comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 8,222
- 5,946
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo kikiwa kwenye maandalizi ya Baraza Kuu, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amekitaka kitoe maelezo ya kina kwa nini kiliwafukuza uanachama wanachama wake 19 ambao ni wabunge wa viti maalumu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 14, 2021, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Benson Kigaila amesema chama hicho kimepokea barua kutoka kwa Msajili huyo Julai 6 na wakaijibu Julai 9 mwaka huu.
Katika maelezo yake, Kigaila amesema barua ya Jaji Mutungi imewataka kutoa maelezo hayo kwake baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa waliokuwa wanachama wao 19.
"Tumemjibu kuwa hatuwezi kutoa maelezo hayo kwa sababu barua aliyotuandika hajaambatanisha malalamiko ya hawa waliomlalamikia.Tunakiona hapa ni kutaka kuvuruga mchakato wa Baraza la Kuu la Chama linalotakiwa kuketi mwaka huu.
"Huwezi kufungua kesi ya aina moja kwenye mahakama mbili tofauti, hawa watu 19 baada ya kufukuzwa uanachama mwaka jana kisha wakakata rufaa Baraza Kuu, ambalo bado halijakaa.Sasa bado rufaa yao haijasikilizwa wamekimbilia kwa msajili," amesema Kigaila
Kigaila amesema hawawezi kutoa maelezo kwa Jaji Mutungi kwakuwa ni kinyume cha utaratibu wa chama hicho.
"Sasa msajili akisema hakubaliani na maelezo yetu na kwamba hawa watu 19 ni wanachama halali, si amevuruga mchakato wa Baraza Kuu?
Wabunge hao 19, wakiongozwa na Halima Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake la Chadema ( Bawacha), walifukuzwa uanachama mwaka jana na kamati kuu ya Chadema baada ya kwenda kinyume na msimamo wa chama hicho kwa hatua yao ya kuapa kuwa wabunge wa viti maalumu bila ridhaa ya chama.
Chanzo: Mwananchi