Mnaowalea watoto wa kike bila kuwafundisha kazi za nyumbani mnawaandalia mazingira gani wakiwa wakubwa?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Ni siku ya leo nimekumbuka nikiwa kwenye mahusiano hapo miaka ya 2015 na binti moja mrembo, mapenzi yalinoga sana lakini baada yakuanza kuishi nae niliona mapungufu mengi sana, la kwanza kabisa alikuwa hajui kupika yani ugali sometimes unakuwa mbichi halafu hata hajishughulishi kuongeza mboga za pembeni wakati vitu vipo vya kutosha stoo, mambo ya kunishuguhulikia usafi wangu mwanaume wake kama kunifulia nguo nayo ni mpaka iwe vuta nikuvute tena jeans anafulia brush!!, Kwakweli taa nyekundu iliwaka kichwani suala la ndoa likafutika kabisa.

Kumuandaa mtoto wako wa kike kujua kuishi kwenye ndoa za kiafrika ni jukumu ambalo wazazi hasa mama hapaswi kulilazia damu,

Kuna wazazi tunawaona kwamba wakiwa na vijipesa basi wanamleta house girl amsaidie mtoto wa kike kazi ambazo inabidi azifanye yeye ili ziwe mazoea ya kumjengea uzoefu ya msingi ya kuwa mke anaeweza kuishi ndani ya ndoa za kiafrika.

Tutofautishe vitu viwili, kuna kufanya kitu kwa kuweza baada ya kujifunza na kufanya kitu kwa mazoea, unaweza ukajifunza leo hii kupika hata kupitia youtube ama google, hapa mfano suala la kupika tupo wanaume wengi sana kwenye yale maisha ya ubachela, kupika tunajua ila inakuwa sio kitu tulichozoea, tunachukulia kupika kama mzigo unaojitaji msaidizi mzoefu. upande wa pili ni kujifunza na kuzoeshwa kwa muda mrefu hasa tangu mtoto, hapa ndipo pa mabinti ambao wakizoeshwa kupika chakula pamoja na kuyazoea mazingira ya jikoni basi huwa wamepata uzoefu mwingi sana na tayari imeshakua ni mazoea, suala la kupika kwao huwa wana enjoy, kupika automatically wanajua ni jukumu lao.

Sasa tukija kwa watoto hawa wanaolelewa kitamthilia inakuwa ngumu sana mwanaume wa kiafrika kumuoa maana sisi wanaume wa kiafrika suala la kwanza kwenye kuoa huwa "tunavuta jiko" hivyo vingine huwa ni vya ziada tu vikiwemo elimu, uzuri, n.k Jiko ndio kazi kuu ya mwanamke akiwa ndani ikifuatiwa na usafi wa mme wake kuanzia kumfulia nguo zake mpaka soksi, na majukumu mengine kama usafi wa nyumba, n.k.

Unakuta binti wazazi wake hawakumfundisha wala kumzoesha shughuli za kupika, matokeo yake huku kwenye ndoa anazidisha chumvi, wali boko, ugali mbichi, n.k. vinaanza kuwa kero, na hata kama anajua kupika anakuwa hana mazoea, anapika kwa kujivuta vuta sana, badala ya kujiongeza asubuhi amuandalie mme wake hata viazi vya kuchemsha yeye anaweka mkate tu, siku ya jumapili mmepumzika myumbani yeye wala hajishughulishi kubadili ratiba, yeye anasonga ugali na mchicha wakati stoo kuna mchele wa kutosha, friji kuna nyama ya kutosha, stoo zipo nazi za kumwaga, n.k. Mwanaume anaanza kumuona mzigo tu.

Kufua nguo za mmewe wala hana muda anampa huse girl sababu huko kwao nae alikuwa anafuliwa ama hakuzoeshwa ama anaangalia sana tamthilia za wazungu, ni mambo yanayotia aibu maana huu sio uafrika wetu, haijalishi hata kama mwanamke ana cheo kizito ni lazima amfulie mme wake nguo, hizo ndio mila zetu waafrika tangu na tangu si vinginevyo.
 
Ni siku ya leo nimekumbuka nikiwa kwenye mahusiano hapo miaka ya 2015 na binti moja mrembo, mapenzi yalinoga sana lakini baada yakuanza kuishi nae niliona mapungufu mengi sana, la kwanza kabisa alikuwa hajui kupika yani ugali sometimes unakuwa mbichi halafu hata hajishughulishi kuongeza mboga za pembeni wakati vitu vipo vya kutosha stoo, mambo ya kunishuguhulikia usafi wangu mwanaume wake kama kunifulia nguo nayo ni mpaka iwe vuta nikuvute tena jeans anafulia brush!!, Kwakweli taa nyekundu iliwaka kichwani suala la ndoa likafutika kabisa.

Kumuandaa mtoto wako wa kike kujua kuishi kwenye ndoa za kiafrika ni jukumu ambalo wazazi hasa mama hapaswi kulilazia damu,

Kuna wazazi tunawaona kwamba wakiwa na vijipesa basi wanamleta house girl amsaidie mtoto wa kike kazi ambazo inabidi azifanye yeye ili ziwe mazoea ya kumjengea uzoefu ya msingi ya kuwa mke anaeweza kuishi ndani ya ndoa za kiafrika.

Tutofautishe vitu viwili, kuna kufanya kitu kwa kuweza baada ya kujifunza na kufanya kitu kwa mazoea, unaweza ukajifunza leo hii kupika hata kupitia youtube ama goole lakini itachukua muda mrefu sana kujenga mazoea ya kupika, ila kama umeshazoeshwa tangu mtoto si kwamba tu unaweza lakini umepata uzoefu mwingi sana na tayari imeshakua ni mazoea, unapika bila kuhisi uchovu wala hujivuti, una enjoy kupika inakua sio shughuli bali hobby.

Sasa tukija kwa watoto hawa wanaolelewa kitamthilia inakuwa ngumu sana mwanaume wa kiafrika kumuoa maana sisi wanaume wa kiafrika suala la kwanza kwenye kuoa huwa "tunavuta jiko" hivyo vingine huwa ni vya ziada tu vikiwemo elimu, uzuri, n.k. na ukikosea ukifanya vinginevyo ujipange!! Jiko ndio kazi kuu ya mwanamke akiwa ndani ikifuatiwa na usafi wa mme wake kuanzia kumfulia nguo zake mpaka soksi, na majukumu mengine kama usafi wa nyumba, n.k.

Unakuta binti wazazi wake hawakumfundisha wala kumzoesha shughuli za kupika, matokeo yake huku kwenye ndoa anazidisha chumvi, wali boko, ugali mbichi, n.k. vinaanza kuwa kero, na hata kama anajua kupika anakuwa hana mazoea, anapika kwa kujivuta vuta sana, badala ya kujiongeza asubuhi amuandalie mme wake hata viazi vya kuchemsha yeye anaweka mkate tu, siku ya jumapili mmepumzika myumbani yeye wala hajishughulishi kupika anasonga ugali na mchicha wakati stoo kuna mchele wa kutosha, friji kuna nyama ya kutosha, yani anaona kupika pilau ni kazi nzito sana, Mwanaume anaanza kumuona mzigo tu.

Kufua nguo za mmewe wala hana muda anampa huse girl sababu huko kwao nae alikuwa anafuliwa ama hakuzoeshwa, ni mambo yanayotia aibu maana huu sio uafrika wetu, haijalishi hata kama mwanamke ana cheo kizito ni lazima amfulie mme wake nguo zake hizo ndio mila zetu waafrika tangu na tangu,
Huu uzi una tatizo la gender roles.

Yani, kuweka kazi ya kupika kuwa ni kazi ya watoto wa kike.

Hii ni tabia ya jamii zenye mfumodume.

Inatakiwa watoto wote wajue kazi zote.

Kujua kupika, kuosha vyombo, kufua ni life skills ambazo hata mtoto wa kiume anatakiwa kuzijua, akiwa peke yake aweze kufanya hizo kazi. Na hata akioa, aweze kusaidiana na mkewe. Kuna uzi nimeuona jana, mtu anasema anamsaidia mke wake kwa sababu anaona mke wake anachoka sana. Sasa, utamsaidiaje mkeo kupika ikiwa mwanamme hujui kupika?

Ila, jamii yetu bado iko nyuma, imefanya kupika, kufua, ni kazi ya mwanamke.

Ndiyo maana hata uzi huu una assume automatically kuwa mwanamke/ mtoto wa kike ndiye anatakiwa kujua vitu hivi, mwanamme ni mtu wa kuhudumiwa tu.

Mfumodume. Dunia fulani ya umasikini wa mawazo.

Najua kwa mfumodume wetu, inawezekana wengi hawataelewa somo.
 
Huu uzi una tatizo la gender roles.

Yani, kuweka kazi ya kupika kuwa ni kazi ya watoto wa kike.

Hii ni tabia ya jamii zenye mfumodume.

Inatakiwa watoto wote wajue kazi zote.

Kujua kupika, kuosha vyombo, kufua ni life skills ambazo hata mtoto wa kiume anatakiwa kuzijua, akiwa peke yake aweze kufanya hizo kazi.

Ila, jamii yetu bado iko nyuma, imefanya kupika, kufua, ni kazi ya mwanamke.

Ndiyo maana hata uzi huu una assume automatically kuwa mwanamke ndiye anatakuwa kujua vitu hivi, mwanamme ni mtu wa kuhudumiwa tu.

Mfumodume. Dunia fulani ya umasikini wa mawazo.

Najua kwa mfumodume wetu, inawezekana wengi hawataelewa somo.
Kuna gender roles za kabla ya ndoa na baada ya ndoa.

Wanaume mabachela hupika, hujifulia, hufanya usafi wa jikoni, n.k. lakini mambo haya inabidi yawe majukumu ya mwanamke baada ya ndoa, ndio maana kuna msemo maarufu wa kuoa kufananishwa na "kuvuta jiko".

Hizo ndizo tamaduni zetu sisi waafrika.
 
We teach girls, marriage is most important thing in life, what about boys?

Yaani mvulana asipofundishwa kupika inakubalika, ila Kwa msichana ni nongwa?
Kuna gender roles za kabla ya ndoa na baada ya ndoa.

Wanaume mabachela hupika, hujifulia, hufanya usafi wa jikoni, n.k. lakini mambo haya inabidi yawe majukumu ya mwanamke baada ya ndoa, ndio maana kuna msemo maarufu wa kuoa kufananishwa na "kuvuta jiko".
 
Kuna gender roles za kabla ya ndoa na baada ya ndoa.

Wanaume mabachela hupika, hujifulia, hufanya usafi wa jikoni, n.k. lakini mambo haya inabidi yawe majukumu ya mwanamke baada ya ndoa, ndio maana kuna msemo maarufu wa kuoa kufananishwa na "kuvuta jiko".

Hizo ndizo tamaduni zetu sisi waafrika.
Hapo umeshakubali kwamba kwenye ndoa kuna gender roles na kupika ni kazi ya mwanamke kwenye ndoa.

Huo ndio mfumodume wenyewe.

Ndiyo maana nikasema kwa mfumo huu ni vigumu kunielewa.

Wewe unafuata mfumo wa kizamani, baba anafanya kazi, mama mke wa nyumbani.

Siku hizi wanawake wanasoma. Inawezekana baba na mama wote wanafanya kazi, kazi za nyumbani wakasaidiana pia.

Sasa hapo ukileta mambo ya gender roles kwamba mama ni mpishi wakati mama naye ni mfanyakazi, unaweza kuwa unamuonea huyo mama.

Kwa sababu na yeye anafanya kazi ofisini kama baba na anarudi kachoka. Msingi wa mama kuwa mpishi kwa kiasi kikubwa ulitokana na mama kuwa mama wa nyumbani.

Msingi huu unatoweka kwa kasi katika dunia ambayo mama naye anafanya kazi ofisini.

Ila, naelewa inawezekana hunielewi kwa sababu ya mfumodume uliokithiri huko kwenye jamii zetu.

Kuna uzi nimeuona jana mtu anasema "anamsaidia" mkewe kazi za nyumbani kwa sababu anaona mkewe anachoka sana.

Sasa kama mkeo anafanya kazi ofisini halafu nyumbani anapika, mume hajui kupika, ikitokea kuna haja mke "asaidiwe" ( neno si sahihi, kwa sababu limefanya kazi ya kupika kuwa ya mke) mume atafanyaje hapo?

Bottom line, hizo gender roles ni za ulimwengu uliopita. Watoto wote wanatakiwa kujua kazi zote na kusaidiana, hata wakikua na kuwa ndani ya ndoa.

Ila naelewa ni somo gumu bado kwa jamii zetu.
 
Hapa kaoe mwanamke ambaye toka mnadate kasema wazi atakuwa Mama wa nyumbani, umfungulie biashara ya yeye kujifurahisha tuu (akitaka kufanya kazi)..hudumia familia.
 
Ni siku ya leo nimekumbuka nikiwa kwenye mahusiano hapo miaka ya 2015 na binti moja mrembo, mapenzi yalinoga sana lakini baada yakuanza kuishi nae niliona mapungufu mengi sana, la kwanza kabisa alikuwa hajui kupika yani ugali sometimes unakuwa mbichi halafu hata hajishughulishi kuongeza mboga za pembeni wakati vitu vipo vya kutosha stoo, mambo ya kunishuguhulikia usafi wangu mwanaume wake kama kunifulia nguo nayo ni mpaka iwe vuta nikuvute tena jeans anafulia brush!!, Kwakweli taa nyekundu iliwaka kichwani suala la ndoa likafutika kabisa.

Kumuandaa mtoto wako wa kike kujua kuishi kwenye ndoa za kiafrika ni jukumu ambalo wazazi hasa mama hapaswi kulilazia damu,

Kuna wazazi tunawaona kwamba wakiwa na vijipesa basi wanamleta house girl amsaidie mtoto wa kike kazi ambazo inabidi azifanye yeye ili ziwe mazoea ya kumjengea uzoefu ya msingi ya kuwa mke anaeweza kuishi ndani ya ndoa za kiafrika.

Tutofautishe vitu viwili, kuna kufanya kitu kwa kuweza baada ya kujifunza na kufanya kitu kwa mazoea, unaweza ukajifunza leo hii kupika hata kupitia youtube ama goole lakini itachukua muda mrefu sana kujenga mazoea ya kupika, ila kama umeshazoeshwa tangu mtoto si kwamba tu unaweza lakini umepata uzoefu mwingi sana na tayari imeshakua ni mazoea, unapika bila kuhisi uchovu wala hujivuti, una enjoy kupika inakua sio shughuli bali hobby.

Sasa tukija kwa watoto hawa wanaolelewa kitamthilia inakuwa ngumu sana mwanaume wa kiafrika kumuoa maana sisi wanaume wa kiafrika suala la kwanza kwenye kuoa huwa "tunavuta jiko" hivyo vingine huwa ni vya ziada tu vikiwemo elimu, uzuri, n.k. na ukikosea ukifanya vinginevyo ujipange!! Jiko ndio kazi kuu ya mwanamke akiwa ndani ikifuatiwa na usafi wa mme wake kuanzia kumfulia nguo zake mpaka soksi, na majukumu mengine kama usafi wa nyumba, n.k.

Unakuta binti wazazi wake hawakumfundisha wala kumzoesha shughuli za kupika, matokeo yake huku kwenye ndoa anazidisha chumvi, wali boko, ugali mbichi, n.k. vinaanza kuwa kero, na hata kama anajua kupika anakuwa hana mazoea, anapika kwa kujivuta vuta sana, badala ya kujiongeza asubuhi amuandalie mme wake hata viazi vya kuchemsha yeye anaweka mkate tu, siku ya jumapili mmepumzika myumbani yeye wala hajishughulishi kupika anasonga ugali na mchicha wakati stoo kuna mchele wa kutosha, friji kuna nyama ya kutosha, yani anaona kupika pilau ni kazi nzito sana, Mwanaume anaanza kumuona mzigo tu.

Kufua nguo za mmewe wala hana muda anampa huse girl sababu huko kwao nae alikuwa anafuliwa ama hakuzoeshwa, ni mambo yanayotia aibu maana huu sio uafrika wetu, haijalishi hata kama mwanamke ana cheo kizito ni lazima amfulie mme wake nguo zake hizo ndio mila zetu waafrika tangu na tangu,
Siku hizi kazi zao ni Kudanga tu.
 
Kuna gender roles za kabla ya ndoa na baada ya ndoa.

Wanaume mabachela hupika, hujifulia, hufanya usafi wa jikoni, n.k. lakini mambo haya inabidi yawe majukumu ya mwanamke baada ya ndoa, ndio maana kuna msemo maarufu wa kuoa kufananishwa na "kuvuta jiko".
Mbona unakwepa kuelezea kwamba nao wanatakiwa kufundishwa kupika wakiwa wadogo pia. Mfano mimi ni mtu mzima ila nilifundishwa shughuli zote ikiwemo kupika nikiwa mtoto na imenisaidia sana sehemu mbalimbali. Ni vijana wangapi mabachela wanaishia kula magengeni na ma chips mayai sababu hawawezi kupika!?,kama ilivyo kwa mtoto wa kike vilevile kwa mtoto wa kiume kwenye shughuli zote, huko mbele ya safari hakuna guarantee ya kuoa wala kuolewa na hujui ni nini kitampa credit kwenye mazingira tofauti maishani awe wa kike au wa kiume.
 
Hapo umeshakubali kwamba kwenye ndoa kuna gender rokes na kupika ninkazi ya mwanamke kwenye ndoa.

Huo ndio mfumodume wenyewe.

Ndiyo maana nikisema kwa nfumo huu ni vigumu kunielewa.

Wewe unafuata mfumonwa kizamani, baba anafanya kazi, mama mke wa nyumbani.

Siku hizi wanawake wanasoma. Inawezekana baba na mama wote wanafanya kazi, kazi za nyumbani wakasaidiana pia.

Sasa hapi ukileta mambo ya gender roles kwamba mama ni mpishi wakati mama naye ni mfanyakazi, unaweza kuwa unamuinea huyo mama.

Kwa sababu na yeye anafanya kazinofisini kama baba na anarudi kachoka. Msingi wa mama kuw ampishi kwa kiasi kikubwa ulitokana na mama kuwa mama wa nyumbani.

Msingi huu unatoweka kwa kasi katika dunia ambayo mama naye anafanya kazi ofisini.

Ila, naelewa inawezekana hunielewi kwa sababu ya mfumodume uliokithiri huko kwenye jamii zetu.

Kuna uzi nimeuina jana mtu anasema "anamsaidia" mkewe kazi za nyumbani kwa sababu anaona mkewe anachika sana.

Sasa kama mkeo anafanya kazi ofisini halafu nyumbani anapika, mume hajui kupika, ikitokea kuna haja mke "asaidiwe" ( neno si sahihi, kwa sababu limefanya kazi ya kupika kuwa ya mje) mume atafanyaje hapo?

