Serikali Kuongeza Bilioni 4 Kukamilisha Upanuzi wa Njia 4 Bukoba Mjini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

SERIKALI KUONGEZA BILIONI 4 KUKAMILISHA UPANUZI WA NJIA NNE BUKOBA MJINI

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa tayari Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kuongeza kiasi cha Shilingi Bilioni 4 kukamilisha upanuzi wa barabara ya njia nne Bukoba Mjini (Rwamishenye Round about - Stendi ya Bukoba Mjini) yenye urefu kilometa 1.6.

Bashungwa amesema hayo leo tarehe 28 Machi 2024 wakati alipowasili katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuanza ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya barabara Mkoani humo.

Bashungwa amesema kuwa awali Serikali ilitoa kiasi cha shilingi Bilioni 4.64 kuanza ujenzi wa wa barabara hiyo kwa kipande cha kilometa 1 ambacho kinaanzia Rwamishenye hadi eneo la Mitaga ambapo kwa sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 25.

Amesema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 4 kitakachoongezwa kitawezesha ujenzi wa kipande cha mita 600 kuanzia eneo la Mitaga hadi stendi na ujenzi wa daraja kubwa katika mto Kanoni.

“Mheshimiwa Rais ameshatoa kibali kwa TANROADS kuendeleza ujenzi wa barabara ya njia nne hadi stendi ya Bukoba ambapo Mkandarasi M/s Abemulo ambaye ameshaanza kazi kwa kipande cha km 1 ataendelea na ujenzi kwa kipande cha mita 600 na daraja kubwa”, amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Kagera kumsimamia Mkandarasi anayeendelea na ukarabarati wa barabara ya Lusahunga - Rusumo (km 92) kwa kiwango cha lami ambapo barabara hiyo inauunganisha Mkoa wa Kagera na nchi jirani.

Naye, Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini, Stephen Byabato amesema kazi ya ujenzi wa njia nne wa barabara ya Bukoba Mjini unaendelea kwa kasi kubwa na ameiomba Serikali kushughulikia suala la fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa barabara hiyo.
 

Attachments

  • SERIKALI KUONGEZA BILIONI 4 KUKAMILISHA UJENZI WA NJIA NNE BUKOBA MJINI .MP4
    70.9 MB
  • WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.30.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.30.jpeg
    180.2 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.31.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.31.jpeg
    346.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.31(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.31(1).jpeg
    431.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.32.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.32.jpeg
    632.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.33.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.33.jpeg
    345.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.33(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.33(1).jpeg
    418.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.34.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.34.jpeg
    541.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.34(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.34(1).jpeg
    646.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.35.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.35.jpeg
    657.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.36.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-28 at 12.46.36.jpeg
    528.5 KB · Views: 3
Tatizo la wahaya ni upigaji ndio maana hapo Bukoba mjini papo kama 1980s,

hizo pesa zilindwe sana lasivyo zitapigwa utaanza sikia wanajisifu milioni 10 ni pesa ya mbogha
 
Back
Top Bottom