Mjadala wa ClubHouse ya JamiiForums: Kero ya Rushwa katika Umiliki wa Ardhi

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
1691379545993.jpeg

Umewahi kulazimika kutoa rushwa ili uweze kukamilishiwa mchakato wa kumiliki ardhi?

Jiunge nasi Alhamisi, Agosti 10, 2023 Saa 12 Jioni hadi saa 2 usiku kupitia ClubHouse ya JamiiForums kujadili Vitendo na Mazingira ya Rushwa katika hatua za Umiliki wa Ardhi Nchini.

Tutajadili Changamoto, Suluhisho, na njia za kuboresha Hali ya umiliki wa Ardhi, ili kujenga Jamii yenye Haki na Uwazi katika Umilikishwaji wa Rasilimali Nchini.

Pia unaweza kuandika maoni yako katika uzi huu yatasomwa siku ya mjadala.

---

- Mjadala umeanza

Baadhi ya mawazo na hoja zilizotolewa wakati wa mjadala

Mjadala kuhusu Vitendo na Mazingira ya Rushwa katika hatua za Umiliki wa Ardhi Nchini unaendelea muda huu kupitia Mtandao wa ClubHouse na XSpaces za JamiiForums.

George Joseph Miringay (Afisa Mipango Miji Mwandamizi Ofisi ya Rais TAMISEMI): anasema umiliki wa ardhi una hatua tatu, kwanza ni Mipango Miji, Kupima na tatu ni Umiliki.

Kumiliki ardhi si hiyari, mtu anapoanza hatua za kwanza lazima zifanyie ili apate nyaraka, ikifika hatua ya umiliki rasmi ni hiyari na watu wengi hawapendi kumiliki ardhiUkipata Hati utaanza kuchajiwa kodi ya ardhi, ndio maana kuna watu wengi wana nyaraka za umiliki wa ardhi lakini hawataki kwenda kumiliki ardhi, kutofanya hivyo kunawapa nafasi matapeli kwenda kuzunguka nyuma ya pazia na kufanya utapeli.

Kuna nafasi kubwa ya watu kutengeneza nyaraka bandia za ardhi, wanatumia udhaifu wa watu kutoelewa michakato inavyotakiwa kufanyikaWakiona mtu ambaye anamiliki ardhi kihalali hana uelewa huo au nafasi ya kujua afanye nini, kunawapa nafasi watu wengine kufanya utapeli kwa siri.

Watu hawapendi kumiliki Ardhi, mfano kuna Halmashauri ambazo hadi ‘control number’ zimetoka kwa ajili ya kwenda kuanza kulipia Hati lakini Watu hawafanyi hivyoAngalau Dar es Salaam kuna uelewa tofauti na sehemu nyingine, ndio maana kuna wakati Waziri wa Ardhi aliwasisitiza watu wakachukue Hati zao, waende wakachukue ili waanze kulipa.

Mhandisi Ndolezi Petro (Waziri Kivuli wa Sekta ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi -ACT Wazalendo): Nashangaa kusikia kuwa watu hawataki kumiliki Ardhi, nadhani ni kasi ndogo ya Mamlaka na ndio maana mpaka sasa wapo katika 25% ya upimaji na urasimilishaji wa masuala ya Ardhi.

Mathew N. Nhonge (Kamishna wa Ardhi): Mifumo yetu ya upimaji inafanana, baadhi ya maeneo yalipimwa zamani mfano miaka ya 1970 kuna teknolojia mpya ambayo inaweza kutumika kufanya vipimo japo si katika maeneo yoteSasa hivi tuna mifumo inayokusaidia kubaini kama sehemu imeshapimwa au la, ikiwemo kupima picha za anga ambazo zinasaidia kuona eneo limeendelezwa au halijaendelezwa.

Idadi ya watu wanaoenda kujiandikisha ni kubwa, takwimu zinaonesha wanaongezeka. Ukipiga hesabu tulikotoka na tulipo kasi ni kubwa, mahitaji ya watu katika kupanga na kupima ni makubwaHalmshauri zinafanya kazi kubwa na tunaona mahitaji na fursa ni kubwa

Tuliona mtu anaweza kupima na kubaki na ramani, tukakubaliana kuwa eneo linapokuwa limepangwa, ndani ya siku 90 mhusika anatakiwa kuingizwa kwenye mfumo wa umiliki Sheria ya Ardhi Namba 4 ya Mwaka 1999 inaeleza kuwa unapopimiwa ardhi unatakiwa kuwasilisha maombi ya Hati ndani ya muda huo.

Kuna Hati zimetoka zaidi ya 20,000 lakini Wananchi hawajaja kuzichukua, pamoja na hivyo inawezekana wanaona Wizara ni sehemu sahihi kwa wao kuhifadhi nyaraka hizo. Teknolojia yetu miaka ya nyuma ilikuwa nyuma, kinachofanyika ni kuwa tunabadilisha kutoka katika mfumo wa zamani na kuwa katika mfumo wa sasa.

George Joseph Miringay (Afisa Mipango Miji Mwandamizi Ofisi ya Rais TAMISEMI): Kupanga na kupima kuna utaratibu wake na haliwezi kufanya kwa kiwanja kimoja kimoja, inaweza kufanyika kwa Mtaa au zaidi ya hapo. Pia, kabla ya kufanyika yote hayo lazima Wananchi wawe wameshaweka utaratibu mzuri wa mipaka yao.

Sheria ya Serikali za Mtaa ya Mwaka 1982 inaonesha maamuzi yote ya Mtaa yanapita kwenye Halmashauri, hivyo zoezi zima la kupanga hadi kumilikisha haliwezi kwenda zaidi ya miezi mitatu kama kila kitu kipo.

Ucheleweshwaji wa Hati mara nyingi unafanyika katika Hatua ya Kupanga, mfano tunaweza kutangaza kuwa tunapita mtaa fulani, ukienda huwakuti watu. Inaweza kumalizika miezi mitatu bila kupata taarifa rasmi na wakati mwingine migogoro ni changamoto.

Mathew N. Nhonge (Kamishna wa Ardhi): Kuna program tulizoanzisha kutatua changamoto za migogoro ya ardhi Nchi nzima, Wakuu wa Wilaya wanasimamia zoezi hilo katika maeneo yote wakiwa na Makamishna wa Ardhi.

Mhandisi Ndolezi Petro: Mchakato wa Hati Miliki unaweza kuwa na mambo mengi hapo katikati, ukweli ni kuwa Sekta ya Ardhi ina migogoro mingi Dhana ya Urasimishaji wa Ardhi inajenga dhana kuwa bidhaa inayoweza kuuzika sokoni, ndio maana kuna Taasisi ambazo zimetumia Ardhi kama dhamana

Kuna kundi kubwa la Wanyonge ambao wameshindwa kumudu mikiki ya umiliki wa ardhi, mwisho wamejikuta wakiuza Ardhi wanazomiliki kutokana na kutokuwa na nguvu ya kiuchumi.

Serikali iliunda Kamati ya Mawaziri 8 wa Kisekta kushughulikia migogoro ya Ardhi lakini ni kama wameshindwa kumudu kumaliza migogoro mingi inayoendelea maeneo tofauti

Migogoro mingi inayoendelea katika ardhi kwa asilimia kubwa inasababishwa na uelewa mdogo wa Wananchi kuhusu masuala ya ArdhiWito wetu ACT ni kuwa Upangaji na Urasimishaji viende kwa kasi.

Petro (Mwananchi): Nilinunua nyumba yenye Hati, nikaanza mchakato wa kubadili umiliki, nilipata usumbufu mkubwa sana. Kuna watu wakanijulisha kuwa ili nifanikiwe lazima nitumie ‘kishoka’, sikutaka kufanya hivyo, nikaenda kufuata hatua zote, nilizungushwa kuanzia ngazi za Halmashauri na TRAKila ukienda lazima watafute njia za kukuzungusha ili ulainishe mambo, nilipata usumbufu mkubwa kote huko isipokuwa Wizarani tu.

Mathew N. Nhonge (Kamishna wa Ardhi): Urasimishaji unafanyika katika maeneo ambayo Wananchi wameendeleza lakini hawana nyaraka, hivyo wanapopata nyaraka ndio inaitwa urasimishaji. Maeneo ya Vijiji hatuiti urasimishaji, wengi wao wanamiliki maeneo Kimila, ndio maana tuna Sheria ya Ardhi ya Vijiji na ile ya Mjini.

Ardhi inaweza kumilikiwa kwa kununua, kurithi au kupewa. Utaratibu wa kuvamia hauwezi kukupa ardhi, unapofanya hivyo unakuwa umetenda kosa.

George Joseph Miringay (Afisa Mipango Miji Mwandamizi Ofisi ya Rais TAMISEMI): Mchoro wa Mipango Miji unaweza kubadilishwa kila baada ya miaka mitano, kabla ya hapo pia kunaweza kufanyika mabadiliko madogo madogo, mfano, idadi ya watu inapoongezeka inaweza kuchangia mabadiliko

Watu wanaweza kupita kwenye kiwanja cha mtu na wasijue kama ni kiwanja cha mtu, inaweza kuwa hivyo kwa watu kutumia kama Barabara lakini kunapofanyika urasimishaji kunatengeneza faida ya kuwa na maeneo rasmi yanayotambulika.

Mchoro wa Mipango Miji unaweza kubadilishwa kila baada ya miaka mitano, kabla ya hapo pia kunaweza kufanyika mabadiliko madogo madogo, mfano, idadi ya watu inapoongezeka inaweza kuchangia mabadiliko.

Watu wanaweza kupita kwenye kiwanja cha mtu na wasijue kama ni kiwanja cha mtu, inaweza kuwa hivyo kwa watu kutumia kama Barabara lakini kunapofanyika urasimishaji kunatengeneza faida ya kuwa na maeneo rasmi yanayotambulika.

Evelyne Mugasha (Mthamini Mkuu wa Serikali): Kabla ya Mwananchi anayetakiwa kuhamishwa kulipwa fidia, atalipwa pia fidia ya mazao, nyumba na ardhiMfano mtu akiwa na nyumba kabla ya kuhamishwa fidia inatakiwa kuhesabu kuwa ili aje ajenge nyumba nyingine inaweza kumchukua miaka mitatu, hivyo anatakiwa kulipwa kodi ya miaka mitatu.

Ofisi yangu ndio inapitisha fidia ya nyumba na ardhi, Kanuni tunazotumia ni za Uthamini za Mwaka 2018, mara nyingi Wananchi wanajua wakichelewa kulipwa fidia lazima walipwe na ribaUkisoma Sheria inasema tutalipa kwa kiwango cha BOT, zamani riba ilikuwa inaendelea lakini sasa hivi ikifika miaka miwili inafutwa uthamini unaanza upya

Regan (Mwananchi): Viongozi wengi wa Serikali wanazungumza mambo mazuri kuhusu ardhi ambayo ni nadharia, hayaendani na uhalisia ulivyo mtaaniNilienda Kibaha, Aprili 2023 kufuatilia Hati, nililipa kila kitu licha ya kusumbuliwa sana lakini hadi leo (Agosti 2023) sijapata Hati na sijui kinachoendelea
 
Back
Top Bottom