Mtei kasema UKWELI ULIOSHINDWA KUTAMKIKA, tuache unafiki!

Mtei kasema UKWELI ULIOSHINDWA KUTAMKIKA, tuache unafiki!

Tume ya Katiba mpya na Agenda ya Siri ya Mahakama ya Kadhi tanzania bara! Chezea baba Riz wewe!
 
Ukitaka kuanza kuteua kwa kuangalia idadi sawa ya udini basi huo ndio mwanzo wa udini, haiwezekani mtu ashindwe kuteua watu flan hata kama wanauwezo eti kisa ni wa dini flan, raisi kateua tume kulingana na uwezo wa mtu husika suala la dini umeliona wewe na mtei baada ya kuanza kuhesabu wateuliwa kwenye hiyo tume na ulipoona wengi ni waislam basi ukakurupuka na hoja udini, vipi ungekuta wakristo ni wengi ungesema? au babaako mtei angesema?

Hoja ya idadi ya wajumbe kwa imani zao ilitolewa mwanzo na balaza la maimamu na radio imani na magazeti ya el-nuur

Pili je nisahihi waislam kuomba 50% bara wakati idadi yao ni chini ya 20% bara. Mikoa yenye waislamu wengi kwa bara ni Tanga, pwani, Mtwara, Lindi tu. Dar kunawageni wengi sasa idad ni sawa. Vip 50%?

Uliza maustadhi wakuambie habari za Marca. Mwanzo waislamu walikuwa 20% na mtume akaongoza kuandikwa katiba maswala ya uongozi kwa idadi hayakuwepo swala ni kuaminiana.

Inshu hapa ni kwamba kunabaadhi ya madai yasiyo ya haki ambayo baadhi ya wasioelewa uislamu wanayapigania
Mfano: Mahakama ya kadhi si kitu kibaya kama wengi wanavyodhani kwani inahusu mashwala ya miradhi na ndoa kwa waumini wa kieslamu tu. Ila ubaya wanataka Majengo, Mahakimu na uendeshwaji ugaramiwe na selikali. Je waislamu wachamungu hawawezi kuchangia uendeshwaji wake?

Kuna inshu za Shule za sec za selekali zilizokuwa za makanisa kama Nganza, Nsumba, Kahororo na Minaki zina Makanisa ya zamani pia. Wanalazimisha zijengewe misikiti na selikali! Je waumini wanafunzi wa makanisa mengine
yasifungamana na kanisa lililopo wajengewe makanisa pia? Na wakristo wakidai shule zao itakuwaje.

Kuna inshu ya misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini zinazotoa huduma na haziko kibiashara kama Hosptal za Bugando, KESMC, Aghakani tena zinaudumia bila ubaguzi wa dini. Eti nao wanaomba wapate fear hizo japo hawana hosptal. Ila wanauza jina la BAKWATA kwa wafanyabiashara ili wakwepe kodi. Hizo za BAKWATA misikiti haijui ata uendeshaji wake. NaUNAFIKI WA MKULO HUKU AKIJUA HILI AKAJA NA MPANGO WA KUTOA MSAMAHA WA KODI kwa asasi za makanisa.

WASIOJUA WANAPOTOSHA JUU YA IMANI YA UISLAMU.
Ukifuatilia historia ya MTUME Alipenda amani. Fuatilia juu ya uundwaji wa katiba ya maka. Aliheshimu watu wote. Alitumia busara sana na si nguvu.

Narudia chimbuko la dini zote mbili ni IBRAHIMU. Ila wote tu wamoja ni bora tuungane tupambane na maadui wa kweli UJINGA UMASIKINI RUSHWA MAOVU KATIKAJANII MFUMO MBOVU WA ELIMU TOFAUTI KUBWA ZA KIPATO UONGOZI MBAYA.

