Kwa mambo haya tunayofanyiana watz Mungu akisaidia nikatoka nitakua narudi Tz kutembea tu. Nchi nzuri ila wapuuzi wanaiharibu mtu unakosa hata hamu ya kuishi humu
Na fikra za kupuuzia kama hizi ndio zina sababisha msipewe
 
Ili kupata passport,unatakiwa uwe na.
1.cheti cha kuzaliwa.
2.cheti cha kuzaliwa cha mzazi mojawapo.
3.Kitambulisho cha Taifa.
4.kitambulisho cha Kazi Kwa watumishi wa umma.au barua ya utambulisho KUTOKA serekali za mitaa Kama hujaajiriwa.
5.barua ya maombi ya passport kama uko mkoani anapitisha kwa kamishna WA mkoa kwenda Kwa kamishna mkuu,anwani zao za posta unaweza kuzipata ofisini kwao.
6.uthibitisho wa safari ukionyesha nchi unauokwenda.
7.baada ya kuwa na vielelezo vyote utaanza kujaza form ya maombi online kupitia uhamiaji portal.kuna sehemu uta upload barua ya utambulisho na Cheti cha kuzaliwa.
Kama ombi limekamilika utapewa contral namba ya kulipia 20,000 ili uweze Ku print form.
Ukishaprint form utatafuta mashaidi waijaze na pia mwanasheria.
8.baada ya hapo utaenda ofisi za uhamiaji ukiwa na hiyo form na vielelezo nilivyotaja hapo juu,
9.Ombi litapitiwa kama hakuna dosari,litapitishwa,utalipia 130,000 Kwa kutumia control namba,alafu utakamilisha ombi Kwa kupiga picha pamoja na kuchukuliwa alama za vidole.
10.Baada ya hapo utasubiri Kwa mwezi mmoja passport kuwa tayari.
11.kama unaihitaji Kwa haraka na hauna baadhi ya vielelezo unaweza watumia vishoka,Ila utawalipa gharama za ziada.almost 100-200k.
Kama wazazi wote wametangulia mbele ya haki ila viambatanisho vingine ninavyo inakuaje hapo mkuu,nitapata kweli passport?
 
Wakurungwa mpaka sasa sijapewa Mwongozo
Kuhusu barua andika simple tu ya kiswahili isiwe ndefu, uthibitisho wa safari andika ni safari binafsi unless iwe ya kiofisi unaweza kuattach barua ya kazini au kama umepata chuo nje utaweka admission letter, hao wanaokwambia uongeze nguvu usikute hata passport yenyewe hawana, jiamini inginia online jaza fomu yao na ukienda ofisini kwa interview view relax akikuuliza swali la kijinga na wewe mrudishie uone atajibuje, Mimi nilipata passport bila kutoa rushwa hata senti na wazazi hawakua na vyeti vya kuzaliwa, walipovidai nikawambia kwani nyie wqzazi wenu wanavyeti vya kuzaliwa? Labda wamechukua hivi vya rita wakachukua finger prints nikasema wiki iliyofuata nikaendea

Sent from my Infinix X606D using JamiiForums mobile app
 
Umeshauriwa vizuri.

1. Hawa wote waliokwambia ni hata siku mbili ,Yes ila ni uwe na hongo. Ukifuata utaratibu utapata lakini si chini ya mwezi.
Nilijua kwa dar wiki mbili ndio Maximum kumbe hadi mwezi?
2.Barua ya mwaliko mwambie mwenyeji wako akuandikie, kama ni email unaprint unapeleka.
Hii sina.. Je uaambatanisha na vyeti vyako ndio unapewa Passport
3.Kokote huduma unapata si lazima kwenda Dar, ila tu kuwa mvumilivu usiwe na haraka wala kimuhemuhe.
Na nina kimuhemuhe kweli asee ila kwa huku naona usumbufu ni mkubwa kuliko dar. Dar napo ghalama ni nyingi mno kwenye mausafiri na nauli za basi

Mkuu nakuomba pm please please
 
Ndiyo unawasilisha kila kitu, unapokwenda kukusanya vinakaguliwa ukiwa palepale visipotimia unarudishiwa rundo lako mpaka vitimie ndiyo unaondoka dirishani.
Daah na kwenye kujaza form online hiyo barua itahitajika pia??
 
Barua andika kwa kamishna jenerali mkuu ya kiswahili ukiomba hati ya kusafiria.

Uwe na sababu ya safari ambayo utaambatanisha.

Jaza form online lipia halafu iprint peleka ofisi ya uhamiaji pamoja na viambatanisho vinavyotakiwa.

Hati unaweza kupata bila kutoa sh. 10 ya ziada ndani ya week mbili.
Cc
harakati za siri
Ushauri wako please
 
Back
Top Bottom