Msanii Wema Sepetu kujiunga na CHADEMA rasmi

Msanii Wema Sepetu kujiunga na CHADEMA rasmi

Bado kuna kundi kubwa linatarajiwa kutajwa na Kingwangwala huenda nao wakatimkia Uchademani! Kazi kweikwei!
Kigwangalah amewajuaje? maana mwenzie ilibidi "ashughulike" na msambwende wa masogange ili awajue anaowatafuta.
 
CHADEMA kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari na kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo msanii Wema Sepetu.
View attachment 473709
Mbowe na Lissu leo wanawasilisha ile hati ya mashitaka iliyorekebishwa na kumuongeza Mwanasheria Mkuu. Wema Sepetu yupo Katikati ya Esther Bulaya na Mbowe hii leo. Kutoka Mahakama Kuu: Kesi ya Mbowe dhidi ya RC Makonda, RPC Sirro na ZCO Wambura
View attachment 473719 View attachment 473718
Baada ya hapa Mbowe ataongea na Waandishi.

Ikumbukwe kwamba Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, jana alijitokeza mahakamani kuwa wakili wa Wema na wenzake wawili akiwamo mfanyakazi wa ndani. Msanii maarufu wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu anakabiliwa na kesi ya kukutwa na bangi. Kesi hiyo ya Wema iliahirishwa hadi Machi 15.
Hivi huyu wema ni nani hasa kwenye jamii yetu hata anapewa umuhimu huu na media?
Maoni yangu ni kwamba watanzania wote wana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa ambacho kimesajiliwa.
 
Mhuu! Hii reasoning hatari sana! It's as if wewe ndiye hakimu wa Watanzania - nani anafaa kujiunga na chama cha siasa na nani hafai. Nikuulize: alipokuwa CCM alistahili au hakustahili? Ameamua kujiunga Chadema, anastahili au hastahili? Then, vigezo vyako vya kijiunga na chama cha siasa ni vipi?
Kujiunga sio tatizo, tatizo ni huo urafiki wao na m/kiti uliotokana na wote kutuhumiwa. Inasemekana sepetu alikuwa na misokoto ya .... Nyumbani kwake na ni sehemu ya ushahidi ktk kesi.
Mbowe yeye katuhumiwa na hakuna ushahidi.
Kwanini aungane na mtu kama huyo?
Inatia shaka na kuharibu taswira ya chama
 
CHADEMA kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari na kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo msanii Wema Sepetu.
View attachment 473709
Mbowe na Lissu leo wanawasilisha ile hati ya mashitaka iliyorekebishwa na kumuongeza Mwanasheria Mkuu. Wema Sepetu yupo Katikati ya Esther Bulaya na Mbowe hii leo. Kutoka Mahakama Kuu: Kesi ya Mbowe dhidi ya RC Makonda, RPC Sirro na ZCO Wambura
View attachment 473719 View attachment 473718
Baada ya hapa Mbowe ataongea na Waandishi.

Ikumbukwe kwamba Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, jana alijitokeza mahakamani kuwa wakili wa Wema na wenzake wawili akiwamo mfanyakazi wa ndani. Msanii maarufu wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu anakabiliwa na kesi ya kukutwa na bangi. Kesi hiyo ya Wema iliahirishwa hadi Machi 15.
wastage of time and resources. No political gain
 
Kama nikweli mbona mnaonekana mmevurugwa sana...mnajibu kila post.... inaonekana Mioyo imejaa uchungu sijui alikuwa anawapa nini huko


Hata wakati wa Lowasa mlibweka Ccm kufa, nahisi majawabu mnayo.

Hivi wema nae asset?
 
Wema naye ni Political figures hapa Tanganyika ?![emoji45] [emoji45] [emoji45]
 
Kiukweli inabidi uwe na akili ya maiti kuishabikia chadema ya sasa.....
Yaani ni kama upinzani umerudi miaka ishirini nyuma.

CCM imepoteana lakini Chadema haijielewi.

Yaani sasa hivi hawana kabisa hoja za kitaifa zaidi ya kutafuta kiki kama wasanii wa bongo movie.!
Poleni sana, ukimaliza kulia ukajitambua karibu nyumbani uwe kamanda
 
Wakati wa Uchaguzi hakika utaona vi-wonders vya wasanii wetu.ni lazima atarudi CCM tena na mijitusi juu
 
Sipati picha na mashoga nao wakiweka alama ya vidole viwili mahakamani.
 
Huyo wema hana effect yoyote kwa ccm hata akiondoka, waliondoka wakina kingunge, sumaye, lowasa na bado ccm iko imara
 
Ndio Maana Nilisema Hapa Mkuu kwamba Huu Usajili wa Dirisha Dogo Ni Very Strategic yaani Followers Wa WEMA tukipata japo 100,000 wakaparticipate Kwenye campaign na Kuvote haKika by 2020 LUMUMBA hakutakalika.
 
hatutaki makapi wala mamluki sisi woii watu twenye akili zetu tutahama hiki chama maana kinawekewa nuksi sasa.kitanuka
 
Ingawa si rasmi,msanii na mlimbwende Wema Sepetu anatajwa kujiunga na wapinzani wetu CHADEMA. Wema amekuwa kada wa kupigiwa mfano wa CCM na ameshiriki kindakindaki katika kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.

Kwa yaliyomkuta na yanayoendelea kumkuta,kwa kuzingatia ahadi kemkem na tamutamu zisizotekelezwa wakati wa kampeni,Wema Sepetu ameichagua CHADEMA ili awe na amani,utulivu na ulinzi. Nani hatakuwa na amani,utulivu na ulinzi akizungukwa na wanaCHADEMA?

Ni chaguo sahihi kwa wakati alionao. CCM yatupasa kujiuliza na kujipanga juu ya hili badala ya kubeza. Wema aweza kutuathiri kichama na kisiasa.

Mwafaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom