sisi wenye asili ya kiasia wazaliwa wa tanzania kupata passport hata kama una cheti cha kuzaliwa chako cha baba babu hadi cheti cha nabii adamu uwapelekee na cha mama bibi mpaka cheti cha eva au hawa hupati
 
Hii nchi ya hovyo yaani kupewa passport mpk uwape uthibitisho wa Safari wakati ilibidi kila mwenye uhitaji awe nayo bila kujali anasafiri au hasafiri

Last month Kuna mzee mmoja aged 59 alipata mchongo wa scholarship South Korea kwakua age imeenda akaona ambless mtu yyte yule akampa mchongo mwalimu mmoja (lakini mda ulibakia mchache sana) mwalimu akaanza kufatilia hyo passport aiseee alisumbuliwa mpaka akaghairi kwenda...... Lakini angekuwa na passport mkononi within a week àngeenda kusoma Korea.
 
Barua andika kwa kamishna jenerali mkuu ya kiswahili ukiomba hati ya kusafiria.

Uwe na sababu ya safari ambayo utaambatanisha.

Jaza form online lipia halafu iprint peleka ofisi ya uhamiaji pamoja na viambatanisho vinavyotakiwa.

Hati unaweza kupata bila kutoa sh. 10 ya ziada ndani ya week mbili.
Ningependa kufahamu je hio Barua unaandika kwa watu walio mkoani tu. Au Hata ukiwa dar utaratibu ni huo huo??
 
Ok mkuu Ahsante kwa muongozo. Sasa ningependa nijibiwe hayo maswali hapo.
Je ni lazima niandike Barua na kupeleka barua ya utambulisho wa Serikali za mtaa??
Yes barua ya uambatanisho kutoka serikali za mitaa ni muhimu, pia nenda kawape 10000 wakujazie wenyewe palepale ukijaza mwenyewe itagoma na hapo utakuwa ushalipa 20000 yako ni hasara bin hasara
 
Yes barua ya uambatanisho kutoka serikali za mitaa ni muhimu,
Nishaipata. Mungu mkubwa
pia nenda kawape 10000 wakujazie wenyewe
Palepale ofisi za uhamiaji ndio wanijazie??? Stationary hapa chuga wanadeal na hii kitu je wakinijazia wao maafisa pale hawataleta figisu kweluhaitagoma
palepale ukijaza mwenyewe itagoma na hapo utakuwa ushalipa 20000 yako ni hasara bin hasara
Daah.. Tanzania yangu
 
Nishaipata. Mungu mkubwa

Palepale ofisi za uhamiaji ndio wanijazie??? Stationary hapa chuga wanadeal na hii kitu je wakinijazia wao maafisa pale hawataleta figisu kweluhaitagoma

Daah.. Tanzania yangu
Shida Wana vishoka wao Wana access na system ukijaza mwenyewe hats ulipie form inagoma ku print na lengo lao wakutapeli hyo elfu kumi yako tu
 
Ili kupata passport,unatakiwa uwe na.
1.cheti cha kuzaliwa.
2.cheti cha kuzaliwa cha mzazi mojawapo.
3.Kitambulisho cha Taifa.
4.kitambulisho cha Kazi Kwa watumishi wa umma.au barua ya utambulisho KUTOKA serekali za mitaa Kama hujaajiriwa.
5.barua ya maombi ya passport kama uko mkoani anapitisha kwa kamishna WA mkoa kwenda Kwa kamishna mkuu,anwani zao za posta unaweza kuzipata ofisini kwao.
6.uthibitisho wa safari ukionyesha nchi unauokwenda.
7.baada ya kuwa na vielelezo vyote utaanza kujaza form ya maombi online kupitia uhamiaji portal.kuna sehemu uta upload barua ya utambulisho na Cheti cha kuzaliwa.
Kama ombi limekamilika utapewa contral namba ya kulipia 20,000 ili uweze Ku print form.
Ukishaprint form utatafuta mashaidi waijaze na pia mwanasheria.
8.baada ya hapo utaenda ofisi za uhamiaji ukiwa na hiyo form na vielelezo nilivyotaja hapo juu,
9.Ombi litapitiwa kama hakuna dosari,litapitishwa,utalipia 130,000 Kwa kutumia control namba,alafu utakamilisha ombi Kwa kupiga picha pamoja na kuchukuliwa alama za vidole.
10.Baada ya hapo utasubiri Kwa mwezi mmoja passport kuwa tayari.
11.kama unaihitaji Kwa haraka na hauna baadhi ya vielelezo unaweza watumia vishoka,Ila utawalipa gharama za ziada.almost 100-200k.
Mkuu Ahsante sana malekezo yako yapo sahihi kwa 95%. Nimeshafanya hatua kafhaa kesho naenda uhamiaji. Niombee nifanikishe Tafadhali
 
Pole, lakini kama hauhitaji kwa haraka sana week sita si nyingi.
Ahsante. Ika ngoja nivumilie asee nikitaa dec isinikute huku kama Mungu akifanya wepesi. Subira ibada ngoja nijitahidi kuvumilia
 
Back
Top Bottom