Mramba, Mrisho, Mgonja, et al.. chunguni?

WHY preferential treatment?.

Ukiba kuku unapata treatment mbaya ukiiba mabilioni unapata treatment nzuri!! WOW I love BONGO.

Hilo la preferential treatment,watu wa magereza nafikiri walishalitolea ufafanuzi.walisema hata zombe hawajamuweka na watuhumiwa wengine kwasababu wapo wanatuhumiwa wenye hasira naye wanaweza kumdhulu.Zombe yuko pamoja na Jeetu na Johnson Lukaza selo moja.
 
Hawa watu wanne ??? nina hamu sana ya kujua walipo sasa hivi.. Kwani nimesikia king'ora kimelia na kuna dalili mmoja wao akawa ametoweka kimoja! Lakini kati ya wote ningependa kujua Basil Mramba leo hii yuko wapi, kuna mtu anamtafuta sana...

Huyu mtu ahabari zake tunaweza kumuuliza Lunyungu na BAK maana wao hutupaga habari za huko Bungeni. Labda tuwaulize hawa ndugu kama Mramba alihudhuria Mkutano wa Bunge ulioisha hivi karibuni.

Kaeni mkao wa kura.. kwa vile hawawezi kumfikia BM moja kwa moja.. the closest thing is to get the closest confidants.. mnakumbuka Balali alivyoondoka nchini..? Mjiulize Mgonja yuko wapi? Sitashangaa na yeye akawa ameenda US kwa matibabu na hali yake ikawa mbaya na kufia Marekani...

I think they need to add more pages kwenye kitabu chao..

Mwanakijiji, remember my thread: Ikulu iliingilia kati vigogo wasifikishwe mahakamani? Wawili ni kati ya hao uliowataja na wa tatu ni BM's close ally ambaye upo ushahidi wa wazi kuwa ni Fisadi, kilichosababisha asifikiswe mahakamani ni kuwa (kwa mujibu wa chanzo) lazima BM naye angejikuta anasimamishwa kizimbani kitu ambacho Mkulu wa Nchi hakuwa tayari kuruhusu; wengine wawili ni yale yale madai ya nchi huenda isitawalike- kisa? Mafisadi wakikamatwa! Nadhani Wakuu wamegundua kinyume chake kuwa Nchi inaweza kutotawalika ikiwa hao Mafisadi hawatafikishwa mahakamani.

Tusubiri wafikishwe Mahakamni ingawa hiyo pia inaweza kutuleta katika madai yako kuwa "Kesi za Mafisadi zimeandaliwa kushindwa!''
 
Wakuu naomba kuelimishwa

Hivi ofisi ya DPP(mkurugenzi wa mashitaka) ipo chini ya muhimili wa utawala(executive) au muhimili wa Mahakama(judiciary)?....
 
Wakuu naomba kuelimishwa

Hivi ofisi ya DPP(mkurugenzi wa mashitaka) ipo chini ya muhimili wa utawala(executive) au muhimili wa Mahakama(judiciary)?....

DPP yupo chini ya AG's chambers ( Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali) which is the Executive na siyo Judiciary
 
Kaeni mkao wa kura.. kwa vile hawawezi kumfikia BM moja kwa moja.. the closest thing is to get the closest confidants.. mnakumbuka Balali alivyoondoka nchini..? Mjiulize Mgonja yuko wapi? Sitashangaa na yeye akawa ameenda US kwa matibabu na hali yake ikawa mbaya na kufia Marekani...

I think they need to add more pages kwenye kitabu chao..

... Hadi jana jumla ya watuhumiwa 12 kati ya 20 walishapata dhamana huku kuanzia leo kukiwa na taarifa za kuwepo vigogo zaidi watakaofikishwa mahakamni hapo kwa tuihuma za wizi wa fedha za EPA.

Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa waendesha mashtaka mahakamani hapo alisema kuwa hata yeye jana alipata taarifa za kuletwa kwa Waziri mmoja aliyekuwa maarufu katika Serikali ya Awamu ya Tatu, lakini baadaye suala hilo 'liliahirishwa.'

Source Majira!
 
Siyo "Watanzania hata kama kula majani watakula lakini Ndege ya Rais itanuinuliwa"?
 
Jimbo la Rombo 2010 ni letu

Jimbo la Sumaye vipi, hamlitaki? au ngoma nzito? Jimbo la Lowassa, Karamagi, Msabaha, Ngasongwa, Chenge hayo pia msiyasahau. Ni muhimu kuongeza nguvu ya upinzani bungeni hata kama mtakosa urais.
 
DPP yupo chini ya AG's chambers ( Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali) which is the Executive na siyo Judiciary

Is that seen to be independent au ndio mambo ya kufuata the will of the CEO (President)?

Baada ya uchambuzi huu wa kina suala la kujiuliza mimi na wewe what next? umejiandaa kuifanyia nini Tanganyika/ Tanzania? Je unalosuruhiho au ndo yale yale kwamba watz kwa kupiga soga??

Change, Yes we can...
 
Shadow,
Kabla sijarukia kujibu suali lako naomba nianze kwa kusema kuwa hii issue ya separation of powers ( Executive, Parliament na Judiciary)ni tata kidogo maana tuelewe kuwa AG ana play a political role which means yuko more inclined to the Executive kama mshauri mkuu wa serikali na ndio maana hata Bungeni ni ex-officio member akiwa siyo mbunge.Anakuwa pale kutetea msimamo wa serikali.
Kikatiba, attorney general does not report to the justice minister or any other Cabinet minister (save for the prime minister).Ila kiutawala na kiutendaji Attorney General's Chambers including the DPP na hata Court of Appeal au tuseme Mahakama falls under the portfolio umbrella of the Justice Ministry na ndiyo maana hata budget zao zinapitishwa chini ya wizara ya sheria...
Hapo bado hatujazungumzia independence of the judiciary..how independent is it wakati uteuzi wa majaji hufanywa na Executive?
Sasa kwa mtaji huu labda nikuulize wewe kama mwananchi unafikiri utafanya nini to bring about the change you are advocating for?
 
Unamshukuru polisi kwa kufukuza mwizi ?

Unamshukuru Mkuu wa Tume ya kupambana na rushwa kwa kupambana na rushwa ?

Unamshukuru Mwanasheria Mkuu kwa kufuata sheria ?

Mimi ni kuli. Kwa kila mzigo ninaopakia na kupakua kwenye ya malori ya kampuni bosi anadunduliza hela sehemu kila mwisho wa siku. Zikifika wiki mbili karani wa kampuni ananipa hundi. Sijawahi kuambiwa ahsante. Tena mwenye mizigo hii, mmiliki wa kampuni, sijawahi hata kuteta nae.

Nikadai shukurani ?

Ndio hayohayo ya kumsifia baba/mama kwa kumnunulia mwanae nepi, waTZ tuna mambo sio kidogo! Tunahitaji kubadilika kifikra kabla ya viongozi wetu.
 
kuna yule aliyekuwa Katibu Mkuu P. Mangula ana clue nyingi za issue hii lakini sijaona sehemu yeyote akitajwa atoe info za EPA kwani kipindi hicho alikuwa hakauki BOT!!!!
 
Shadow,
Kabla sijarukia kujibu suali lako naomba nianze kwa kusema kuwa hii issue ya separation of powers ( Executive, Parliament na Judiciary)ni tata kidogo maana tuelewe kuwa AG ana play a political role which means yuko more inclined to the Executive kama mshauri mkuu wa serikali na ndio maana hata Bungeni ni ex-officio member akiwa siyo mbunge.Anakuwa pale kutetea msimamo wa serikali.
Kikatiba, attorney general does not report to the justice minister or any other Cabinet minister (save for the prime minister).Ila kiutawala na kiutendaji Attorney General's Chambers including the DPP na hata Court of Appeal au tuseme Mahakama falls under the portfolio umbrella of the Justice Ministry na ndiyo maana hata budget zao zinapitishwa chini ya wizara ya sheria...
Hapo bado hatujazungumzia independence of the judiciary..how independent is it wakati uteuzi wa majaji hufanywa na Executive?
Sasa kwa mtaji huu labda nikuulize wewe kama mwananchi unafikiri utafanya nini to bring about the change you are advocating for?

Women of Substance,

Asante kwa uchambuzi wako yekinifu. Nimefurahia mnyambulisho wako na nakuunga mkono katika huo mchanganuo. Kwa kuongezea Tanzania imemezwa na executive power. Hii yote inachangiwa na costitutional making ya Tanzania. Ulitegemea nini chama kikiwa kimeshika hatamu kutengeneza bomu litakalowaangamiza. Kama mimi na wewe hatuta simama kidete kuamasisha umma kuhusu mabadiliko ya kweli, tusitegemee jipya Tanzania.

Kujibu swali lako, badala ya kukaa na kuangalia kangaroo courts in action and sham proceedings, Najaribu kupanda mbegu ya uzalendo wa kweli kwa wananchi, tumeanza na passive resistance kutaka mabadiliko ya katiba kwani hapo ndipo kwenye kiini cha tatizo.

Shadow.
 
Shadow,
Kabla sijarukia kujibu suali lako naomba nianze kwa kusema kuwa hii issue ya separation of powers ( Executive, Parliament na Judiciary)ni tata kidogo maana tuelewe kuwa AG ana play a political role which means yuko more inclined to the Executive kama mshauri mkuu wa serikali na ndio maana hata Bungeni ni ex-officio member akiwa siyo mbunge.Anakuwa pale kutetea msimamo wa serikali.
Kikatiba, attorney general does not report to the justice minister or any other Cabinet minister (save for the prime minister).Ila kiutawala na kiutendaji Attorney General's Chambers including the DPP na hata Court of Appeal au tuseme Mahakama falls under the portfolio umbrella of the Justice Ministry na ndiyo maana hata budget zao zinapitishwa chini ya wizara ya sheria...
Hapo bado hatujazungumzia independence of the judiciary..how independent is it wakati uteuzi wa majaji hufanywa na Executive?
Sasa kwa mtaji huu labda nikuulize wewe kama mwananchi unafikiri utafanya nini to bring about the change you are advocating for?

Women of Substance,

Kiini ni hiyo katiba ya kiini macho. Sasa unaonaje tukianzisha mchakati kwa kujadili katiba lets say in form of "shadow consitution" and bring awareness kwa umma ambao wengi awana uwezo wa kujisimamia katika kutafuta haki zao? I can see we have something in common as far as good governance, rule of law and democracy is concerned.
 
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Rombo Mhe. Basil Pesambili Mramba anatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa KLHN imefahamishwa. Waziri huyo ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za juu tangu utawala wa awamu ya kwanza na kushika nafasi ya uwaziri katika awamu ya tatu na awamu ya nne hadi pale alipotemwa katika mabadiliko ya Mawaziri mapema mwaka huu.
Mhe. Mramba anatarajiwa kufikishwa mahakamani kutokana na makosa mbalimbali ya yanayohusiana na utendaji wake wa kazi akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara na inawezekana pia kutokana na nafasi aliyowahi kushirikia ya Wizara ya Miundo Mbinu. Wachunguzi wengine wanaelezea pia Waziri mwingine wa zamani wa serikali ya Rais Mkapa Bw. Daniel Yona naye ajiandae kukutana na kibano cha sheria.

Endapo Bw. Mramba atafikishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa atakuwa ni waziri mwingine wa serikali ya Mkapa kupanda kizimbani. Huko nyuma Bw. Nalaila Kiula aliyekuwa Waziri wa katika mhula wa kwanza wa utawala wa Rais Mkapa alijikuta akipandishwa kizimbani kufuatia mashtaka ya ufujaji wa mali ya umma yenye thamani ya zaidi ya bilioni 3 na kukutwa na hatia hata hivyo hukumu yake ilitupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa.

Kesi dhidi ya Mramba inatarajiwa kuletwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kufuatia uchunguzi wake wa msamaha wa madeni ya Alex Stewart na pia malipo ya mabilioni ya shilingi yaliyofanyika miezi michache (na wakati mwingine wiki chache) kabla ya kikomo cha muhula wa pili wa utawala wa Rais Mkapa.

Chanzo chetu katika uchunguzi huo kimeiambia KLHN kuwa "Bw. Mramba akiwa Waziri wa Fedha ndipo tunaweza kuona malipo ya kushangaza na miradi ya ajabu ikiibuka nayo ikihusisha Benki Kuu." Chanzo chetu hicho cha kuaminika chenye ujuzi wa maendeleo ya uchunguzi huo kimesema kuwa "kuanzia mwaka 2000 hadi 2005, serikali ya Tanzania chini ya Rais Mkapa iliingia na kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo ununuzi wa Rada, Ndege ya Jeti ya Rais (Mramba alinukuliwa kusema kuwa "hata ikibidi Watanzania wale majani ndege ya itanunuliwa"), wizi kutoka Akaunti ya EPA (ambapo watu zaidi ya 20 wameshafikishwa mahakamani), malipo kwa makampuni ya Mwananchi Gold, Deep Green Finance, Meremeta na kuongezewa muda kwa mkataba wa kampuni ya Makontena ya TICTS".

Chanzo hicho kimeiambia KLHN kuwa "kinyume na mawazo ya watu wengi fedha hizi nyingi hazikwenda kwenye uchaguzi wa CCM bali zilikwenda kwenye mifuko ya watu wachache katika utawala wa serikali ya Mkapa na sasa zimehifadhiwa kwenye akaunti mbalimbali duniani hasa kwenye nchi zenye sheria zinazosaidia watu kuficha fedha zao kama Uswisi, Cayman Islands, Bahamas, na Isle of Man".

Katika mazungumzo na KLHN chanzo hicho kimefafanua zaidi kuwa "kuna kiasi ambacho kilitumika katika kampeni lakini kile kikubwa kimeenda mifukoni mwa watu. Hata zile fedha za "vijisenti" vya Mhe. Chenge ni sehemu ya fedha hizo ikiwa ni malipo kwake kama Mwanasheria Mkuu kuweza kufanikisha madili yote yale na ili kumuweka katika kujua akapewa nafasi ya kugombea Ubunge ili baadaye awekwe ndani ya Baraza la Mawaziri na hivyo kuwa 'inside man' wa Mkapa katika serikali ya Kikwete".

Alipoulizwa kama kuna watumishi wengine kutoka serikali ya Rais Mkapa ambao wanakabiliwa na mkono wa sheria chanzo hicho kilisema kuwa "ingekuwa hatuna kinga ya Rais, tungemsimamisha Mkapa mwenyewe kizimbani lakini katika hili hatuna msalie mtume kwani tutawakusanyika jamaa zake hadi wa mwisho wao"!

KLHN itaendelea kukuletea taarifa zaidi kufuatia maendeleo ya mashtaka haya ambayo yanatarajiwa kuletwa wakati wowote kwani mafaili yote tayari yamesharudishwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka na baraka zote zimekwishatolewa.
 
Back
Top Bottom