Moshi: Mkandarasi atoa wiki 1 kwa Serikali kumlipa fedha zake zaidi ya Bilioni 1

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,523
2,000
Mkandarasi anayejenga stendi kubwa ya mabasi ya kimataifa ya Ngangamfumini, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro yenye thamani ya bilioni 28, ametoa wiki moja kwa serikali imlipe fedha zake ambazo ni zaidi ya bilioni 1 anazodai kabla hajasimama kuendelea na ujenzi wa stendi hiyo.

Charles Shimilwa, Msimamizi wa ujenzi wa stendi hiyo kutoka kampuni ya CRJE East Africa.

Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka kampuni ya CRJE East Africa, Charles Shimilwa, amesema kuwa mpaka sasa kampuni hiyo imeshindwa kuendelea na ujenzi kutokana na madeni wanayoidai serikali kwa kipindi kirefu hali iliyosababisha kupoteza ajira zaidi ya 100.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya fedha na utawala ambaye pia ni mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu, amesema endapo mkandarasi huyo atasimamisha ujenzi wa jengo hilo serikali italazimika kumlipa fidia kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi huo na kuiomba serikali kulipa fedha hizo ili kukamilisha kwa wakati ujenzi wa stendi hiyo.

Naye Diwani wa kata ya Ngangamfuni inapojengwa stendi hiyo, Stuart Nathanael, amesema endapo mradi wa stendi hiyo utasimama utaathiri shughuli za uchumi katika kata hiyo na manispaa kukosa mapato na kuiomba serikali kuangalia uwezekano wa kulipa fedha hizo kwa haraka.

EATV
 

Bombabomba

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
1,246
2,000
Kuna Jamaa aliwahi kusema Serikali/Halmashauri ni artificial person ambaye hakuna anayemuona lkn kila mmoja anamheshimu na kumuogopa. Hawa Viongozi kuwekwa pale juu kuisemea tu! Yaani hata Rais akitendewa sivyo Ndivyo ataishikati Serikali au kushitakiwa na Serikali.
Mkataba na sheria havina cha serikali.Na serikali sio jiwe, jiwe ni mpitaji serikali ipo milele
 

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,177
2,000
STANDI YA BILIONI 28 MOSHI???? TAKUKURU WAMULIKE HUO MRADI LAZIMA UNA UFISADI MKUBWA SANAAAA! MIMI KAMA MWANA MOSHI SIKUBALIANI NA HILO.

WEKENI HUMU MICHORO NA DESIGN KAMA MLIVYOFANYA KWA DAR ILI TUJADILI VIZURI! DUUUU!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom