Nov 10, 2023
7
2
(fungu la 24 - 30)

UTANGULIZI

Mwongozo huu wa umiliki kwa ajili ya raia wa Tanzania unatokana na fungu la 24 - 30 la sheria ya ardhi Na. 4 ya mwaka 1999. Aidha, ardhi inayoombewa milki inaweza kuwa kwenye mojawapo ya makundi yafuatayo kwa maeneo ya mijini hapa Tanzania.

Ardhi inayotolewa na Serikali kwa waombaji mbalimbali

Ardhi hii ni ile ambayo imetwaliwa kwa wenyeji, ikalipiwa fidia, ikapangwa kwa matumizi mbalimbali, ikapimwa na kugawiwa kwa waombaji mbalimbali kwa mujibu wa taratibu, kanuni na Sheria za kugawa ardhi nchini. Mfano wa ardhi aina hii ni ardhi ya mradi wa viwanja 20,000.

Ardhi inayomilikiwa kiasili

Hii ni ardhi ambayo tayari inamilikiwa na woambaji tangu asili, kisha wanatekeleza taratibu za kupima kwa gharama zao na kuomba kumilikishwa kisheria katika mamlaka husika.

ARDHI INAYOTOLEWA NA SERIKALI KWA MAKUNDI MBALIMBALI

IKIWA MWOMBAJI NI MTU BINAFSI

Atawasilisha Fomu Na. 19 ya Maombi ya Haki ya kumiliki Ardhi iliyojazwa kikamilifu. Ona fomu hapa chini.

Land Form No. 19

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

THE LAND ACT, 1999

(No. 4 OF 1999)

APPLICATION FOR RIGHT OF OCCUPANCY

(Under section 25)​

This application shall be sent to the Commissioner/Authorized Officer ...............................

.............................................................................................................................

I/We hereby apply for the grant of a long term right of occupancy over the land..................................................................................................................

Citizenship ........................................................................................................

Purpose/use of land applied .................................................................................

........................................................................................................................

I/We hereby declare that I/We hold other land as follows:

...................................................................................................................................................................................................................................................

Other facts which are relevant to the application e.g disability,widow/widower, orphan, guardian ...........................................................................................................

.......................................................................................................................

Date ............................................. Name .........................................................

Business Address ...............................................................................................

........................................... Residential Address ................................................

I/We declare that what is stated above is true to my/our knowledge.

Signature .................................. Fee: ...............................................................

FOR OFFICIAL USE

...............................................................................................................................................................................................................................................................

REF: No. ............................................................................................................

Acknowledgement of receipts

For Official use only
Approcal/Rejected
Remarks ...............................................
............................................................
............................................................
............................................................
Commissioner for Lands/Authorized Officer

Date: ............................................................

____________________________

Signature of Applicant​

Served upon me/us Date: ................................................

Uthibitisho wa uraia wa mmiliki i.e. nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa au passport (hati ya kusafiria).

Ofisi yenye mamlaka husika itahakiki maombi yaliyowasilishwa.

Ankara ya malipo stahili juu ya maombi yaliyowasilishwa inaandaliwa na mamlaka husika na kisha kukabidhiwa kwa mwombaji kwa ajili ya kufanya malipo.

Mwombaji kuwasilisha stakabadhi za malipo kwa kumbukumbu za ofisi na atakabidhiwa fomu ya ushuhuda wa malipo (Acknowledgement form).

Nakala tatu za rasimu za hati zitaandaliwa baada ya kupata ramani ndogo (Deed Plan) na kukabidhiwa kwa mwombaji kwa ajili ya kusaini mbele ya mashahidi wanaotambulika kisheria.

Mwombaji atarejesha nakala 3 za hati kwa ajili ya kusainiwa na Kamishna wa Ardhi na kuelekezwa kwa Msajili wa Hati kwa hatua za Usajili.

Baada ya taratibu za usajili kukamilika mwombaji atakabidhiwa hati yake katika ofisi ya Msajili wa Hati wa Kanda husika.

IKIWA MWOMBAJI WA ARDHI HUSIKA NI TAASISI CHINI YA WADHAMINI WALIYOSAJILIWA NA (REGISTERED TRUSTEES)

Atawasilisha Fomu Na. 19 ya Maombi ya Haki ya kumiliki Ardhi iliyojazwa kikamilifu. Ona fomu hapa chini.

Ofisi yenye mamlaka husika itahakiki maombi yaliyowasilishwa.

Nakala mbili (2) za kibali cha kumiliki ardhi husika kutoka kwa Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali (Administrator General).

Nakala mbili (2) za Cheti cha Usajili zilizothibitishwa kuwa nakala ya cheti halisi.

Ankara ya malipo stahili juu ya maombi yaliyowasilishwa inaandaliwa na mamlaka husika na kisha kukabidhiwa kwa waombaji kwa ajili ya kufanya malipo.

Waombaji watawasilisha stakabadhi za malipo kwa kumbukumbu za ofisi na atakabidhiwa fomu ya ushuhuda wa malipo (Acknowledgement form).

Nakala tatu za rasimu za hati zitaandaliwa baada ya kupata ramani ndogo (Deed Plan) na kukabidhiwa kwa mwombaji kwa ajili ya kusainiwa Wadhamini wa Taasisi husika na kugonga lakiri yao (seal).

