Moshi: Mkandarasi atoa wiki 1 kwa Serikali kumlipa fedha zake zaidi ya Bilioni 1

STANDI YA BILIONI 28 MOSHI???? TAKUKURU WAMULIKE HUO MRADI LAZIMA UNA UFISADI MKUBWA SANAAAA! MIMI KAMA MWANA MOSHI SIKUBALIANI NA HILO.

WEKENI HUMU MICHORO NA DESIGN KAMA MLIVYOFANYA KWA DAR ILI TUJADILI VIZURI! DUUUU!
Usijifanye mjuaji sana,hata huyo mungu wako Jiwe alishapita hapo na akakubaliana na hiyo budget.
 
I don't care about you distorted mind.. nikukosee heshima kwa kuhighlight mapungufu ya fikra wakati wa kujenga wazo!?

Mjini moshi kuna majengo yako tupu.. hayana wapangaji. Huko stand mpya unakwenda kuwatoa wapangaji wapi!? Au washona viatu unatarajia wataingia walipe kodi ya pango!?

Na trip generation moshi iko wapi!? Mabasi yote yanaondoka asubuhi na kurudi usiku.. asilimia hamsini na zaidi na watu wanapita tu kwenye DOm Arusha Tanga na DSM... Halafu unaweka bilioni 28!? Uzirudisheje!? Kama sio ufahari tuu
Moshi jengo gani halina watu?
Stend kusiwe na biashara Moshi?
Unaijua Moshi mjini vizuri?
Kuanzia dar Street,majengo na mitaa yake,njoro na mitaa yake,kcmc na mitaa yake, rau na mitaa yake , ngangamfumuni na mitaa yake,ushirika,Kiboriloni,shant town,ccp,Soweto, mbuyuni,
 
Moshi jengo gani halina watu?
Stend kusiwe na biashara Moshi?
Unaijua Moshi mjini vizuri?
Kuanzia dar Street,majengo na mitaa yake,njoro na mitaa yake,kcmc na mitaa yake, rau na mitaa yake , ngangamfumuni na mitaa yake,ushirika,Kiboriloni,shant town,ccp,Soweto, mbuyuni,
Uchumi house

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Unajua mkuu, Kuna watu ujuaji mwingi alafu hamna kitu.
Bora umewafafanulia vizuri wasipoelewa usiumize kichwa, unafikiri malipo ya kazi za serikali kama unaenda kwa mangi kununua mchele
Yaani kuna watu,ni wa ajabu sana!!kila sehemu analeta ushabiki wa yanga na simba, bila hata kujua utaratibu uliopo wa jambo husika!!
 
Mkandarasi anayejenga stendi kubwa ya mabasi ya kimataifa ya Ngangamfumini, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro yenye thamani ya bilioni 28, ametoa wiki moja kwa serikali imlipe fedha zake ambazo ni zaidi ya bilioni 1 anazodai kabla hajasimama kuendelea na ujenzi wa stendi hiyo.

Charles Shimilwa, Msimamizi wa ujenzi wa stendi hiyo kutoka kampuni ya CRJE East Africa.

Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka kampuni ya CRJE East Africa, Charles Shimilwa, amesema kuwa mpaka sasa kampuni hiyo imeshindwa kuendelea na ujenzi kutokana na madeni wanayoidai serikali kwa kipindi kirefu hali iliyosababisha kupoteza ajira zaidi ya 100.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya fedha na utawala ambaye pia ni mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu, amesema endapo mkandarasi huyo atasimamisha ujenzi wa jengo hilo serikali italazimika kumlipa fidia kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi huo na kuiomba serikali kulipa fedha hizo ili kukamilisha kwa wakati ujenzi wa stendi hiyo.

Naye Diwani wa kata ya Ngangamfuni inapojengwa stendi hiyo, Stuart Nathanael, amesema endapo mradi wa stendi hiyo utasimama utaathiri shughuli za uchumi katika kata hiyo na manispaa kukosa mapato na kuiomba serikali kuangalia uwezekano wa kulipa fedha hizo kwa haraka.

EATV

Asicheze na JIWE atamfanyia kitu mbaya ,amuulize MANJI.
 
Nirudie nini ??, we ndo rudia , unakrupuka tuu, stend Gharama ni bil 28 , mkandarasi anadai bil 1....matokeo ya shule za kata tabu sana
Amekueleza vizuri kuwa urudie kusoma, hujaelewa.

Gharama ya mradi 28 billion. Hawajasema amelipwa 27 bilioni. Mradi huwa una phases, na kila phase ina malipo yake. Anaposema anadai bilioni 1 ina maana ni malipo ya phase aliyokamilisha. Na haijulikani kuna phases ngapi, na amekamilisha phase ya ngapi.

Hiyo 28 bilioni ni thamani ya mradi mzima, na inawezekana kuna subcontractors.
 
Mkuu kama hujui utaratibu wa malipo kwa hizi kazi za ukandarasi ni bora kuuliza kuliko kuja hivi, ulivyokuja!!kazi za ukandarasi , hulipwa kulingana na certificates, unaamaliza kazi fulani, una issue certificate, wanakuja kukagua unalipwa kwa kazi hiyo kwanza, ndipo unaendelea!!sasa ka awamu hii mkandarasi ana issue certificate kibao, halipwi, ana kuja kiongozi wa kisiasa anaanza kubwabwaja, kuwa kazi imekushinda, nitafanyaje kazi bila kulipwa pesa??huyu amethubutu kujitoa muhanga kwani kwa mazingira ya sasa ni ngumu kujitokeza nankusema hayo!!lakini ndio hali inayowakumba wakandarasi wote nchini!!na huyu usije shangaa akavunjiwa mkataba kuwa sio MZALENDO!!!Anatumika na mabeberu na asipewe kazi tena nchini!!!
Mkandarasi mwenyewe ni beberu wa kikomunisti ambaye ndio alijenga na kuwekeza kwenye miradi mikubwa nazani hata reli ya tazara alijenga yeye pia kwaio sio wa mchezo mchezo mjini amejenga majengo mengi na hoteli visiwani
 
Ndiyo, si anadai chake?? Sasa anajenga kwa pesa ipi km ela hapewi??

Serikali iache uhuni na imlipe, mbona hawazembei kt kukusanya kodi
Anataka kugusa nyeti ya simba huyo!! Eti anaipa serikali wiki??
 
Back
Top Bottom