Nchi inayumba kwa uteuzi usizingatia uwezo bali urafiki udini na matabaka.
ONA MUSTAPHA mkulo uchumi hoi
OMARI NUNDU na mgomo wa madaktari
VUAI NAHODHA na magari ya maji ya kuwasha na kupiga raia
ELIMU walimu madai yasiyoisha na kufaulu wasiojua kusoma na ajira za walimu mpaka maandamano

OMARI NUNDU wapi Meli Ndege na Reli?
Ngeleja? Labda H Mwinyi
UMEFIKA WAKATI WA KUHOJI LAZIMA TUHOJI

Omar Nundu na mgomo wa Madaktari wapi na wapi?
 
jmushi1 usiwe mpenzi wa mtu/dini vikakufanya kuwa blind!- maana ya busara ni kutenda, kunena mambo fulani kwa akili na kwa wakati wake, ukweli peke yake siyo justification kutamka mtu!. Mathalani jambazi wanavamia nyumba yenu na mzee anajificha chini ya uvungu, wanakuuliza mzee yuko wapi, kuwa honest, wewe utawaeleza mzee alipo eti kwa sababu unasema ukweli?- je katika familia mathalani unakuja kudokezwa siri kwamba mmoja wa ndugu zako siyo mtoto wa baba yako, siku mgeni akitembelea kwenu akakuomba utambulisho wa ndugu zako utasema ukweli "kwamba lakini huyu fulani si mtoto wa baba, mama alipitia nje?".

Kuna wakati mwalimu nyerere akiitolea ufafanuzi ishu za uteuzi wa viongozi kwenye serikali yake akasema kwamba kipindi wakati huo anateua alikuwa haangalii kabisa dini zao, bali alikuwa anaangalia utendaji wao- ni dhahiri basi wakati huo kwa watu wenye muono kama wa mzee mtei, walikuwa wanaona nyerere mdini.

Jmushi1 tumeshaona teuzi nyingi nchini, kuanzia wagombea ubunge, wakuu wa mikoa, mabalozi, tume zilizopita na nakuhakikishia mara nyingi sana wakiristo ni wengi kuliko waislamu, hebu niambie honestly baadhi ya waislamu walipokuwa wakilalamika wamekuwa wakijibiwaje?- kwamba wamesema ukweli na hivyo wako sawa, au kwamba teuzi haziangalii dini bali utendaji?

Usiwe blind jmushi1- udini ni pale unapoliangalia kila jambo kidinidini wakati kumbe huyo unayemdhania anatenda udini wala hafikirii kabisa jambo hilo.

Unazungumzia kubalance kati ya waislamu na wakiristo kwa pande zote mbili. Hebu piga mahesabu mwnyewe, tanzania bara kwa logic yako ilistahili waislamu wengi zaidi ya hao iliowapata maana inasemekana waislamu wa tanganyika ni almost sawa na wakiristo na kuna sehemu nyingine nimesoma wanasema waislamu ni wengi kidogo kuliko wakiristo.

Zanzibar ukiangalia percentagewise ni dhahiri hata ukijaribu kubalance yaani utakuta waislamu bado ni wengi kuliko wakiristo. Cheki mwenyewe kwa kuchukua 1% uzidishe na wajubmbe kutoka zenji uone watakuwa wangapi dhidi ya wale 99%.

At the end of the day tukifanya haya mambo kidinidini, kwa kuwa kila upande wa muungano unatoa wajumbe kwa usawa, always waislamu watakuwa wengi kuliko wakiristo kutokana na factor ya zanzibar. Lakini tukifuata vigezo vingine tofauti, sura ya teuzi inaweza kuchukua form ya aina yoyote ile.
Mkuu naomba unielewe.Ukweli unaouzungumzia wewe ambao umeutolea mifano kadhaa siyo sawa na ukweli ninaouzungumzia mimi.

Nilichozungumzia mimi, ni ukweli ambao unaweza kulinusuru Taifa.Tukiacha unafiki tutafanikiwa.

Wakati mjadala huu unaanza kwenye ile original post ya Mzee Mtei, niliuliza kama katiba tunayoitafuta ni ya Tanganyika, Zanzibar ama Tanzania?

Kwasababu mimi sijali kuhusu wajumbe wa Tanganyika wala wale wa Zanzibar, mimi najali kuhusu wajumbe wa tume ya katiba ya Tanzania, na tume hiyo ni kweli ina asilimia kubwa ya watu wa dini moja, hilo wala halihitaji "special gogles" or "binoculars" to see.

Haya ya kutaka kuwepo usawa sikuyaanzisha mimi.Na wala sikusema kuwa tuchaguwe wajumbe ambao ni wanasiasa peke yake.

Katiba ni ya wananchi na si baadhi ya wanasiasa, huo ulikuwa msimamo wa wengi wetu humu jf, nyie wenye vyama ndo mlisababisha mvutanao uwe wa kivyama vyama zaidi.

Ya kutaka usawa, yalianzishwa na wengine na yanapigiwa kelele kilu siku, even humu ndani.

Mwalimu Nyerere alikabiliana na issue hii kwa tofauti pia, lakini kwa mwelekeo ule ule wa "kuleta usawa". Hilo lipo, lilikuwepo na litaendelea kuwepo.

Ukweli ni kwamba kama wajumbe wote in total wangekuwa ni wakristo, basi lazima kelele zingepigwa pande zote.

Ninaamini mjadala huu utasaidia wengi wetu kutambua umuhimu wa kutokuangalia dini, wale watu tunaowapigia kelele za udini humu ndani, mtajuwa sasa how it feels to be on the "other side"

Kama mnataka kweli tujenge Tafa, basi tujenge Taifa na si unafiki!
 
Mkuu JM1 nimemuita mdini rejea kwenye ule uzi wake .. nadhani post yangu ilikuwa ya 3 kupingana na kile alichokiandika na pia serikali ni kubwa sana, serikali sio JK peke yake, wala wabunge wake, mpaka JK ametua yale majina kutakuwa na vigezo alivyopitia na sidhani serikali huwa inaendeshwa kwa maoni ya waandishi wa magazeti ..! mwandishi wa ar-nuur hakutoa mawazo yoyote zaidi ya maoni yake yeye mwenyewe na kanzu yake aliyovaa hiyo siku akiandika yale maoni yake.





Of course kwa tanzania bara tume ina wakristo wengi kuliko waislam...?! je umesikia ndugu zetu waislam wabara wakilalamika..?! sababu wenyewe wanapigania kadhi upande wa bara .... nadhani sasa wame giveup . hapa usiichukulie tanzania kama nchi moja. chukulia tanzania ni muungano wa NCHI MBILI TOFAUTI.



sijajua ni vigezo gani vimetumia kuchagua ila nadhani kigezo kimoja ni uzoefu katika nyanja ya siasa na sheria!... Je jiulize politicians wa kizanzibari kuna mkristo..?! kama wapo ni wangapi.. you can not just pick any one from michenzani streets just bcz his name is joseph and he is zanzbarian kumbuka majority ya wazanzibar ni tuseme 98% ni waislam Je mkuu inamaana ulitarajia hili jambo lichukuliwe kidini zaidi ya vigezo!. Na pia nina uhakika majina kutoka zanzbar yalipendekezwa na wazanzibar wenyewe.. maybe kupitia baraza lao la wawakilishi..!? udini wa JK unaingia wapi hapo..?!

kumbuka zanzibar ni nchi sidhani kama wangekubali JK mwenyewe awataulie yale majina bila serikali ya mapinduzi ya zanzbar kuwa consulted first! so majina yaliotoka zanzbar yamependekezwa na wazanzbar wenyewe ambao asilimia kubwa ni wa dini moja.

