Mramba, Mrisho, Mgonja, et al.. chunguni?

Mwanakijiji ni lini huyo bwana atafikishwa mahakani maaana hii story ya Mramba kufikishwa mahakamani nimeisikia kabla hata kabla ya ujio wa Yesu
 
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Rombo Mhe. Basil Pesambili Mramba anatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa KLHN imefahamishwa. Waziri huyo ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za juu tangu utawala wa awamu ya kwanza na kushika nafasi ya uwaziri katika awamu ya tatu na awamu ya nne hadi pale alipotemwa katika mabadiliko ya Mawaziri mapema mwaka huu.
Mhe. Mramba anatarajiwa kufikishwa mahakamani kutokana na makosa mbalimbali ya yanayohusiana na utendaji wake wa kazi akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara na inawezekana pia kutokana na nafasi aliyowahi kushirikia ya Wizara ya Miundo Mbinu. Wachunguzi wengine wanaelezea pia Waziri mwingine wa zamani wa serikali ya Rais Mkapa Bw. Daniel Yona naye ajiandae kukutana na kibano cha sheria.

Endapo Bw. Mramba atafikishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa atakuwa ni waziri mwingine wa serikali ya Mkapa kupanda kizimbani. Huko nyuma Bw. Nalaila Kiula aliyekuwa Waziri wa katika mhula wa kwanza wa utawala wa Rais Mkapa alijikuta akipandishwa kizimbani kufuatia mashtaka ya ufujaji wa mali ya umma yenye thamani ya zaidi ya bilioni 3 na kukutwa na hatia hata hivyo hukumu yake ilitupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa.

Kesi dhidi ya Mramba inatarajiwa kuletwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kufuatia uchunguzi wake wa msamaha wa madeni ya Alex Stewart na pia malipo ya mabilioni ya shilingi yaliyofanyika miezi michache (na wakati mwingine wiki chache) kabla ya kikomo cha muhula wa pili wa utawala wa Rais Mkapa.

Chanzo chetu katika uchunguzi huo kimeiambia KLHN kuwa "Bw. Mramba akiwa Waziri wa Fedha ndipo tunaweza kuona malipo ya kushangaza na miradi ya ajabu ikiibuka nayo ikihusisha Benki Kuu." Chanzo chetu hicho cha kuaminika chenye ujuzi wa maendeleo ya uchunguzi huo kimesema kuwa "kuanzia mwaka 2000 hadi 2005, serikali ya Tanzania chini ya Rais Mkapa iliingia na kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo ununuzi wa Rada, Ndege ya Jeti ya Rais (Mramba alinukuliwa kusema kuwa "hata ikibidi Watanzania wale majani ndege ya itanunuliwa"), wizi kutoka Akaunti ya EPA (ambapo watu zaidi ya 20 wameshafikishwa mahakamani), malipo kwa makampuni ya Mwananchi Gold, Deep Green Finance, Meremeta na kuongezewa muda kwa mkataba wa kampuni ya Makontena ya TICTS".

Chanzo hicho kimeiambia KLHN kuwa "kinyume na mawazo ya watu wengi fedha hizi nyingi hazikwenda kwenye uchaguzi wa CCM bali zilikwenda kwenye mifuko ya watu wachache katika utawala wa serikali ya Mkapa na sasa zimehifadhiwa kwenye akaunti mbalimbali duniani hasa kwenye nchi zenye sheria zinazosaidia watu kuficha fedha zao kama Uswisi, Cayman Islands, Bahamas, na Isle of Man".

Katika mazungumzo na KLHN chanzo hicho kimefafanua zaidi kuwa "kuna kiasi ambacho kilitumika katika kampeni lakini kile kikubwa kimeenda mifukoni mwa watu. Hata zile fedha za "vijisenti" vya Mhe. Chenge ni sehemu ya fedha hizo ikiwa ni malipo kwake kama Mwanasheria Mkuu kuweza kufanikisha madili yote yale na ili kumuweka katika kujua akapewa nafasi ya kugombea Ubunge ili baadaye awekwe ndani ya Baraza la Mawaziri na hivyo kuwa 'inside man' wa Mkapa katika serikali ya Kikwete".

Alipoulizwa kama kuna watumishi wengine kutoka serikali ya Rais Mkapa ambao wanakabiliwa na mkono wa sheria chanzo hicho kilisema kuwa "ingekuwa hatuna kinga ya Rais, tungemsimamisha Mkapa mwenyewe kizimbani lakini katika hili hatuna msalie mtume kwani tutawakusanyika jamaa zake hadi wa mwisho wao"!

KLHN itaendelea kukuletea taarifa zaidi kufuatia maendeleo ya mashtaka haya ambayo yanatarajiwa kuletwa wakati wowote kwani mafaili yote tayari yamesharudishwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka na baraka zote zimekwishatolewa.

Ina maana Mkapa na mme mwenza na mke wao walihusika kwenye kwenye meremeta, Deep Green Finance, Mwananchi, EPA Kagoda?

Tutapenda kusikia hizo hela zimerudishwa ziwalipe walimu na wanafunzi wa chuo kikuu wasomeshwe nazo, tungependa kuona mtu kama huyu hapewi dhamana maana wananchi tumekula majani vya kutosha.
 
jamani eeeh

mzee wa DATAZ ndio keshapewa BAN sasa mnafikiri ES angekwepo atungekuwa na inside info
 
Mwanakijiji ni lini huyo bwana atafikishwa mahakani maaana hii story ya Mramba kufikishwa mahakamani nimeisikia kabla hata kabla ya ujio wa Yesu

Ilikuwa iwe jana lakini ikaahirishwa; ni leo jioni ndio nimefahamu kwanini waliahirisha.. nitaupdate the original story in a minute.
 
Mzee wa Dataz ES ndio mshamfungia sasa sijui mtazipata wapi zingine

yale yaleee ya Mkulima kula mbegu
 
Women of Substance,

Kiini ni hiyo katiba ya kiini macho. Sasa unaonaje tukianzisha mchakati kwa kujadili katiba lets say in form of "shadow consitution" and bring awareness kwa umma ambao wengi awana uwezo wa kujisimamia katika kutafuta haki zao? I can see we have something in common as far as good governance, rule of law and democracy is concerned.

Seconded!
Anzisha basi thread nyingine tusijekuharibu mtiririko wa thread hii...
 
Ilikuwa iwe jana lakini ikaahirishwa; ni leo jioni ndio nimefahamu kwanini waliahirisha.. nitaupdate the original story in a minute.

Mzee Mkjj lete update hiyo, maana inavyoonekana hapa kuna watu wapo kwa ajili ya kuchota mawazo ya watu na kuwaondoa kwenye mwelekeo wa hii thread.

By the way yule mgonjwa wetu kule US anaendeleaje?
 
kwanini huyu mkuu wa medani afungiwe?? Kuna ukweli ktk hili au GOT umeamua kuwa kauzu.
 
Kuhani said:
Unamshukuru polisi kwa kufukuza mwizi ?

Unamshukuru Mkuu wa Tume ya kupambana na rushwa kwa kupambana na rushwa ?

Unamshukuru Mwanasheria Mkuu kwa kufuata sheria ?

Kuhani,

..nilipotuma posting ile nilikuwa na nia ya kuchokoza mjadala tupime kama hii timu ya Raisi imetimiza wajibu wake, na kwa kiwango kipi.

..nilitegemea wachangiaji makini kama wewe wangetoa hoja kuhusu mafanikio na mapungufu kuhusu kazi iliyofanyika.

..kuhusu maswali yako: Polisi akifukuza mwizi sugu na kusababisha mali aliyoiba kupatikana, hata kama asipomkamata mwizi yule, wananchi wanaweza kumpa asante/pongezi.

..tunaweza kumshukuru Mkuu wa Taasisi ya Rushwa ya serikali ya CCM kwa kujirudi na kuamua kupambana na rushwa. tunapofanya hivyo siyo lazima tuwe tumeridhika na kazi yake, bali ni kumpa moyo apambane na rushwa kubwa zaidi.

..zingatia kwamba tunaishi ktk Tanzania inayoongozwa na CCM.


Kitila Mkumbo said:
Ndio hayohayo ya kumsifia baba/mama kwa kumnunulia mwanae nepi, waTZ tuna mambo sio kidogo! Tunahitaji kubadilika kifikra kabla ya viongozi wetu.

Kitila Mkumbo,

..sijui Chadema mmejiandaa vipi with these developments.

..sidhani kama mlifanya kazi ya kuridhisha katika ku-establish a link btn rushwa na wizi huu na CCM na kampeni za uchaguzi.

..pia mmeelekeza nguvu nyingi kumuandama Raisi mstaafu kuliko huyu ambaye yuko madarakani.

..nadhani the end game ni JK kujikosha mbele ya wananchi kwamba anashughulikia rushwa, na kupata huruma na imani ya wananchi.

..nilitegemea ungejielekeza kujenga hoja ktk masuala hayo hapo juu, badala yake umekuja na hoja ya BABA na NEPI!!!
 
Kaeni mkao wa kura.. kwa vile hawawezi kumfikia BM moja kwa moja.. the closest thing is to get the closest confidants.. mnakumbuka Balali alivyoondoka nchini..? Mjiulize Mgonja yuko wapi? Sitashangaa na yeye akawa ameenda US kwa matibabu na hali yake ikawa mbaya na kufia Marekani...

I think they need to add more pages kwenye kitabu chao..
cjakusoma mkuu..clarifications please...
 
Niachieni jimbo langu jamani....Rombo 2010 for a change!! teh teh teh teh

Ushi wa Rombo

Nadhani mkuu wewe ndiye utakayeni-endorse ktk dakika za mwisho,yaani wewe ndiye utakaekua Colin Powell wangu .Teh teh teh! Aika mmeku.
 
Wakuu huyu Mramba nimelia nae sana hapa JF lakini nilikua nashangaa kwanini yeye alikua haguswi.

Ni wakati sasa wa kumkomalia mpaka kieleweke
 
Back
Top Bottom