mkuu ni kawaida yetu kusahau na kuchangia bila kujali mada halisi ya mleta hoja.
Soma posti ya kwanza halafu majibu ama maswali yako yatokane na hoja zake.
Kwamfano umebakia kumwita mzee mtei mdini na wakati hujasema kama ni kweli ama si kweli kuwa mawazo ya ar-nuur yameonekana kufuatwa?
Na kama ingekuwa the other way around, yani wangekuwa wakristo wengi zaidi, si kungekuwa na malalamiko?
Hata wenye kusema tanganyika tume ina wakristo wengi, waki balance hilo na zanzibar watabalance?
Kuna maswali kama hayo ambayo yanauathiri uhusiano wa muungano wetu na usalama wake.
jmushi1 usiwe mpenzi wa mtu/dini vikakufanya kuwa blind!- maana ya busara ni kutenda, kunena mambo fulani kwa akili na kwa wakati wake, ukweli peke yake siyo justification kutamka mtu!. Mathalani jambazi wanavamia nyumba yenu na mzee anajificha chini ya uvungu, wanakuuliza mzee yuko wapi, kuwa honest, wewe utawaeleza mzee alipo eti kwa sababu unasema ukweli?- je katika familia mathalani unakuja kudokezwa siri kwamba mmoja wa ndugu zako siyo mtoto wa baba yako, siku mgeni akitembelea kwenu akakuomba utambulisho wa ndugu zako utasema ukweli "kwamba lakini huyu fulani si mtoto wa baba, mama alipitia nje?".
Kuna wakati mwalimu nyerere akiitolea ufafanuzi ishu za uteuzi wa viongozi kwenye serikali yake akasema kwamba kipindi wakati huo anateua alikuwa haangalii kabisa dini zao, bali alikuwa anaangalia utendaji wao- ni dhahiri basi wakati huo kwa watu wenye muono kama wa mzee mtei, walikuwa wanaona nyerere mdini.
Jmushi1 tumeshaona teuzi nyingi nchini, kuanzia wagombea ubunge, wakuu wa mikoa, mabalozi, tume zilizopita na nakuhakikishia mara nyingi sana wakiristo ni wengi kuliko waislamu, hebu niambie honestly baadhi ya waislamu walipokuwa wakilalamika wamekuwa wakijibiwaje?- kwamba wamesema ukweli na hivyo wako sawa, au kwamba teuzi haziangalii dini bali utendaji?
Usiwe blind jmushi1- udini ni pale unapoliangalia kila jambo kidinidini wakati kumbe huyo unayemdhania anatenda udini wala hafikirii kabisa jambo hilo.
Unazungumzia kubalance kati ya waislamu na wakiristo kwa pande zote mbili. Hebu piga mahesabu mwnyewe, tanzania bara kwa logic yako ilistahili waislamu wengi zaidi ya hao iliowapata maana inasemekana waislamu wa tanganyika ni almost sawa na wakiristo na kuna sehemu nyingine nimesoma wanasema waislamu ni wengi kidogo kuliko wakiristo.
Zanzibar ukiangalia percentagewise ni dhahiri hata ukijaribu kubalance yaani utakuta waislamu bado ni wengi kuliko wakiristo. Cheki mwenyewe kwa kuchukua 1% uzidishe na wajubmbe kutoka zenji uone watakuwa wangapi dhidi ya wale 99%.
At the end of the day tukifanya haya mambo kidinidini, kwa kuwa kila upande wa muungano unatoa wajumbe kwa usawa, always waislamu watakuwa wengi kuliko wakiristo kutokana na factor ya zanzibar. Lakini tukifuata vigezo vingine tofauti, sura ya teuzi inaweza kuchukua form ya aina yoyote ile.