BASATA: Nay wa Mitego ni mtoto wetu, hatujamfungia

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Dkt. Kedmon Mapana, ameeleza kwamba BASATA haikumfungia mwanamuziki Emmanuel Elibariki, maarufu kama ‘Nay wa Mitego,’ kufanya maonyesho, lakini walimuita kuzungumza naye ili kurekebisha baadhi ya mambo.

Akizungumza na waandishi wa habari, alisema kwamba BASATA imempa Nay wa Mitego siku saba ili kufanya mkutano naye na kumsikiliza kuhusu wimbo wake wa ‘Amkeni.’ Pia, alisisitiza kwamba msanii huyo anaweza kuendelea na shughuli zake za muziki kama kawaida.

“Leo namwambia kwamba sisi hatujakufungia, tunakusikiliza, wewe ni mtoto wetu, tupo hapa kukulea. Kwa hiyo, tumempa siku saba tumsikilize,” alisema Katibu Mtendaji.

Mnamo tarehe 9 Septemba mwaka huu, Nay wa Mitego alialikwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusiana na tuhuma za uchochezi kupitia wimbo wake wa ‘Amkeni.’ Alikuwa kizuizini kwa takribani saa tatu. Hata hivyo, BASATA ilisema hawahusiki na kuitwa kwake polisi, ingawa walimuita mara kadhaa afike katika ofisi zao bila kuitikia wito huo.
 
Nay anapaswa kutumia diplomasia ya kichwa chake vizuri kwani baadhi ya mambo huhitaji busara na hekima kimaamuzi zaidi.
Hakuna ubaya kwa yeye kwenda na kukaa na BASATA na wakayamaliza.

Asfuate mkumbo wa Chadema maana tofauti na yeye anayeutegemea usanii wake kujiingizia kipato.
Wao Chadema wanategemea na kuingiza Pesa kupitia mabilioni ya Ruzuku toka serikalini kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa nchini.

Hivyo hawako level moja na Nay wa Mitego.

Muhimu Nay azingatie future yake badala ya kuendekeza Sifa bila kipato.
 
Acha uoga dogo
 
Kwani alishawahi kusema yeye ni CHADEMA??huo mkumbo wa CHADEMA ni upi??mtu anaandika vitu halisi halafu CHOKO wewe unasema ni CHADEMA??kama kuimba na kusifia aliimba Capt.Komba lakini leo watoto wake wanahangaika mitaani!!!peleka UCHOKO wako huko KENGE wewe
 
Back
Top Bottom