Msaada: Nahitaji kujifunza udereva na kupata cheti pamoja na leseni kwa ujumla

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,962
6,891
Habari wakuu,

Kama heading inavyoeleza hapo juu, Naomba kwa mwenye experience na masuala haya ya mafuzo ya udereva yanavyokwenda anishauri ni Driving school gani niende ili kupata elimu ya mafunzo ya kuendesha Magari japo haya mdogo kwanza lakini muhimu nijipatie cheti...

Ningeomba kujua pia cost zake, pamoja na duration ya muda wa kumaliza mafunzo na vipi itawezekana mimi kuwa nahudhuria kwa muda nitakaopata nafasi binafsi n.k.

Mimi ni mkazi wa Dar es Samia.
 
Mkuu mbona unapenda na kuendekeza anasa? Kuna haja gani ya wewe kumiliki nakujifunza kuendesha Gari wakati una miguu? Mbona mababu zetu waliishi bila magari na mambo yalienda na walikuwa na furaha tu?
Kuna haja gani ya kuvaa nguo wakati una ngozi na vinyweleo!!?
 
Mkuu mbona unapenda na kuendekeza anasa? Kuna haja gani ya wewe kumiliki nakujifunza kuendesha Gari wakati una miguu? Mbona mababu zetu waliishi bila magari na mambo yalienda na walikuwa na furaha tu?
Sasa unataka kila mtu aishi kama babu yako, kenge wengine mna matatizo sana
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Sasa unataka kila mtu aishi kama babu yako, kenge wengine mna matatizo sana
Ndio tumezidi kupenda na kuendekeza anasa sana. Umeme ukikatika kidogo tu makelele mbona mababu zetu hawakutumia umeme kabisa na walikuwa na furaha tu hawalalamiki na maisha yalienda?
 
Mlimani (Mwenge au Tegeta, hapo ada yake kwa mwezi ni 270K kwa manual, na 300K kwa auto sijui kama sasa hivi wamebadili)
Nenda hapo inatazamana na kanisa la Kakobe ukiwa unatokea Milimani City na nyingine IPO Tabata Ila sababu wewe upo maeneo ya Magomeni basi hii ya Milimani City itakufaa zaidi
 
Rudi Namtumbo kaishi kama babu yako. Ondoka uache kubweka ka mbwa Ughaibuni Cph
Tulia wewe. Nyinyi ndo mmesababisha hadi Serikali ya Canada iingilie kati kupiga marufuku wageni kununua nyumba. Rudisha iyo passport ya Canada urudi nyumbani ulime matikiti. Halafu unaishi Ottawa hujui kifaransa nenda uishi BC huko.
 
Habari wakuu,

Kama heading inavyoeleza hapo juu, Naomba kwa mwenye experience na masuala haya ya mafuzo ya udereva yanavyokwenda anishauri ni Driving school gani niende ili kupata elimu ya mafunzo ya kuendesha Magari japo haya mdogo kwanza lakini muhimu nijipatie cheti...

Ningeomba kujua pia cost zake, pamoja na duration ya muda wa kumaliza mafunzo na vp itawezekana mimi kuwa nahudhuria kwa muda nitakaopata nafasi binafsi n.k.

Mimi ni mkazi wa Dar es Samia.
Nanda VETA hapo chang'ombe ndio utapata mahitaji yako, NIT ni kwa ajili ya wale ambao tayari ni madereva wanaenda kuongeza umahiri na utaalamu zaidi.
 
Ndio hiyo niliyoiongelea mimi na siyo mimi mwenye huo uhitaji, nafahamu hiyo ya hapo na Tegeta na nyingine iko Bagamoyo, kwa kuwa wewe unaishi Magomeni ndio unadhani kila mtu humu ni jirani yako
Huyo mleta mada ni mwenyeji wa Magomeni Mapipa sio Mimi mkuu, nilikua nampa uelekeo wa sehemu ya karibu na eneo alilopo au ulitaka aje kwako Tegeta?
 
Ndio tumezidi kupenda na kuendekeza anasa sana. Umeme ukikatika kidogo tu makelele mbona mababu zetu hawakutumia umeme kabisa na walikuwa na furaha tu hawalalamiki na maisha yalienda?
We nawe kumbe hamu nazo, Nikawa nakuheshimugiii
 
Huyo mleta mada ni mwenyeji wa Magomeni Mapipa sio Mimi mkuu, nilikua nampa uelekeo wa sehemu ya karibu na eneo alilopo au ulitaka aje kwako Tegeta?
Hapana, Mimi naishi Tabata bros
 
Back
Top Bottom