Halmashauri ziache kuwalazimisha Watumishi kuchangia Mwenge

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Hii tabia ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuwataka watumishi wa umma ndani ya Halmashauri imetoka wapi?

Yaani mkuu wa wilaya anaagiza wakuu wa idara kusimamia zoezi na kuomba majina ya wachangiaji, sasa hatujui wasiochangia wafanywaje.

Pia wakuu wa idara wamekuwa wakionywa endapo atashindwa kulazimisha watumishi wa idara yake watapokonywa madaraka.

Wanatumishi wa umma huwa wanajiuliza wizara ya TAMISEMI haina bajeti kwa ajili ya mwenge?

Mh Rais piga marufuku hiki kitu,kinakera na kuudhi watumishi wa umma,kama utaratibu huu upo wa kuchangia mwenge watumishi wawe wanakatwa asilimia fulani huko hazina kwa ajili ya mwenge lakini si hii tabia ya kushupalia kuchangia
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
3,705
2,000
Serikali ya JMT, iwe inapanga bajeti ya kukimbiza mwenge wa Uhuru. Mfano, bajeti ya 2021/2022 ni Tsh 34 trillion hatuoni huko bajeti ya kukimbiza mwenge wa Uhuru.
 
Malaika Mkuu

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
868
1,000
Halmashauri za majiji, manispaa, miji, wilaya, na vijiji zinachangisha watumishi na wanachi baada ya kukubaliana kwenye vikao na mikutano yao.

Mwenge ni tunu na alama inayotambulisha nchi yetu. Makubaliano yakifikiwa ni ya wengi wape kame ilivyo ada kwenye vikao.

TUNAUPENDA MWENGE

UNAWAMRIKA WAZEMBE , WALA RUSHWA NA KUFICHUA MAOVU KWENYE MIRADI.
MWENGE HOYEEEEE

Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
 
Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Halmashauri za majiji, manispaa, miji, wilaya, na vijiji zinachangisha watumishi na wanachi baada ya kukubaliana kwenye vikao na mikutano yao.
Mwenge ni tunu na alama inayotambulisha nchi yetu...
Huo Mwenge si una bajeti yake
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
29,587
2,000
Halmashauri za majiji, manispaa, miji, wilaya, na vijiji zinachangisha watumishi na wanachi baada ya kukubaliana kwenye vikao na mikutano yao.
Mwenge ni tunu na alama inayotambulisha nchi yetu.
Makubaliano yakifikiwa ni ya wengi wape kame ilivyo ada kwenye vikao.
TUNAUPENDA MWENGE
UNAWAMRIKA WAZEMBE , WALA RUSHWA NA KUFICHUA MAOVU KWENYE MIRADI.
MWENGE HOYEEEEE

Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
Mwenge hauna maana yoyote,ile ni ibada ya sanamu tu
 
Empty maisha

Member
Oct 10, 2020
31
125
Hii tabia ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuwataka watumishi wa umma ndani ya Halmashauri imetoka wapi?

Yaani mkuu wa wilaya anaagiza wakuu wa idara kusimamia zoezi na kuomba majina ya wachangiaji ,sasa hatujui wasiochangia wafanywaje....
Ukikataa utasikia mwenge utaondoka na mtu hapa ho hooo!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom