Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Sasa Kila mtu nchii hii akiwa mfanyabiashara nani atakuwa mnunuzi wa mwenzanke?
Katika maisha nilichojifunza usitegemee chanzo kimoja cha kipato ,hata kama una biashara ya Duka basi jitahidi uwe na Genge ,kama una biashara ya kuku basi jitahidi uwe na biashara ya matunda /mboga mboga
 
Sasa Kila mtu nchii hii akiwa mfanyabiashara nani atakuwa mnunuzi wa mwenzanke?
Market share ni kubwa sana ,hauwezi kulimaliza soko lote.

Kwani MO au Bakhresa anatengeneza ndege? Si anatumia kusafiri? So hata uwe mfanyabiashara mkubwa kuna bidhaa lazima utanunua kutoka kwa wafanyabishara wenzako, Hivyo hivyo kwangu nachoma mkaa lakini silimi mahindi au mchele hivyo nanunua kutoka kwa wafanyabiasha ,same kwa hao wakulima wananua mkaa /gesi etc

Hata mwenye genge atatumia bajaji/pikipiki/guta kubeba mizigo yake.

Mimi nazungumzia usitegemee chanzo kimoja cha kipato ,kama umeajiriwa basi pembeni uwe hata na kitu kingine cha kukuingizia pesa ,huenda isiwe biashara(exchange ya bidhaa kwa fedha) lakini hata kuuza ujuzi wako kupata pesa eg Mwalimu kuuza vitabu ,kufundisha tution etc

Mfano tu Soko la Kuku na Mayai ni kubwa sana ,kuna kipindi kinafika kuku na mayai kupata tabu au ukipata bei inakuwa juu ,soko la samaki wa baharini ni kubwa sana uhitaji mkubwa availability ndogo.
 
Back
Top Bottom