Malalamiko ya Wananchi kuhusu mabadiliko na gharama za vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo mwaka 2021

Feb 3, 2019
11
45
1611911673875.png

Mtandao wa Tigo umekuwa mtandao wa ajabu sana. Yaani saizi wana-program ya ovyo sana ukinunua salio kupitia Tigo pesa, pesa iliyokuwa kwenye acc ya Tigo pesa unakatwa haijalishi hata kama umenunua kifurushi kwa salio la kawaida. Naamini watu wa Sheria mpo humu mtalizungumza suala hili kwa Lugha ya ki-Sheria.

Ni sawa sababu mnadai pesa yenu, lakini kwenye technique za kibiashara mna feli sana. Sababu

1. Mnafanya service yenu kuwa ya gharama sana kwa wateja wenu kitu kinachofanya Vodacom akutandike kila siku sokoni. Mfano mimi mlikuwa mnanidai 3500/= Nimelipa pia nikaongeza vocha ya 3000/= nyingine ili niweze kujiunga kifurushi maana yake hapo nimetumia 6,500/= mnaona Mteja wenu Mlivyo mpatia gharama kubwa.

2. Customer care wanna-midomo michafu sana halafu ukipeleka lalamiko wana kucheka punde unakatiwa simu.

3. MB’s pia mnachakachua tena sana tu. Kweli mnatuogopesha wateja wenu

Niwaambie tu nilikuwa loyal customer wenu ila enough wazee.

WADAU WENGINE WENYE MALALAMIKO HAYA

Vodacom:
A4414141-9397-480E-9641-DC4BAF4F8D87.jpeg
B82CFD25-70EA-4247-87C7-527F84AB0A32.jpeg


Nilikia najiunga vifurushi vya Tigo muda si mrefu,khe!kuangalia menu naona wamepandisha gharama kwa 100% na kupunguza huduma.

Ndio nikageukia vifurushi vya TTCL(laini ninayo),nikaona kwa robo ya gharama ya TTCL unapata huduma mara 2 zaidi kwa Tigo.

Waungwana na wapenda maendeleo wote naomba tuhamie TTCL haraka iwezekanavyo.....nina uhakika hata hapo ofisi ya Tigo makao makuu wote watakua wanatumia TTCL .

1.vifurushi vya TTCL vya wiki View attachment 1686635

2.Vifurushi vya Tigo vya wiki
View attachment 1686650
Leo nilikuwa najaribu kujiunga kifurushi cha internet mwezi kutoka Tigo, ambapo nilikuwa napata GB 7 kwa sh 10,000/=

Ila kwasasa hiyo Sh 10,000/= napewa GB 2.5

Kwa uchumi huu wa kati tunaelekea wapi?

Ni muda sasa wa kuanza kuhama huu mtandao, maana vifurushi vya data kutoka tigo havishikiki kabisaaa.

Mtandao gani kwa sasa una nafuu kuliko Zantel?
Nimeona niandike hili juu ya wizi wa kampuni ya (TIGO) kwenye vifurushi vyao, haijarishi ni kifurushi cha dakika au ni cha sms au internet,

Wamekuwa wakipandisha vifurushi vyao bila kujali hali halisi ya maisha tuliyonayo

Jana nimejaribu kununua kifurushi cha internet
ambacho nimezoea kununua cha Tsh 3000 gb 2 kwa wk

Nimekuta kimepunguzwa gb1 na kubakia gb 1 kwa tsh 3000 nimeshindwa kununua kifurushi hicho bado najiuliza nihamie kampuni gani yenye unafuu wa vifurushi tofauti na hawa wezi @tigo_tz

View attachment 1688193
Nina laini za mitandao yote inayopatikana kwenye mazingira yangu lakini cha ajabu nazunguka tu humohumo hakuna mwenye nafuu

TTCL walikuja moto ila ikawa kifurushi hakifanyi kazi mpaka kinaexpire (yaani ukituma sms haiendi au unafungua data internet haifunction labda kwa mara chache tu)

Zantel nao wako vizuri lakini dakika unaweza kushangaa tu paap! zimeisha. saa zingine una kifurushi ila wanakata vocha yako bila sababu na ukipiga customer care unakutana na majibu yaleyale ya kukaririshwa darasani

Airtel kwa kachenji kadogo ti utapata bonge la kifurushi (hasa internet) ila ndo utajua mwenyewe utaenda kuipata wapi access ya mtandao

Tigo ndo hata sijui nianzie wapi maana kila uozo ni wao. Kifurushi cha kawaida kabisa lakini kinagawanywa dk nyingine kwa ajili ya usiku tu (yaani unalazimishwa kupiga simu usiku) wakati hii tumezoea inawekwa kwenye vifurushi vile vingine vya ziada kama ofa nk

Halotel nao ndo walewale

Voda kama kawaida yao wao ni wazee wa ghali

Basi nimejikuta nahama mtandao fulani kwa muda tu mara huko kwingine wakileta ujinga nakuja kuurudia tena.

Lakini kuna mtandao mmoja katika hiyo nimeapa sitakaa nije kurudi tena!
pia soma > Malalamiko mbalimbali kuhusu mabadiliko ya vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo kwa mwaka 2020
 

wegman

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
1,066
2,000
Hamieni Airtel.

Mwanzo nilipata shida sana kuhamia mtandao mpya ila kwa sasa sijutii kwa maamuzi yangu ni mwendo wa kuperuzi. Line ya tigo imebaki kuwa ya kupokea simu na mihamala tu.

Yani kwa maoni yangu binafsi sikuhizi naona Voda ananafuu kuliko tigo. Tigo wamekua majambazi haswa.
 

cool d

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
771
1,000
Alafu Sasa hivi wamekuja na njia mpya ya kukwapua pesa eti Pata Pata sh 300 yaani mtu anakaa anawaza jinsi ya kumuibia mteja wake bila huruma badala ya kuwaza kumfurahisha kwa kukubali kumuungisha, mara Patapata na mara jibu maswali Kuna pesa wakati ni uongo hebu waache hayo mambo ya kuibia wateja wao.
 

Bengalisis

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
1,694
2,000
Hakuna mtandao wa kiduanzi kama tigo nafikiri management ya tigo vichwani mwao wamejaza upuuzi mtupu, eti mteja anajiunga kifurushi wanagawanya dakika zingine utumie usiku wa manane tu zingine mchana hawa jamaa ni wa hovyo sana, mm mwezi wa 4 huu sijaweka salio kwa laini ya tigo kwa sababu ya mambo ya kijinga kama hayo
 

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
9,229
2,000
Tigo washenzi sana!

Walikuwa wanakuja vizuri ila sasa wamekuwa wabaya wa mwisho. Siku hizi wametegesha ukipiga simu ikifika pale pa kuongea na mhudumu inakata automatic.

Vifurushi hovyo na network hovyo 😏😏😏
Bora airtel japo wana mapungufu kiasi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom