Moshi: Mkandarasi atoa wiki 1 kwa Serikali kumlipa fedha zake zaidi ya Bilioni 1

Mkandarasi anayejenga stendi kubwa ya mabasi ya kimataifa ya Ngangamfumini, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro yenye thamani ya bilioni 28, ametoa wiki moja kwa serikali imlipe fedha zake ambazo ni zaidi ya bilioni 1 anazodai kabla hajasimama kuendelea na ujenzi wa stendi hiyo.

Charles Shimilwa, Msimamizi wa ujenzi wa stendi hiyo kutoka kampuni ya CRJE East Africa,

Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka kampuni ya CRJE East Africa, Charles Shimilwa, amesema kuwa mpaka sasa kampuni hiyo imeshindwa kuendelea na ujenzi kutokana na madeni wanayoidai serikali kwa kipindi kirefu hali iliyosababisha kupoteza ajira zaidi ya 100.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya fedha na utawala ambaye pia ni mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu, amesema endapo mkandarasi huyo atasimamisha ujenzi wa jengo hilo serikali italazimika kumlipa fidia kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi huo na kuiomba serikali kulipa fedha hizo ili kukamilisha kwa wakati ujenzi wa stendi hiyo.

Naye Diwani wa kata ya Ngangamfuni inapojengwa stendi hiyo, Stuart Nathanael, amesema endapo mradi wa stendi hiyo utasimama utaathiri shughuli za uchumi katika kata hiyo na manispaa kukosa mapato na kuiomba serikali kuangalia uwezekano wa kulipa fedha hizo kwa haraka.

EATV
Mkandarasi .......yes!
 
Pesa Zipo Haa 😂😁😀😄😃🤣😂😀😀
Serikali Ninayoiongoza Hakuna Michakato
 
Na yeye anatekeleza mktataba maana kila siku tunasikia serikali inasema mkandarasi akichelewesha mradi anakatwa hela. Sasa it is their turn.
 
Kuna kipindi nilikuwa na mkandarasi mmoja akawa analalamika malipo kuchelewa sana. Akawa anasema shida ni kwamba ukilalamika sana, wanaku-blacklist, unakuwa hupati kazi tena za serikali. Na wakati mwingine unapewa kazi ya pili wakati ya kwanza hujalipwa, lalamika unapigwa "lock" ya tender. Ni dhuluma tupu
 
Ulitegemea mradi mkubwa namna ile ugarimu kiasi gani
Ukubwa wake ni upi!? Gharama ya kujenga mita moja ya mraba ni kati ya sh. 500k na milioni moja na nusu.
Fanya nusu ya gharama zote ni jengo.. na nusu ni miundombinu. Bado huwezi sema jengo hilo lina mita za mraba 9500. Ambazo ni karibia viwanja viwili vya mpira wa miguu.

Tufanye wewe hapo jikoni/stoo tumekubali jengo lina sq 9500 ili mlifanyie nn Moshi!? Mumpangishe nani!? Na kwa sh. Ngapi ili kurudisha 28bn!?
 
Back
Top Bottom