Chadema kama kweli tunahitaji kuiondoa CCM madarakani.... basi kuna vitu vinatakiwa kuwa adjusted .... aim glad viongozi wa CDM walitoa tamko wakasema yale ni maneno ya MTEI na wala si msimamo wa chama kwani it was totaly very low from him.

Mzee Mtei namkumbusha maneno ya Mahatma Gandhi and i quote "I suppose leadership at one time meant muscles; but today it means getting along with people"hapo kwenye RED panahusika sana
Mkuu umeingia mtegoni tena, najua ulisema mzee Mtei ni mdini kwenye ile thread yake mwanzoni, lakini umesahau kwenye uzi huu kuna issue ya "mpinga dini" vs. "mpinga udini"

Ni vyema kabisa kama ukijibu bandiko ambalo umeelekeza kwenye posti ya kwanza, uhakikishe ni angle ya tofauti ambayo mleta mada hajaigusia, hilo litasaidia kutokuwepo na duplicates.Na pia kupata a constructive dissussion.

Pia unauliza kama ndugu zetu wa bara hawakulalamika basi ni sawa.

Nilishauliza hapo nyuma kuhusu katiba tunayoitafuta kuwa ni ya Tanzania na si Tanganyika wala Zanzibar, kwenye tume ya katiba ya Tanzania, kuna waislam wengi, hilo liko wazi, je hayo ni mazingira ya kuwafanya wasilam bila kujali walikotoka (either Zanzibar ama Bara)walalamike?
Jibu unalo...

Hayo ya kuhusu "majority" Zanzibar, umeshajibiwa kwa namna nyingi tu, hata posti ya kwanza uisome vyema zaidi itasadia mkuu.

Kwenye kuhusu chadema kutoa tamko la kuyakana maneno ya Mtei, hayo ni yao ndani ya chama chao, mimi bado sina chama.
 
Wengi tumejitenga na ukweli unaouzi. Katika kuunda tume ya katiba JK Ameshindwa kuepuka shinikizo la Redio Imani na Gazeti la al-nuur.

Ubaya tumefundishwa kuchukia DINI na si UDINI! MFANO chadema kinaitwa chama cha kikristu kwasababu tu uongozi wake wa juu unawakristo wengi.

Lakini CUF kimejaa waislamu wengi toka miaka ya tisini lakini JK hakukiusisha na udini! Unajua ni kwanini ni mpinga dini na si udini!

Tunataka kuaminishwa kuwa adui mkubwa wa mwislamu ni mkristo na adui mkubwa wa ukristo ni mwislamu. Tunasahau kuwa uislamu na ukristo asili yake ni moja Ibrahimu. Tunataka kuwasahau maadui tunaopambana nao ni walewale Ujinga, Umasiki, Maradhi na Rushwa.

Ubaya tumeitupa ELIMU tukaaminishwa UJINGA tukashindwa kuutambua ukweli. Majizi yanachangia makanisa na misikiti kwenye arambee tunayaona kama marafiki.

Mawazo ya Ar-nuur na Redio Imani ambayo ni msingi wa uteuzi wa tume;-
Tume iundwe na nusu ya wajumbe kutoka bara na nusu kutoka zanzibar(bila kujari ukubwa na idadi ya watu kutoka pande hizo). Na hili tundulisu alilipinga vikali akaonekana Mjinga.

Wajumbe kutoka zanzibar wawe waislamu wote sababu zanzibar ni nchi ya kiislamu na wajumbe kutoka bara wawe nusu wakristo nusu waislamu sababu ndio dini kuu kwa huku bara. Na kutowatambua kabisa wasio na dini.

Kwa mchanganuo huo maslai ya waislamu yataingia kwenye katiba mpya. Kwani 75% ya wajumbe watakuwa waislamu na25% tu ndio wawe wakristo. Ila moja ya dai kuu la waislamu ni nafasi sawa za uongozi, mahakama ya kadhi na kupinga mfumo kristo. Hawana habari juu ya ufisadi mfumo mbovu wa elimu, huduma duni za afya, rushwa na mfumuko wa bei.

Katika kuteua tume JK Kazingatia maoni ya media za kiislam. Je anaamini kama wao au ni kupunguza mashinikizo ya waislamu zidi yake.

Ata katika uteuzi wa majaji, wakuu wa mikoa na wilaya, mawaziri JK ujitaidi kuzingatia hili. Hii ni hatari! Tuzingatie uwezo tu.

Sioni tatizo atakama jk angeteua waislamu wote ila tu wawe na uwezo.
PILLI NATOARAI WATUMBE WA TUME WAANGALIE MASLAI YA TAIFA NA SIO DINI ZAO KWAN UMA HAUTAWEZA KUKAA KIMYA

So ******* unaumia na kitu ambacho you can do nothing about it;
 
Mitazamo ya kidini ya akina Mzee Mtei na William Mushumbusi zinasikitisha sana. Hata kama Mtei si kiongozi wa CDM bado ana kofia ya uasisi na anawakilisha identity ya CDM.

Nautazama upya uungaji mkono wangu kwa Chadema. Huenda nikatengua msimamo wangu wa ki-People's Power. Aidha sitaiunga mkono CCM.
 
Wapo waliotafsili vibaya Mada hapo juu nimeonesha wazi kuheshimu dini zote mbili

Nimeonesha umuhimu wa kuaminiana

nimesema sioni tatizo atakama wajumbe wa tume wangekuwa waislamu wote ila tu ni wale wenye uwezo

Wasiwasi nilioonesha ni kwamba kwanini mawazo ya media za kiislam yachukuliwe yote yaliyoleta over 70% kuwa waislamu.

Nimeuliza pia jk anaamini kama wao au anaogopa shinikizo

Je nikwanini utaratibu wa kuteua kwa jk kwa kulinganisha udini kumeanza toka kwenye wizara, majaji hadi tume

Pia niliitimisha kwa kuwaomba wajumbe waangalie taifa na si dini zao kwani kitanuka

na niliuliza kwanini chadema ambay uongozi wa juu una mchanganuo
Mwkt Mkristo
Makam mwkt zanz Mwislam
Katibu mkuu mkristo
Naib ktb Mwislam
kinausishwa na ukristo Wakati CUF full waislam lkn akihusishwi na waislam
Mi si mnafiki ila mi sio MWANACHADEMA NA BADO SIJAONA HARAKATI ZINAZONISHAWISHI KUJIUNGA CHADEMA naomba maoni yangu yasihusishwe na cdm uwa inanikera sana
 
tatizo la hapa Tanzania mahala ambapo atateuliwa muislamu kuongoza lazma waseme ni udini lakin wakiwa ni wakristo hamsemi kwann mnapenda hizi chokochoko zisizo na mantiki?. Udom vc muislamu kapata lawama sana za udini, mzumbe udsm na kwingineko viongozi ni wakristo so waislam hawafai kuongoza ofisi zzte?.
 
tatizo la hapa Tanzania mahala ambapo atateuliwa muislamu kuongoza lazma waseme ni udini lakin wakiwa ni wakristo hamsemi kwann mnapenda hizi chokochoko zisizo na mantiki?. Udom vc muislamu kapata lawama sana za udini, mzumbe udsm na kwingineko viongozi ni wakristo so waislam hawafai kuongoza ofisi zzte?.

Ni second citizen.
 
Rais wa jamuhuri ya muungano, makamu wake, jaji mkuu, waziri wa ulinzi, mambo ya ndani, mambo ya nje, fedha na wizara zote nyeti, wakurugenzi wa idara nyeti serikalini, ushahidi upo; nenda smz yote, wote ni waislam. Mbona wakristu hawalalamiki? Mbona JK unataka kutuletea balaa? Kumbuka wakristu kukaa kimya si ujinga kwani kimya kingi kina mshindo.

Haya yote uliyoyasema Waislam wakiyalalamikia huwa mnawaambia hawakusoma kwa hiyo wajibibidishe na elimu. Sasa na nyie yamewakuta yepi? Mimi nadhani wakati umefika kwa Wakristo wawekeze zaidi kwenye elimu ili wasizidi kubaguliwa badala ya kulalamika tu. Wakati Waislam wanaenda shule nyie mlikuwa mnakazana kulishana sakramenti na kupeana kipaimara. Mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu mchungu. Na bado mtatia sana akili.
 
kwasababu mimi sijali kuhusu wajumbe wa tanganyika wala wale wa zanzibar, mimi najali kuhusu wajumbe wa tume ya katiba ya tanzania, na tume hiyo ni kweli ina asilimia kubwa ya watu wa dini moja, hilo wala halihitaji "special gogles" or "binoculars" to see.

(1) je kuna ubaya wowote kwa tume kuwa na asilimia kubwa ya WAJUMBE WAISLAMU ?

(2) je, waislamu walio wengi katika tume wakisaidia katika kuunda katiba, je hiyo katiba itacease kuwa ya tanzania?

(3) ni kipi teuzi kinaifanya tume hii iwe ya kidini wakati nchi hii imeshafanya teuzi nyingi sana "kwa ajili ya tanzania" lakini hazifanyi teuzi hizi kuwa za kidini?.

(4) je siyo kweli kwamba teuzi nyingi nchini tokea uhuru wakiristo ndiyo wengi katika teuzi hizo?- je mwalimu nyerere muasisi wa teuzi za namna hii alikuwa mdini?.

(5) Usiwe kama Layman, ambaye eti kwa kuwa wenzake wanafanya basi na yeye anafanya: hoja yako eti LAITI TUME INGEKUWA NA WAKIRISTO WOTE TUSINGELALAMIKA?- Jibu ni kwamba WANGEKUWA WAKIRISTO WENGI, WALA ISINGEKUWA ISHU MAANA TUMEISHAIZOEA HALI HIYO. HOJA YAKO HAINA MSHIKO MAANA RAISI HAJACHAGUA "WOTE" WAISLAMU, BALI KACHAGUA "WENGI" WAISLAMU. MBONA TEUZI ZAKE NYINGI TU KATEUA "WENGI" WAKIRISTO NA WALA EDWIN MTEI AU JMUSHI1 HAMJATOKEA KUKEMEA?

(6) JE BWANA JMUSHI1 ULITAKA ATLEAST ASILIMIA YA WAISLAMU IWE NGAPI KATIKA TUME?
 
Nchi hii udini unaletwa na Wakristo hasa Wakatoliki. Wao wanaamini kuwa nafasi zote za uongozi nchi hii ni haki yao. Waislam ni raia daraja la pili. Wizara au ofisi ikiwa na Waislam watano na Wakristo wanne hapo pana udini. Ofisi ikiwa na Wakristo ishirini na Mwislam mmoja hapo ni sawa na hakuna anayelalamika. Kama mnaona kila anachofanya JK anawapendelea Waislam basi na tugawane nchi mkae huko ambako nafasi zote zitakuwa zenu peke yenu.

Pia, kuna ajenda dhahiri zinazoendelea hivi sasa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kutaka kuonyesha kuwa Waislam hawawezi kuongoza. Angalia idadi kubwa ya viongozi na mawaziri wanaosakamwa ni Waislam kana kwamba mawaziri wote Wakristo ni watendaji wazuri. Kwenye Wizara ya Nishati na Madini badala ya kulaumiwa Ngeleja ambaye ndiye Waziri kamili wanalaumiwa Malima na JK. Kazi kwelikweli!
 
nikiwasikiliza akina ali kiba, juma nature nk kitu cha kwanza kinachoingia akilini ni kipaji/radha ya mziki...nikiwaangilia akina ngasa,maftah au wale akina dada wa twiga stars: fatuma bushiri,mwajuma abdalla,fatuma omari,asha rashid,fadhila hamad nk huwa hata sioni dini zao bali ushindi wao ambao huwa unatupa burudani na kutuunganisha watanzania wote kwa furaha tukishangilia pamoja...hivi inashindikana nini kuwaangalia viongozi wetu wa serikali/kisiasa kwa jicho hilihili la 'utanzania' tunalolitumia kuiangalia twiga stars? kincho matter ni uadilifu au dini ya mtu?
 
Mzee Mtei has a full right to give out his opinions because he is a tanzanian like others and he should speak out what he saw is ok to say. It is true that the commision comprising a lot of muslim members even if you argue against this point but the truth remain the same. Let us now give them assistance while awe re taking care, once we see there is some sort of religiouslism tanzanians dont hestate to revoke out, dont be silence for things which may put our country into controvercial. GOD BLESS TANZANIA.

Duh! Hichi Kiengereza cha kutafsiri kutoka Kiswahili ni taabu kweri kweri!!!!!
 
Haya yote uliyoyasema Waislam wakiyalalamikia huwa mnawaambia hawakusoma kwa hiyo wajibibidishe na elimu. Sasa na nyie yamewakuta yepi? Mimi nadhani wakati umefika kwa Wakristo wawekeze zaidi kwenye elimu ili wasizidi kubaguliwa badala ya kulalamika tu. Wakati Waislam wanaenda shule nyie mlikuwa mnakazana kulishana sakramenti na kupeana kipaimara. Mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu mchungu. Na bado mtatia sana akili.

Na kuimba kwaya.... Nibeeeeebe, nibebe!
 
Wengi tumejitenga na ukweli unaouzi. Katika kuunda tume ya katiba JK Ameshindwa kuepuka shinikizo la Redio Imani na Gazeti la al-nuur.

Ubaya tumefundishwa kuchukia DINI na si UDINI! MFANO chadema kinaitwa chama cha kikristu kwasababu tu uongozi wake wa juu unawakristo wengi.

Lakini CUF kimejaa waislamu wengi toka miaka ya tisini lakini JK hakukiusisha na udini! Unajua ni kwanini ni mpinga dini na si udini!

Tunataka kuaminishwa kuwa adui mkubwa wa mwislamu ni mkristo na adui mkubwa wa ukristo ni mwislamu. Tunasahau kuwa uislamu na ukristo asili yake ni moja Ibrahimu. Tunataka kuwasahau maadui tunaopambana nao ni walewale Ujinga, Umasiki, Maradhi na Rushwa.

Ubaya tumeitupa ELIMU tukaaminishwa UJINGA tukashindwa kuutambua ukweli. Majizi yanachangia makanisa na misikiti kwenye arambee tunayaona kama marafiki.

Mawazo ya Ar-nuur na Redio Imani ambayo ni msingi wa uteuzi wa tume;-
Tume iundwe na nusu ya wajumbe kutoka bara na nusu kutoka zanzibar(bila kujari ukubwa na idadi ya watu kutoka pande hizo). Na hili tundulisu alilipinga vikali akaonekana Mjinga.

Wajumbe kutoka zanzibar wawe waislamu wote sababu zanzibar ni nchi ya kiislamu na wajumbe kutoka bara wawe nusu wakristo nusu waislamu sababu ndio dini kuu kwa huku bara. Na kutowatambua kabisa wasio na dini.

Kwa mchanganuo huo maslai ya waislamu yataingia kwenye katiba mpya. Kwani 75% ya wajumbe watakuwa waislamu na25% tu ndio wawe wakristo. Ila moja ya dai kuu la waislamu ni nafasi sawa za uongozi, mahakama ya kadhi na kupinga mfumo kristo. Hawana habari juu ya ufisadi mfumo mbovu wa elimu, huduma duni za afya, rushwa na mfumuko wa bei.

Katika kuteua tume JK Kazingatia maoni ya media za kiislam. Je anaamini kama wao au ni kupunguza mashinikizo ya waislamu zidi yake.

Ata katika uteuzi wa majaji, wakuu wa mikoa na wilaya, mawaziri JK ujitaidi kuzingatia hili. Hii ni hatari! Tuzingatie uwezo tu.

Sioni tatizo atakama jk angeteua waislamu wote ila tu wawe na uwezo.
PILLI NATOARAI WATUMBE WA TUME WAANGALIE MASLAI YA TAIFA NA SIO DINI ZAO KWAN UMA HAUTAWEZA KUKAA KIMYA

Huyu Mtei ana matatizo ya Udini pamoja na ukabila,kimsingi unapotaka kutoa tamko kama hili lazima ufanye utafiti kwanza kabla ya kuanza kulaumu.angeanzaza kutafuta data za uwiano wa kidini wa baraza la mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi,wakuu wa mikoa na viongozi wengine wote ambao wanateuliwa na Rais.Huyo hana loloe anataka kutumia mwamvuli wa udini kukijenga chama chao cha kichaga cha Chadema. Nchi hii idadi ya waislamu ni wengi kuliko wakristo(angalia world fact book) lakini kutokana na mfumo kristo maslahi ya waislamu yanapuuzwa na wanaonekana hawastahili kitu chochote hapa bongo.
 
Wana JF Nilikwishasema siku nyingi Rais Jakaya Kikwete is not serious watu wengi wanadhani ni utani niko serious huyu Mdini Juha Kalulu(JK) yuko tayari kufa kwa Jihad. Badala ya kuangalia mambo kwa upeo analeta uswahili na Utani kwenye jambo zito katiba ya Nchi. Kwenye hili sheria ilikosewa and I stand to be corrected. Zanzibar sio nchi you can't have 1.5 million people balanced with 45 million. Labda kama utatumia Makalio kufikiria Kama alivyosema Masaburi! Narudia uteuzi aw this useless tume utakuja kuwatokea puani it's just a matter of time . Tumeanza safari kwa mguu wa kushoto hatutafika tutaishia jangwani Kama ilivyokuwa furaha ya nyani. We actually need a to undertake a military take over tuanze kuhesabu kwa vijiti. Where is my AK 45 tuanzie porini hii politic shall take us back to square one!

Muda mrefu mliwaburuza waislamu na mlifanikiwa kupitia Dikteta Nyerere, sasa mjinga amerevuka .Tanganyika iliungana na nchi iitwayo Jamuhuri ya Watu wa Zanzibar. Urefu, upana ,ukubwa na udugo sio kigezo cha nchi. Kama kweli wewe ni mkereketwa, basi huu ndio wakati wa kudai kurudishwa kwa Tanganyika. Vinginevyo acha unafiki na udini usio na mshiko...
 
Naona wanazi wa chadema wanajaribu kumpaka "lipstick nguruwe", hata awe na midomo myekundu namna gani kama "miss world" atabaki kuwa nguruwe- kauli ya mtei ni kauli "divisive", "discriminatory", "hate inspiring", "islamophobic". Kiufupi ni kwamba kwa mtu mwenye status yake katika jamii hapaswi kutoa kauli kama hiyo hasa ukizingatia katika historia yake ya utumishi wa umma hakuna rekodi yoyote ile aliyowahi kushutumu bosi wake nyerere kuchagua wakiristo wengi kwenye serikali kuliko waislamu, au hata yeye katika chama chake kuwa na uwakilishi wowote unaobalance kidini, sana sana chama chake kina stracture ambayo wakiristo ni wengi sana kuliko waislamu.


mtabebwa lakini mwisho wa siku mtaanguka tu maana mnategemea kubebwa badala ya kutembea wenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom