Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

a)Huyu jamaa kaleta mikataba ya kanisa na serikali =Upendeleo dahiri ulaaniwe!
b) kama kuna mtu ameona kuna mkataba kati ya serikali na Wailamu aulete ndio tujadili
lakini kwa sasa evidence iliyopo ni kwamba "serikali inapendele wakrsto" kwa kuweka mkataba wa siri,
Wachangiaji wakristo wanaona raha kanisa kunyonya walipa kodi==Huo unaitwa "Unafiki"
 
Sitaki kuamini hili lakini uvumi huu umeeneea

Ok.. tutaujadili at face value.
sana kiasi cha kwamba umenifanya niwe na shauku kutaka kujua yaliyojiri kwenye kusign hiyo memorandum

Hii MoU ilisainiwa lini, na nani, na wapi? tuweze kujua msingi wake.
maana naona kwa taarifa nilizokuwa nazo

taarifa gani hizo?

malalamishi ni kuwa serikali imeipa CCT na TEC nguvu kubwa ajabu na matokeo yake leo watu watu wanaanza kulalama kwa nini serikali haiipi nguvu hizo NGO zingine kama walivopewa na serikali.

kwa hiyo hii CCT na TEC walisaini hiyo MoU pamoja?

Na under this memorandum seriali inatoa nafasi za kazi kwa Church candidates kwenye chuo chake cha Teachers Training College

Hiki Chuo cha serikali cha Teachers Training College kiko mkoa gani?

Hakuna ubaya hata kidogo kwa serikali kusign hii memorandum

Kama hakuna ubaya, hakuna malalamishi! Kuna malalamishi hivyo kuna ubaya.

lakini nataka kujiuliza je ni sawa serikali kufanya agreements kama hizi na taasisi za kidnini?

that is a huge leap! tuestablish kwanza without a doubt that there is such an agreement. Kwa sababu jambo kama hilo ni kinyume na Katiba, period.

na Je imefanya gareement kama hii na taasisi za Kisslam au wahindu au ni Kanisa tu ndio walifanya nao?

Unazungumza kana kwamba this is an established fact. Kama kuna mkataba wa aina hiyo kati ya serikali na Kanisa lolote inabidi kesi ya Kikatiba ifunguliwe kwani ina vunja "non-discrimination clause" ya Katiba yetu, haijalishi ina lengo zuri kiasi gani. Na kwa vile kuna wasomi wengi tu wa Kiislamu na maprofesa wa sheria nina uhakika taasisi za Kiislamu na za dini nyingine zinaweza kufungua kesi ya Kikatiba kwanini serikali iingie mkataba wa aina hiyo.

Je hamuoni hapo mambo ya bilateral negotiations wakaachiwa wataalam wa mambo hayo?

Kwani tumeambiwa waliosaini au watakaosaini hizo "bilateral negotiations" siyo wataalamu wa mambo hayo? Hiyo inference umeipata wapi kwenye huo "mkataba"?
 
a)Huyu jamaa kaleta mikataba ya kanisa na serikali =Upendeleo dahiri ulaaniwe!

Jifunze kureason vizuri. Mikataba ya kanisa na serikali umeiona wapi na nani kaileta?
b) kama kuna mtu ameona kuna mkataba kati ya serikali na Wailamu aulete ndio tujadili

Kwani nani kadai kuna mikataba hiyo?

lakini kwa sasa evidence iliyopo ni kwamba "serikali inapendele wakrsto" kwa kuweka mkataba wa siri,

inaonekana hujui maana ya "evidence". Hivi hiki ulichokiona humu unaweza kukisimamisha mahakamani na kudai ni evidence?

Wachangiaji wakristo wanaona raha kanisa kunyonya walipa kodi==Huo unaitwa "Unafiki"

umejuaje kanisa linanyonya walipa kodi?
 
GT,
Mkuu ndio hapo naposema kila siku watu wanakataa OIC bila kujua wala kufikiria kwa sababu tu kuna jina la Uislaam lakini ni serikali hiyo hiyo imeweka mikataba kibao na Taasisi za Kikristu kwa kutumia jina la Vatican ambayo ni Taasisi ya kidini vile vile.

Fundi Mchundo,
Mkuu unakataa hili kwa sababu kiingereza kilichotumika ni kibovu au?..Hivi katika akili yako unafikiri watu hawafdahamu mikataba ambayo serikali imekwisha ingia na taasisi za kidini?..Au kwa sababu hazitangazwi isipokuwa inapofikia za Kiislaam basi kila mtu hupiga kelele hata mwenye kulala huamka..Mkuu hatusemi tuu na mjue kwamba Waislaam ni watulivu sana kiasi kwamba ingekuwa maswala mengi yametokea upande wa pili sidhani kama nchi ingekalika..

Mkandara. Huu unaoitwa mkataba ni forgery. Hii haihusiani na kuwepo au kutokuwepo kwa makabuliano kya kushirikiana kati ya serikali katika nyanja mbalimbali. Mbona serikali ina shirikiana na Bakwata (institution ya waislamu), na Hindu Mandal (hospitali ya wahindu), Aga Khan ( taasisi ya kiislamu ), Chuo Kikuu cha Tumaini ( taasisi ya wamisheni), hospitali ya KCMC (taasisi ya wamisheni) n.k.? Ninachopinga ni kutuwekea kitu ambacho ni blatantly forgery kwa nia ya uchonganishi. Tukiangalia tena mada iliyo mbele yetu:

1) mwandishi anadai katika hiyo MoU kuna makubaliano ya kupewa upendeleo wa AJIRA kwa wakristu katika vyuo vya walimu vya serikali! CCT na TEC wataanzaje kuwaombea nafasi za KAZI (sio elimu) kwa watu wao (ambao ni sehemu kubwa ya wamisheni wote ) katika taasisi za serikali yao! Hao ambao mwandishi anadai ni watu wa CCT na TEC si raia wa nchi hii na wana kila haki ya kupata ajira huko? Au mwandishi anataka kutuambia kuwa CCT na TEC wameona kuna vizuizi kwa wamisheni kuajiriwa hadi waombe upendeleo maalum? Hivi kweli kuna upungufu wa wamisheni katika vyuo vya ualimu nchini?

2) CCT haina watu wake. Hiki ni chombo kinachounganisha baadhi ya madhehebu ya wamisheni. Hayo madhehebu ndiyo yana watu (tukichukulia kuwa hii ina maana ya wafuasi wake). Kwa hali hiyo upendeleo huo utakuwa vigumu kuutekeleza maana kila dhehebu litataka watu wake ndio wapate upendeleo! Au mwandishi anataka kutuambia kuwa upendeleo huo wa ajira utakuwa kwa wafanyakazi wa CCT? Hauoni ni upuuzi kwa CCT waombe ajira kwa waajiriwa wao! Ili iwaje?

3) Tunaposema serikali katika upuuzi huu tuna maanisha nani? Mnataka kutuambia Rais wa nchi ndiye amesaini mkataba huu? Au Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha? Au waziri wa Fedha? Au Hawa Ghasia? Nani basi ndiye ataiwakilisha serikali katika utekelezaji wa MoU?

Aliyeuweka huu unaodaiwa kuwa ni MoU ni Agent Provocateur. Na wengine wenu kwa vile kila wakati wanapenda kuona kuwa wameonewa wameingia mkenge! Mbaya zaidi hamkawii ( hasa wewe Mkandara) kuja na lugha ya vitisho. Kwani ni waislamu peke yao walioonewa na serikali yetu? Mbona wamisheni na wahindu hawakulalamika wakati rasilmali zao zilipopokonywa na serikali? Si walijua nia na makusudi ilikuwa kutoa nafasi kwa raia wote wa nchi hii kufaidika na rasilmali hizo. Ndivyo inavyotakiwa.

Kama nilivyosema awali. Tuoneeni huruma raia wa nchi yetu.

Amandla........
 
Fundi.. swali jingine ambalo liko wazi kabisa ni juu ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu kutoka katika majengo yaliyokuwa Chuo cha Tanesco (cha serikali). Hivi taasisi ya Waislamu imeweza vipi kupewa jengo la serikali bila ya mkataba? Je ni kinyume cha sheria? Je chuo hicho ni kwa ajili ya waislamu tu?

Mahusiano ya serikali na taasisi au vyombo vya kidini yapo na yameendelea kuwepo. TAtizo ni upotoshaji wa yale makubaliano. Kwa mfano mtu akija na kusema kuwa kwenye mkataba wa chuo kikuu cha Waislamu Morogoro kuna kipengele kinachosema "The University shall be used solely and exclusively for the education of the Muslim community" tutaanza kujadili kipengele hicho kwa jazba zote!
 
Fundi.. swali jingine ambalo liko wazi kabisa ni juu ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu kutoka katika majengo yaliyokuwa Chuo cha Tanesco (cha serikali).

"The University shall be used solely and exclusively for the education of the Muslim community" tutaanza kujadili kipengele hicho kwa jazba zote!

Hiki chuo kikuu tangu wapewe ndugu zetu ....hawajaongeza hata banda moja...wakati huo wenzao wamejenga vyuo vikuu vipya lushoto,moshi,makumira,iringa ,mwanza,dodoma,dar es salaam etc hivi ni mbali vyuo vikuu vya kcmc,bugando na nyegezi ambavyo kabla vilikuwa vimetaifishwa..... hii ingetakiwa iwe changamoto....,nadhani tushindane kuwaletea wananchi maendeleo,si maneno!

tungependa kuona chuo kikuu cha waislamui nacho kikipanuka ....na kutapakaa nchi nzima ili watu wapate huduma...mnaonaje kama waislamu wangesaidia serikali kwa kuwapa hospitali ya rufaa kigoma au lindi ambako maendeleo ni duni na ni wazi ni kati ya maeneo yenye waumini wengi wa kiislamu.....kuliko kupiga maneno matupu hapa kijiweni..!!! nitashangaa kama mtu atataka kuleta ubishi hata kwenye hili...au kusema kuna upendeleo...wakati wenzao kila jumapili wanatoa sadaka maalum makanisani kuchangia maendeleo ya elimu....!!!
 
People are talking as if the government has never signed agreements with Islamic groups. Did it not sign off to BAKWATA the former TANESCO College? We did not complain because we saw it as a good thing. It is very good for the government to encourage our Muslim brothers to take education more seriously.

Mkandara says that he has argued, in the past, that The Vatican is not only a state but an institution. His must have been a bad argument because the Vatican is certainly a state and not an institution. This state happens to be the headquarters of a certain institution called The Catholic Church. The state of Vatican and the institution that is the Catholic Church are headed by one and the same person, but that does not obliterate the distinction between them. If you can bear the profanity, then you may compare the relationship between the Vatican and the Catholic Church to that which exists between CCM and the state of Tanzania.

I see that some are assuming that there was a secret deal between the government and the Churches. That is hardly so. GT has seen the agreement. Is he privy to secret governmental agreements? I am convinced that our Churches would not sign secret deals with the dubious characters that presently inhabit the corridors of power in Dar.

Let me end by assuring all and sundry that the JK government has not suddenly fallen in love with the Churches. It is simply worried sick about losing the next elections, and it will do and promise anything to win. I assume that Church leaders will not be swayed by these moves.
 
Wakuu wangu,

Tutumie juhudi zetu kuhakikisha kuwa mambo ya dini hayatugawi. Imani zetu zibaki kwenye mioyo na matendo yetu. Tusijiingize kwenye unafiki na kuleta mfarakano. Wajibu wa serikali nikukusanya kodi na kutoa huduma za jamii kwa watu wake wote. Serikali inao pia wajibu wakutoa haki sawa kwa raia wake wote bilakujali kabila, dini wala ukanda. Serikali inayoligawa taifa lake kwamisingi ya udini nihatari na inapaswa kukemewa.
 
Kama hamtuwekei full MoU, mjadara ufungwe maana inawezekana tunajadiri kitu kisichokuwepo. Isije kuwa ni janja ya watu kututoa katika mijadara mizito ya Cheyo na Spika, Selelii na Spika, Zitto na Spika nk.
 
Ok.. tutaujadili at face value.

Hii MoU ilisainiwa lini, na nani, na wapi? tuweze kujua msingi wake.

taarifa gani hizo?

kwa hiyo hii CCT na TEC walisaini hiyo MoU pamoja?

Hiki Chuo cha serikali cha Teachers Training College kiko mkoa gani?

Kama hakuna ubaya, hakuna malalamishi! Kuna malalamishi hivyo kuna ubaya.

that is a huge leap! tuestablish kwanza without a doubt that there is such an agreement. Kwa sababu jambo kama hilo ni kinyume na Katiba, period.

Unazungumza kana kwamba this is an established fact. Kama kuna mkataba wa aina hiyo kati ya serikali na Kanisa lolote inabidi kesi ya Kikatiba ifunguliwe kwani ina vunja "non-discrimination clause" ya Katiba yetu, haijalishi ina lengo zuri kiasi gani. Na kwa vile kuna wasomi wengi tu wa Kiislamu na maprofesa wa sheria nina uhakika taasisi za Kiislamu na za dini nyingine zinaweza kufungua kesi ya Kikatiba kwanini serikali iingie mkataba wa aina hiyo.

Kwani tumeambiwa waliosaini au watakaosaini hizo "bilateral negotiations" siyo wataalamu wa mambo hayo? Hiyo inference umeipata wapi kwenye huo "mkataba"?

Interesting...mbona yapo mengine mengi tuu ambayo ni kinyume na katiba?

mfano Anti terrorism Act ya 2002 ni Kinyume na katiba au kama huna then waweza soma "Bill supplement No.11" ambayo pia ilinakiliwa na Gazette of the United Republic of Tanzania.2002. 83.40 pp1-39
 
Kama hamtuwekei full MoU, mjadara ufungwe maana inawezekana tunajadiri kitu kisichokuwepo. Isije kuwa ni janja ya watu kututoa katika mijadara mizito ya Cheyo na Spika, Selelii na Spika, Zitto na Spika nk.

kazi kweli kweli...
 
Kwa ufahamu wangu sirikali ya Tanzania haina dini, kwa hivyo suala la kusaini MOU with any religion is incorrect. Kama ikiwezekana waweke kinaga ubaga kwamba dini zote zitapata misaada based on the MOU signed with Muslims or Chrisitians - this is my thought

Kusema serikali haina dini maana yake ni kwamba serikali si ya dini fulani - ya Kikristo, Kiislamu, nk. Ku'sign MoU' ni dhehebu fulani la dini (ya Kiislamu au Kikristo) ndani ya nchi na linalosaidia huduma za afya, elimu, miundo mbinu na harakati za kupiga vita maradhi (kama ukimwi) na umaskini hakuna maana kuwa serikali sasa ni ya dini fulani.

Kama kuna udini wowote ni hao wanaodai mambo yao yawekwe kwenye Katiba ya nchi. Huo ndio udini hasa!
 
makubwa tena haya. Ingekuwa waislamu wamefanya hivi ingekuwa NONGWA.

Kwani Waislam kuanza kutoa taaluma kuhusu uchaguzi kila mtu anapiga kelele japo malengo ake ni sawa na a kanisa
 
Interesting...mbona yapo mengine mengi tuu ambayo ni kinyume na katiba?

mfano Anti terrorism Act ya 2002 ni Kinyume na katiba au kama huna then waweza soma "Bill supplement No.11" ambayo pia ilinakiliwa na Gazette of the United Republic of Tanzania.2002. 83.40 pp1-39

Ni kinyume na Katiba vipi?
 
makubwa tena haya. Ingekuwa waislamu wamefanya hivi ingekuwa NONGWA.

Kwani Waislam kuanza kutoa taaluma kuhusu uchaguzi kila mtu anapiga kelele japo malengo ake ni sawa na a kanisa

Na tena kama Wakristo ndiyo wangetaka mahakama zao ziwe kwenye katiba na serikali kushinikiza serikali ijiunge na mashirika ya Kikristo ingekuwa nongwa zaidi! Mbona Kanisa halijapiga kelele Waislamu kuanzisha shule au hospitali?
 
Mimi hii parallel inayokuwa drawn kati ya Vatican na OIC huwa inanishangaza sana. Bahati mbaya sana hata watu ambao mi nawaheshimu wanairudia rudia hata baada ya kutolewa maelezo mengi. Sijui ni nini hii? Ila nadhani hii inafanya credibility ya madai mengi ya waislam iwekwe kwenye question.

Hata kama Vatican ni institution, serikali ya Tanzania haijaridhia na haijashiriki kwa namna yoyote kutunga katiba ya Vatican. Serikali ya Tanzania in uhusiano na Vatican wa kibalozi kwa sababu Vatican wana Balozi wao Tanzania. Tanzania haijawahi kupeleka Balozi Vatican.

Serikali ya Tanzania si mwanachama wa hiyo Taasisi inayoitwa Vatican hata kama ni taasisi si nchi. Hata Vatican haichukui uanachama wa nchi kama nchi.

Sasa hii parallel inayokuwa drawn kati ya Vatican na OIC na kina Mkandara iko wapi? Please kama we have a cause to defend let's do it by using hard facts and evidence. Hii kuleta vidocument visivyo na kichwa wala miguu na kuviita memorundum of understanding kati ya serikali na kanisa haisaidii. Only inasaidia kushusha credibility ya madai tunayoya-advance.
 
makubwa tena haya. Ingekuwa waislamu wamefanya hivi ingekuwa NONGWA.

Kwani Waislam kuanza kutoa taaluma kuhusu uchaguzi kila mtu anapiga kelele japo malengo ake ni sawa na a kanisa
Kutoa elimu ya uraia na uchaguzi dini zote zinaruhusiwa,ila kinacho gomba ni pale taasisi ya kidini inapotumika kumpigia kampeni mtu wa dini isiyo yao. hapa wakristo hawajasema asichaguliwe muislama au pagani, bali uzuri au faida za kumchagua kiongozi aliye bora awe muislamu/pagana au mkristo etc awe wa ccm au wa vyama vingine, sasa hofu ni ya nini? au huyu aliyepo hafai hivyo wafuasi wake wanahisi anafuatwa kwa kuwa ni Mkristo/muislamu? kama aliyepo ni kiongozi bora basi wafuasi wake au mashabiki wake hawana haja ya kuwashwa washwa maana atapita tu kwa sifa zake, lakini kama si hivyo tutayaona ya Mabuto ambaye hakuwa muislamu bali hakuwa kiongozi Bora.
 
Mkandara. Huu unaoitwa mkataba ni forgery. Hii haihusiani na kuwepo au kutokuwepo kwa makabuliano kya kushirikiana kati ya serikali katika nyanja mbalimbali. Mbona serikali ina shirikiana na Bakwata (institution ya waislamu), na Hindu Mandal (hospitali ya wahindu), Aga Khan ( taasisi ya kiislamu ), Chuo Kikuu cha Tumaini ( taasisi ya wamisheni), hospitali ya KCMC (taasisi ya wamisheni) n.k.? Ninachopinga ni kutuwekea kitu ambacho ni blatantly forgery kwa nia ya uchonganishi. Tukiangalia tena mada iliyo mbele yetu:

1) mwandishi anadai katika hiyo MoU kuna makubaliano ya kupewa upendeleo wa AJIRA kwa wakristu katika vyuo vya walimu vya serikali! CCT na TEC wataanzaje kuwaombea nafasi za KAZI (sio elimu) kwa watu wao (ambao ni sehemu kubwa ya wamisheni wote ) katika taasisi za serikali yao! Hao ambao mwandishi anadai ni watu wa CCT na TEC si raia wa nchi hii na wana kila haki ya kupata ajira huko? Au mwandishi anataka kutuambia kuwa CCT na TEC wameona kuna vizuizi kwa wamisheni kuajiriwa hadi waombe upendeleo maalum? Hivi kweli kuna upungufu wa wamisheni katika vyuo vya ualimu nchini?

2) CCT haina watu wake. Hiki ni chombo kinachounganisha baadhi ya madhehebu ya wamisheni. Hayo madhehebu ndiyo yana watu (tukichukulia kuwa hii ina maana ya wafuasi wake). Kwa hali hiyo upendeleo huo utakuwa vigumu kuutekeleza maana kila dhehebu litataka watu wake ndio wapate upendeleo! Au mwandishi anataka kutuambia kuwa upendeleo huo wa ajira utakuwa kwa wafanyakazi wa CCT? Hauoni ni upuuzi kwa CCT waombe ajira kwa waajiriwa wao! Ili iwaje?

3) Tunaposema serikali katika upuuzi huu tuna maanisha nani? Mnataka kutuambia Rais wa nchi ndiye amesaini mkataba huu? Au Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha? Au waziri wa Fedha? Au Hawa Ghasia? Nani basi ndiye ataiwakilisha serikali katika utekelezaji wa MoU?

Aliyeuweka huu unaodaiwa kuwa ni MoU ni Agent Provocateur. Na wengine wenu kwa vile kila wakati wanapenda kuona kuwa wameonewa wameingia mkenge! Mbaya zaidi hamkawii ( hasa wewe Mkandara) kuja na lugha ya vitisho. Kwani ni waislamu peke yao walioonewa na serikali yetu? Mbona wamisheni na wahindu hawakulalamika wakati rasilmali zao zilipopokonywa na serikali? Si walijua nia na makusudi ilikuwa kutoa nafasi kwa raia wote wa nchi hii kufaidika na rasilmali hizo. Ndivyo inavyotakiwa.

Kama nilivyosema awali. Tuoneeni huruma raia wa nchi yetu.

Amandla........
The fact kwamba mmekasirika na kutetea mkataba kwa nguvu zote inaonyesha jinsi mlivyo.....biased (one sided thinkers)
Mkataba wa aina hii ni Upendeleo and injust
hakuna service ya kanisa inayotolewa bure "kila mtu analipia shule na hospital big junk of money to have servie" name any church school linganisha bei yake na shule za serikali
kama wana pata pesa toka serikalini then watoe huduma kwa bei poa! otherwsie ni mafisadi kwa jina la kanisa...
 
Back
Top Bottom