Waombaji watarejesha nakala 3 za hati kwa ajili ya kusainiwa na Kamishna wa Ardhi na kuelezwa kwa Msajili wa Hati kwa hatua za Usajili.

Baada ya taratibu za usajili kukamilika waombaji watakabidhiwa hati yake katika ofisi ya Msajili wa Hati wa Kanda husika.

IKIWA MWOMBAJI WA ARDHI HUSIKA WATAKUWA KAMPUNI

Atawasilisha Fomu Na. 19 ya Maombi ya Haki ya kumiliki Ardhi iliyojazwa kikamilifu. Ona fomu hapa chini.

Ofisi yenye mamlaka husika itahakiki maombi yaliyowasilishwa.

Nakala mbili (2) ya Memorandum and Articles of Association za Kampuni husika ambazo kurasa zake zmethibitishwa kama nakala halisi.

Nakala mbili (2) za Cheti cha Usajili cha Kampuni kutoka kwa Msajili wa Kampuni (Certificate of Incorporation) zilizothibitishwa kuwa nakala halisi.

Uthibitisho wa uraia kwa wenye hisa wakubwa wa Kampuni (Majority Shareholders) vyote ikiwa vimethibitishwa kama nakala halisi.

Ankara ya malipo stahili juu ya maombi yaliyowasilishwa inaandaliwa na mamlaka husika na kisha kukabidhiwa kwa mwombaji kwa ajili ya kufanya malipo.

Waombaji kuwasilisha stakabadhi za malipo kwa kumbukumbu za ofisi na watakabidhiwa fomu ya ushuhuda wa malipo (Acknowledgement form).

Nakala tatu za rasimu za hati zitaandaliwa baada ya kupata ramani ndogo (Deed Plan) na kukabidhiwa kwa waombaji kwa ajili ya kusaini na Wakurugenzi wa Kampuni husika au Katibu wa Kampuni na kugongwa lakiri (seal) ya kampuni.

Waombaji watarejesha nakala 3 za hati kwa ajili ya kusainiwa na Kamishna wa Ardhi na kuelezwa kwa Msajili wa Hati kwa hatua za Usajili.

Baada ya taratibu za usajili kukamilika mwombaji atakabidhiwa hati yao katika ofisi ya Msajili wa Hati wa Kanda husika.

IKIWA MMILIKI WA ARDHI HUSIKA ATAKUWA TAASISI YA UMMA

Nakala ya Sheria iliyopitishwa na bunge iliyoanzisha au kuzalisha hiyo Taasisi ya Umma au Shirika la Serikali.

Ankara ya malipo stahili juu ya maombi yaliyowasilishwa inaandaliwa na mamlaka husika na kisha kukabidhiwa kwa mwombaji kwa ajili ya kufanya malipo.

Waombaji kuwasilisha stakabadhi za malipo kwa kumbukumbu za ofisi na watakabidhiwa fomu ya ushuhuda wa malipo (Acknowledgement form).

Nakala tatu za rasimu za hati zitaandaliwa baada ya kupata ramani ndogo (Deed Plan) na kukabidhiwa kwa mwombaji kwa ajili ya kusainiwa na waliodhinishwa kwa mujibu wa Sheria ya Taasisi husika.

Waombaji watarejesha nakala 3 za hati kwa ajili ya kusainiwa na Kamishna wa Ardhi na kuelezwa kwa Msajili wa Hati kwa hatua za Usajili.

Baada ya taratibu za usajili kukamilika waombaji watakabidhiwa hati yao katika ofisi ya Msajili wa Hati wa Kanda husika.

IKIWA MWOMBAJI NI TAASISI NYINGINE

Atawasilisha Fomu Na. 19 ya Maombi ya Haki ya kumiliki Ardhi iliyojazwa kikamilifu. Ona fomu hapa chini.

Ofisi yenye mamlaka husika itahakiki maombi yaliyowasilishwa.

Sheria iliyoanzisha taasisi hiyo au Cheti cha Usajili cha taasisi husika.

Kuwasilisha uthibitisho wa Uraia wa wenye taasisi uliothibitishwa kama nakala halisi.

Ankara ya malipo stahili juu ya maombi yaliyowasilishwa itaandaliwa na mamlaka husika na kisha kukabidhiwa kwa waombaji kwa ajili ya kufanya malipo.

Waombaji watawasilisha stakabadhi za malipo kwa kumbukumbu za ofisi na atakabidhiwa fomu ya ushuhuda wa malipo (Acknowledgement form).

Nakala tatu za rasimu za hati zitaandaliwa baada ya kupata ramani ndogo (Deed Plan) na kukabidhiwa kwa mwombaji kwa ajili ya kusaini walioidhinishwa kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha Taasisi husika na kugongwa lakiri (seal).

Waombaji atarejesha nakala 3 za hati kwa ajili ya kusainiwa na Kamishna wa Ardhi na kuelezwa kwa Msajili wa Hati kwa hatua za Usajili.

Baada ya taratibu za usajili kukamilika waombaji watakabidhiwa hati yao katika ofisi ya Msajili wa Hati wa Kanda husika.

Imeandaliwa na Danvast Land and Property
 
Back
Top Bottom