Msanii Wema Sepetu kujiunga na CHADEMA rasmi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
CHADEMA kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari na kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo msanii Wema Sepetu.

a88bba6e-ed7e-422b-a17d-e0de0abb7490.jpg

Mbowe na Lissu leo wanawasilisha ile hati ya mashitaka iliyorekebishwa na kumuongeza Mwanasheria Mkuu. Wema Sepetu yupo Katikati ya Esther Bulaya na Mbowe hii leo. Kutoka Mahakama Kuu: Kesi ya Mbowe dhidi ya RC Makonda, RPC Sirro na ZCO Wambura
fe6e1a3b-3fbd-4a15-ba8e-548f75c1b13b.jpg
f182fb41-04e9-45df-a6be-0e48c1482adf.jpg

Baada ya hapa Mbowe ataongea na Waandishi.

Ikumbukwe kwamba Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, jana alijitokeza mahakamani kuwa wakili wa Wema na wenzake wawili akiwamo mfanyakazi wa ndani. Msanii maarufu wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu anakabiliwa na kesi ya kukutwa na bangi. Kesi hiyo ya Wema iliahirishwa hadi Machi 15.
 
Kipindini cha Kampeni walikuwa na kiherehere kusimama majukwaani kutoa support kwa "kijani" leo ndo wanagundua that was crap.. warudi nyumbani kwao, tena siyo huyo tu, wooote! Ingawa ningewa-caution sana CHADEMA kuitoifanya hii ishu kama ni ya kisiasa. Kama wanataka kumpa support (Lisu being her Lawyer) iwe as professionalism na si kwasababu tu ku-attack upande wa pili, pia kama kweli Wema amehamia CHADEMA, uongozi should just take it kawaida, NOT a big deal. Si lazima kumtangaza..
 
Chama kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari na kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo msanii Wema Sepetu.
Good Riddance...ccm haihitaji wanaotaka kulindwa na chama kuendesha udhalimu wao.
 
tmp_8088-IMG-20170223-WA0028-1286468311.jpg

tmp_8088-IMG-20170223-WA0031-1122800591.jpg

Wafuasi wa chadema pamoja na Viongozi mbalimbali wakiwa mahakamani kwenye kesi ya Mbowe dhidi ya Makonda
 
Back
Top Bottom