiba ya mwaka 1977 haikuwa hoja.
 
Naona wanazi wa chadema wanajaribu kumpaka "lipstick nguruwe", hata awe na midomo myekundu namna gani kama "miss world" atabaki kuwa nguruwe- kauli ya mtei ni kauli "divisive", "discriminatory", "hate inspiring", "islamophobic". Kiufupi ni kwamba kwa mtu mwenye status yake katika jamii hapaswi kutoa kauli kama hiyo hasa ukizingatia katika historia yake ya utumishi wa umma hakuna rekodi yoyote ile aliyowahi kushutumu bosi wake nyerere kuchagua wakiristo wengi kwenye serikali kuliko waislamu, au hata yeye katika chama chake kuwa na uwakilishi wowote unaobalance kidini, sana sana chama chake kina stracture ambayo wakiristo ni wengi sana kuliko waislamu.
Kama kweli Kikwete hapendi hili taifa liparaganyike avunje hii tume haraka sana. We gamba la nyoka huwezi kufananisha uteuzi wa tume itakayoratibu maoni ya kuunda katiba mpya na uteuzi mwingine. Je ni nani atakayeamini kuwa hawatachakachua maoni ya wengi kwa maslahi ya wana tume? Mi nawaamini lakini kwa wingi huu uliokithiri utafanya wakristu waone kuwa ni ya kiupendeleo, na kitakachozaliwa kitakataliwa na wakristu ambao ni wengi na hivyo huenda tukashindwa kupata katiba mpya.
TUACHE UNAFIKI,. TANZANIA UDINI UPO NA UKITAKA KUJUA SIKILIZA REDIO IMANI NA KUSOMA MAGAZETI YA EL-NUUR.
PIA WAISLAMU WENGI WANAICHUKIA CHADEMA ETI KWA SABABU MWENYEKITI NI MKRISTU, huu pia ni UDINI.
 
Kwa udini huu wa JK natabiri watanzania kuingia vitani b4 2015.

mi hapa nadhani mtei ndio MDINI...! na kwa hili tumewapa magamba chance ya kuthibitisha kauli yao cdm ni chama cha kidini... kama katika hii nchi kila jambo tukiangalia wakristo wangapi ... waislam wangapi...! then itakuwa ni balaa! ....

zanzbar tuseme 98% ni waislam! wabunge wao wote waislam sababu wananchi wanaowachagua ni waislam! sasa sijui wenzangu mliitaka kwa upande wa znz awekwe mkristo hata kama sifa.


Alichokosea mtei nadhani amesahau hapa ni nchi mbili .. Tanzania bara na visiwani..! leo hii wenzetu waislam wa tanzania bara wakianza kulalamika mbona upande wa bara huku kwetu wakristo wengi kuliko waislam! tutafanikisha kweli hili jambo...

mbona jamani tunataka kurudishana Nyuma.!!!:yell::yell:
 
mi hapa nadhani mtei ndio MDINI...! na kwa hili tumewapa magamba chance ya kuthibitisha kauli yao cdm ni chama cha kidini... kama katika hii nchi kila jambo tukiangalia wakristo wangapi ... waislam wangapi...! then itakuwa ni balaa! ....

zanzbar tuseme 98% ni waislam! wabunge wao wote waislam sababu wananchi wanaowachagua ni waislam! sasa sijui wenzangu mliitaka kwa upande wa znz awekwe mkristo hata kama sifa.


Alichokosea mtei nadhani amesahau hapa ni nchi mbili .. Tanzania bara na visiwani..! leo hii wenzetu waislam wa tanzania bara wakianza kulalamika mbona upande wa bara huku kwetu wakristo wengi kuliko waislam! tutafanikisha kweli hili jambo...

mbona jamani tunataka kurudishana Nyuma.!!!:yell::yell:
Mkuu ni kawaida yetu kusahau na kuchangia bila kujali mada halisi ya mleta hoja.

Soma posti ya kwanza halafu majibu ama maswali yako yatokane na hoja zake.

Kwamfano umebakia kumwita mzee Mtei mdini na wakati hujasema kama ni kweli ama si kweli kuwa mawazo ya Ar-nuur yameonekana kufuatwa?

Na kama ingekuwa the other way around, yani wangekuwa wakristo wengi zaidi, si kungekuwa na malalamiko?

Hata wenye kusema Tanganyika tume ina wakristo wengi, waki balance hilo na Zanzibar watabalance?

Kuna maswali kama hayo ambayo yanauathiri uhusiano wa muungano wetu na usalama wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom