Nawezaje kupata mkopo wa Tsh. Milion 1 na laki 2 kwa dhamana ya vyeti vyangu?

A43

JF-Expert Member
Nov 18, 2023
385
757
Ndg nawezaje kupata mkopo wa tsh Milion 1 na laki 2 tu, kwa dhamana ya vyeti vyangu?


1.Cha form 4

2.Cheti cha kuzaliwa

3.Leseni ya udereva iliyo ndani ya muda

4.Cheti cha diploma chuo cha biashara CBE

5.Cheti cha degree chuo cha uhasibu TIA


Vyote ni Original kabisa, na ni vyakwangu mwenyewe, sina nia mbaya na siwezi kutelekeza nyaraka zangu kwani bado nazihitaji, ni jinsi yakupata msaada tu. Asante.




Kiukweli nina shida nahitaji msaada.

Niko tayari kulipa kwa riba na kuandikishana kwa mwanasheria, kwasasa nipo Mkoa wa Pwani ya Kibaha.

Naomba kuwasilisha kwenu wana JF.
 




 
Yaani yeye akupe milioni afu wewe umpe mikaratasi miwili?

Cheti na milioni moja kipi ni orijino?
Ahahaha

Huwa siwalewi watu wanaoweka dhamana vyeti.

Cheti Mali ya mtu hata mdaiwa skishindwa lipa utakipeleka wapi na Hela Yako ishapotea.

Ndugu mkopaji tafuta dhamana ya kueleweka Ili ikitokea anayekukopa hujamlipa Hela yake awesa kujifidia.
 
Unadhani cheti kinaokotwa,cheti kinagharamiwa yaani mtu analipa ada ili akipate hicho cheti husika,unachokidharau.
Sure, japo hakina monetary value kuwa dhamana lakini cheti ni cha thamani sana, tunapitia magumu thats why inafka mahal tunaomba msaada, dunia ya leo mtu kukusaidia n kaz sn. Na kimfaacho mtu chake ndio maana naomba msaada kwa kigezo cha vyeti niktambua kbs hakfai kuwa dhamana, ila kw msamalia atayeguswa anisaidie angalau bas niweke vyet tu ishara kuwa nitalipa deni
 
Back
Top Bottom