Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,897
- 941
MKUTANO WA MJADALA WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UHIMALISHAJI YA MILIKI YA ARDHI (LAND TENURE IMPROVEMENT PROGRAM)
Tumefungua mkutano wa mjadala wa Utekelezaji wa Mradi wa uhimalishaji Salama ya Miliki za Ardhi yaani Land Tenure Improvement Program. Mradi huu unakwenda kupima, na kutambua Vipande vya Ardhi katika Mikoa 16, Halmashauri 41 na Ujenzi wa Miundombinu ikiwemo Majengo ya Makamishna wa Ardhi Mikoa yote ya Tanzania Bara na kufunga Mifumo ya kiteknolojia kwa ajili ya kurahisisha upimaji na utambuzi katika utawala wa Ardhi.
Gharama ya Mradi mzima ni Shilingi Bilioni 345 Mkopo toka Benki ya Dunia.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb)
#KaziInaendelea
#ArdhiYetu