Msimu wa Mateso kwa Watumishi: Halmashauri zimeanza kuwatishia Walimu na watumishi wengine kutoa mchango wa Mwenge, 2023

13F75D13-5647-47E2-906B-1F47F33DC440.jpeg
 
Mbio za mwenge zimeanza tenaaa, nakumbuka mwaka fulani nikiwa mikoa ya kusini, tulipanga lodge moja hivi kwa siku 10, zimebaki siku 3 tukaambiwa tunatakiwa tukatafte malazi sehemu nyingine ili kupisha wageni wa mbio za mwengeee, wakishapita ndo turudi kuendelea kukaa
 
Mbio za mwenge zimeanza tenaaa, nakumbuka mwaka fulani nikiwa mikoa ya kusini, tulipanga lodge moja hivi kwa siku 10, zimebaki siku 3 tukaambiwa tunatakiwa tukatafte malazi sehemu nyingine ili kupisha wageni wa mbio za mwengeee, wakishapita ndo turudi kuendelea kukaa
 
Walimu wa hii nchi ni wajinga saana
Tafadhari sana Kiongozi kwa heshima ya kutosha nikupayo naomba uwaombe radhi walimu wate wa Tanzania kwa kauli yako hapo juu. binafsi naona umepitiliza sana katika uhuru wako wa kutoa maoni kikatiba lakini pia unajinasibu vipi wewe ni msomi na mwerevu katika mambo mengi kama unamdharau Mwalimu wako aliekufundisha mpaka kufika hapa?

Unaandika kwa kufuata taratibu za uandishi na kupangilia Herufi vizuri bila kukosea na unamtukana aliekufundisha kuwa MJINGA SANA hii ni sawa kweli? Nilikuwa na nguvu za kusoma komenti za wadau lakini nilivyofika kwenye mchango wako nikakwama na kujisikia vibaya.

Ukiwa askari unaweza kutambua hili kwamba Senior kwako hubaki senior tu hata akistaafu na cheo kidogo kupita wewe.

Kwangu naona umeikosea Taaluma ya ualimu nchini na umewakosea walimu wetu na umewakosea watu wote waliopewa na kurithishwa taaluma na walimu hao.
 
Yaani mishahara yenu midogo, mapunjo na maslahi mengine kulipwa ni mbinde, matibabu mnayopaswa kugharamiwa ni kama fadhila lakini bado mnachangishwa kwa nguvu kutoka katika mishahara yenu kugharimia mbio za Mwenge kama kwamba nyie ndio mlioziomba zifanyike.

Ualimu ni kaliba ya juu yenye hadhi na heshima yake lakini kwa Tanzania na pengine Africa wanasiasa wameinyonga kifo cha mateso sana
 
Baada ya serikali kubadili kutoka wenye ufaulu mkubwa ndio kupelekwa ualimu na kuwapa nafasi wa ufaulu mdogo ndio hadhi ya Mwalimu ilianza kuyumba.
Ni kama ilionekana kazi ya hisani kwa walioipewa hivyo kutawaliwa na woga
 
Back
Top Bottom