Mtandao wa Halotel wanafanya wizi wa kutisha kwenye bundle za wateja kuanzia leo saa 6 mchana tarehe 05.01.2023

MHP

Senior Member
Apr 2, 2012
105
203
Kuanzia leo saa 6 Mchana tarehe 05.01.2023 Mtandao wa Halotel unawaibia wateja wake bila huruma kupitia Vifurushi vya Internet. Ukijiunga kifurushi cha Siku cha Shilingi 1,000 ambacho wanakupa MB 490 na mara Tu ukianza kukitumia ndani ya Dakika 3 Kinakuwa kimeisha.

Kwa MB 490 ukiangalia video ya dakika 1 na nusu YouTube hata kabla ya kufika nusu ya video mb zinakuwa zimeisha.

Ndo hivyo tena tuombe Mungu aingilie kati
 
Mimi natumia halotel muda wote na sijakutana na wizi wa kifurushi changu.
 
Ni kweli siku hizi bundle ni gharama.

Ila hiyo video ya Youtube uliyoicheki ilikuwa kwenye quality ipi? Maana quality kubwa husababisha MB kuisha kwa haraka pia.
 
Mimi natumia halotel muda wote na sijakutana na wizi wa kifurushi changu.
Hili nilishawahi kuliona. Halotel ni wapigaji wazuri wa data. Nimetumia mitandao karibia yote isipokuwa TTCL ila Halotel hata ukiperuzi zinaisha fasta.
Walikuwa wananipa 1gb kwa 2000 ila sasa mpk niliacha kununua na sijawahi kununua tena.
 
Vocha iliyoandikwa Shilingi 500 huku inauzwa shilingi 600, hilo limekaaje wakuu!?

Hiyo vocho ya mia 5 uliyonunua kwa mia 6 ukiweka, unapewa message ya hongera kwa kuingiza shilingi mia 5

Yaani kwa kweli nilichoka sana, nilivyoambiwa kwamba mabadiliko hayo ni effective kuanzia tarehe mosi Januari mwaka huu...

Hilo jambo lina ukweli au huku tunaibiwa!?
 
Ukionaje weka salio kwenye halopesa uwe unajinunulia vocha mbona jambo rahisi sana kuliko kulalamika kisa shl.100
 
Sema nini wakuu, hili neno

"TUMUOMBE MUNGU AINGILIE KATI"
au

"TUMUOMBE MUNGU ATUSAIDIE"

linanichefua sana nafsi yangu.

Yaani linaonesha ni kwa jinsi gani sisi hatuwezi kuchukua hatua dhidi ya tatizo husika. Badala tuchukue hatua tunakimbilia "Tumuombe Mungu atusaidie.

Huo naona ni aina fulani ya UPUMBAVU
 
Hili nilishawahi kuliona. Halotel ni wapigaji wazuri wa data. Nimetumia mitandao karibia yote isipokuwa TTCL ila Halotel hata ukiperuzi zinaisha fasta.
Walikuwa wananipa 1gb kwa 2000 ila sasa mpk niliacha kununua na sijawahi kununua tena.
Sahihi kabisa.
 
Sema nini wakuu, hili neno

"TUMUOMBE MUNGU AINGILIE KATI"
au

"TUMUOMBE MUNGU ATUSAIDIE"

linanichefua sana nafsi yangu.

Yaani linaonesha ni kwa jinsi gani sisi hatuwezi kuchukua hatua dhidi ya tatizo husika. Badala tuchukue hatua tunakimbilia "Tumuombe Mungu atusaidie.

Huo naona ni aina fulani ya UPUMBAVU
Ni hatua gani tuchukue? Unamfahamu waziri husika na majibu yake? ....wengine kuacha kutumia tushaacha lkn sio dawa.
 
Kama una line 2,moja kati ya hizo bando linaliwa balaa,hasa ile line unayotumia mara nyingi...mimi nina Airtel na Halotel, hiyo laini ya Airtel bundle lina liwa sio mchezo,ukiweka tu halichukui muda,..lkn Halotel haendi sana.
 
Kuanzia leo saa 6 Mchana tarehe 05.01.2023 Mtandao wa Halotel unawaibia wateja wake bila huruma kupitia Vifurushi vya Internet. Ukijiunga kifurushi cha Siku cha Shilingi 1,000 ambacho wanakupa MB 490 na mara Tu ukianza kukitumia ndani ya Dakika 3 Kinakuwa kimeisha.

Kwa MB 490 ukiangalia video ya dakika 1 na nusu YouTube hata kabla ya kufika nusu ya video mb zinakuwa zimeisha.

Ndo hivyo tena tuombe Mungu aingilie kati

Mkuu mi nilishangaa hiyo dakika moja nyingi mbona cheki hii
IMG_1213.jpg
 
Sema nini wakuu, hili neno

"TUMUOMBE MUNGU AINGILIE KATI"
au

"TUMUOMBE MUNGU ATUSAIDIE"

linanichefua sana nafsi yangu.

Yaani linaonesha ni kwa jinsi gani sisi hatuwezi kuchukua hatua dhidi ya tatizo husika. Badala tuchukue hatua tunakimbilia "Tumuombe Mungu atusaidie.

Huo naona ni aina fulani ya UPUMBAVU

Eti ni aina fulani ya upumbavu
 
Back
Top Bottom