Moshi: Mkandarasi atoa wiki 1 kwa Serikali kumlipa fedha zake zaidi ya Bilioni 1

Ukubwa wake ni upi!? Gharama ya kujenga mita moja ya mraba ni kati ya sh. 500k na milioni moja na nusu.
Fanya nusu ya gharama zote ni jengo.. na nusu ni miundombinu. Bado huwezi sema jengo hilo lina mita za mraba 9500. Ambazo ni karibia viwanja viwili vya mpira wa miguu.

Tufanye wewe hapo jikoni/stoo tumekubali jengo lina sq 9500 ili mlifanyie nn Moshi!? Mumpangishe nani!? Na kwa sh. Ngapi ili kurudisha 28bn!?

Unavuta bangi?
 
Anataka kugusa nyeti ya simba huyo!! Eti anaipa serikali wiki??
Yuko sahihi, nimemuona ITV, ndiyo utaratibu ilivyo amefanya kazi asilimia fulani ukaguzi umefanyika na Certificate ya malipo imesainiwa since November, 2020... Wafanyakazi 100 our of 150 wameshaacha kazi kwa kutolipwa. Sasa hapo ulileta ubabe haisaidii ni kulipa tuu...

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Nirudie nini ??, we ndo rudia , unakrupuka tuu, stend Gharama ni bil 28 , mkandarasi anadai bil 1....matokeo ya shule za kata tabu sana
Shule za Kata sasa zinaongoza kufaulisha vizuri sana
 
Mkuu kama hujui utaratibu wa malipo kwa hizi kazi za ukandarasi ni bora kuuliza kuliko kuja hivi, ulivyokuja!!kazi za ukandarasi , hulipwa kulingana na certificates, unaamaliza kazi fulani, una issue certificate, wanakuja kukagua unalipwa kwa kazi hiyo kwanza, ndipo unaendelea!!sasa ka awamu hii mkandarasi ana issue certificate kibao, halipwi, ana kuja kiongozi wa kisiasa anaanza kubwabwaja, kuwa kazi imekushinda, nitafanyaje kazi bila kulipwa pesa??huyu amethubutu kujitoa muhanga kwani kwa mazingira ya sasa ni ngumu kujitokeza nankusema hayo!!lakini ndio hali inayowakumba wakandarasi wote nchini!!na huyu usije shangaa akavunjiwa mkataba kuwa sio MZALENDO!!!Anatumika na mabeberu na asipewe kazi tena nchini!!!
Unajua mkuu, Kuna watu ujuaji mwingi alafu hamna kitu.
Bora umewafafanulia vizuri wasipoelewa usiumize kichwa, unafikiri malipo ya kazi za serikali kama unaenda kwa mangi kununua mchele
 
Mkandarasi .......yes!
Nilikuwa nakusumbiri Mkanda!!!
Ukubwa wake ni upi!? Gharama ya kujenga mita moja ya mraba ni kati ya sh. 500k na milioni moja na nusu.
Fanya nusu ya gharama zote ni jengo.. na nusu ni miundombinu. Bado huwezi sema jengo hilo lina mita za mraba 9500. Ambazo ni karibia viwanja viwili vya mpira wa miguu.

Tufanye wewe hapo jikoni/stoo tumekubali jengo lina sq 9500 ili mlifanyie nn Moshi!? Mumpangishe nani!? Na kwa sh. Ngapi ili kurudisha 28bn!?
Zile bei za mabibo hostel bado zinaendelea? Maana kwa kamba hamjambo bei mnapanga mtakavyo na malipo mnafuata sheria na zaidi
 
Mkandarasi anayejenga stendi kubwa ya mabasi ya kimataifa ya Ngangamfumini, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro yenye thamani ya bilioni 28, ametoa wiki moja kwa serikali imlipe fedha zake ambazo ni zaidi ya bilioni 1 anazodai kabla hajasimama kuendelea na ujenzi wa stendi hiyo.

Charles Shimilwa, Msimamizi wa ujenzi wa stendi hiyo kutoka kampuni ya CRJE East Africa.

Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka kampuni ya CRJE East Africa, Charles Shimilwa, amesema kuwa mpaka sasa kampuni hiyo imeshindwa kuendelea na ujenzi kutokana na madeni wanayoidai serikali kwa kipindi kirefu hali iliyosababisha kupoteza ajira zaidi ya 100.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya fedha na utawala ambaye pia ni mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu, amesema endapo mkandarasi huyo atasimamisha ujenzi wa jengo hilo serikali italazimika kumlipa fidia kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi huo na kuiomba serikali kulipa fedha hizo ili kukamilisha kwa wakati ujenzi wa stendi hiyo.

Naye Diwani wa kata ya Ngangamfuni inapojengwa stendi hiyo, Stuart Nathanael, amesema endapo mradi wa stendi hiyo utasimama utaathiri shughuli za uchumi katika kata hiyo na manispaa kukosa mapato na kuiomba serikali kuangalia uwezekano wa kulipa fedha hizo kwa haraka.

EATV
Serikali hii hailipi madeni ya wakandarasi ndio maana inaamua kutumia taasisi za za uma kwenye miradi karibu yote kwani haziruhusiwi kulalamika. Mimi naishi serikali ya Magufuli kwa zaidi ya miaka 6 na nimeiahakata tamaa ya kupata haki yangu
 
Nilikuwa nakusumbiri Mkanda!!!

Zile bei za mabibo hostel bado zinaendelea? Maana kwa kamba hamjambo bei mnapanga mtakavyo na malipo mnafuata sheria na zaidi
Hizi ni public investments kama hazina faida ..ziwekwe kwenye uhujumu uchumi.. uchukue bilioni 28 kwa mji usiogenerate trips.. 50 percentage ya wasafiri wake ni wa kupita.. kwenda au kutoka Arusha..

Na hapo hapo inajenga mjengo mkubwa ili upangishe wakati kuna majengo mjini kati hayana wapangaji!?
 
Unaona Nani kakosa heshima hapo
I don't care about you distorted mind.. nikukosee heshima kwa kuhighlight mapungufu ya fikra wakati wa kujenga wazo!?

Mjini moshi kuna majengo yako tupu.. hayana wapangaji. Huko stand mpya unakwenda kuwatoa wapangaji wapi!? Au washona viatu unatarajia wataingia walipe kodi ya pango!?

Na trip generation moshi iko wapi!? Mabasi yote yanaondoka asubuhi na kurudi usiku.. asilimia hamsini na zaidi na watu wanapita tu kwenye DOm Arusha Tanga na DSM... Halafu unaweka bilioni 28!? Uzirudisheje!? Kama sio ufahari tuu
 
Mkandarasi anayejenga stendi kubwa ya mabasi ya kimataifa ya Ngangamfumini, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro yenye thamani ya bilioni 28, ametoa wiki moja kwa serikali imlipe fedha zake ambazo ni zaidi ya bilioni 1 anazodai kabla hajasimama kuendelea na ujenzi wa stendi hiyo.

Charles Shimilwa, Msimamizi wa ujenzi wa stendi hiyo kutoka kampuni ya CRJE East Africa.

Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka kampuni ya CRJE East Africa, Charles Shimilwa, amesema kuwa mpaka sasa kampuni hiyo imeshindwa kuendelea na ujenzi kutokana na madeni wanayoidai serikali kwa kipindi kirefu hali iliyosababisha kupoteza ajira zaidi ya 100.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya fedha na utawala ambaye pia ni mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu, amesema endapo mkandarasi huyo atasimamisha ujenzi wa jengo hilo serikali italazimika kumlipa fidia kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi huo na kuiomba serikali kulipa fedha hizo ili kukamilisha kwa wakati ujenzi wa stendi hiyo.

Naye Diwani wa kata ya Ngangamfuni inapojengwa stendi hiyo, Stuart Nathanael, amesema endapo mradi wa stendi hiyo utasimama utaathiri shughuli za uchumi katika kata hiyo na manispaa kukosa mapato na kuiomba serikali kuangalia uwezekano wa kulipa fedha hizo kwa haraka.

EATV
Ajaribu aone. Atafugiwa kufanya kazi hapa mpaka alipe fidia
 
Back
Top Bottom