Bottom line, hizo gender roles ni za ulimwengu uliopita. Watoto wote wanatakiw akujua kazi zote na kusaidiana, hata wakikua na kuwa ndani ya ndoa.

Ila naeleea ni somo gumu bado kwa jamii zetu.
Sio mfumo dume ni majukumu ya jinsia katika ndoa,

Kiasi ambacho mwanamke inabidi afundwe mambo ya mapishi, usafi, n.k, huwa ni kikubwa zaidi kuliko mwanaume maana haya ni majukumu inayoobidi ayazoee, sisi wanaume kupika tunaweza lakini ni kitu ambacho hatujakizoea hivyo tunapooa huwa tunapokezwa jukumu hili na wanawake

Mwanamke ambae kazoeshwa na kufundwa majukumu ya ndoa huyafanya kwa ku enjoy wala sio kazi kwake, huona faraja kumpikia mme wake na kumfulia nguo, ni kitu ambacho kipo automated tayari wala sio jambo la kuanza kuambiana.

Ni kama sisi wanaume kukiwa na hatari inayotaka kuikumba familia ni jukumu letu automatically kuchukua steps za kulinda familia, sio suala la kuanza kujiuliza, ila siku hizi naona kuna wanaume wanakimbia wake zao hata kukiwa na nyoka na hii imechangiwa kwa baadhi kutojua majukumu yao,
 
Hapo umeshakubali kwamba kwenye ndoa kuna gender rokes na kupika ninkazi ya mwanamke kwenye ndoa.

Huo ndio mfumodume wenyewe.

Ndiyo maana nikisema kwa nfumo huu ni vigumu kunielewa.
Mfumo dumo uko dunia nzima na hakuna namna utaisha

Kibaya ni Mfumo Dume wenye dhamila mbovu ndio unapigwa vita

Kiranga nakuuliza swali unijibu hapa.

Tazama movie na miziki ya aina yoyote duniani........utakuta Mwanamke Character yuko Uchi ila kokote Mwanaume kavaa na kujistiri.

Huo ndio mfumo dume mbaya kupita yote.

Marekani kwenye mfumo unaodhaniwa ni Huru kwa Rika zote wana zaidi ya miaka 300 mpaka leo hakuna Rais Mwanamke.

Hata vyeo vya juu vya serikali wanawake ni wachache sana.

Sio kwamba hawana uwezo.

Tuna wanawake wengi wenye akili sana tu kuzidi Wanaume.

Tatizo ni vile mnatazama mfumo dume kama uadui na mnautumia vibaya.
 
Kiasi ambacho mwanamke inabidi afundwe mambo ya mapishi, usafi, n.k, huwa ni kikubwa zaidi kuliko mwanaume maana haya ni majukumu inayoobidi ayazoee, sisi wanaume kupika tunaweza lakini ni kitu ambacho hatujakizoea hivyo tunapooa huwa tunapokezwa jukumu hili na wanawake

Mwanamke ambae kazoeshwa na kufundwa majukumu ya ndoa huyafanya kwa ku enjoy wala sio kazi kwake, huona faraja kumpikia mme wake na kumfulia nguo, ni kitu ambacho kipo automated tayari wala sio jambo la kuanza kuambiana.

Ni kama sisi wanaume kukiwa na hatari inayotaka kuikumba familia ni jukumu letu automatically kuchukua steps za kulinda familia, sio suala la kuanza kujiuliza, ila siku hizi naona kuna wanaume wanakimbia wake zao na hii imechangiwa kwa baadhi kutojua majukumu yao,
Unarudi kulekule kwenye dunia ya kijima ya gender roles kwamba kazi ya kupika ni ya mwanamke.

Wakati tunaishi kwenye dunia ambayo ina wanawake wameolewa na professional chefs.
 
Mfumo dumo uko dunia nzima na hakuna namna utaisha

Kibaya ni Mfumo Dume wenye dhamila mbovu ndio unapigwa vita

Kiranga nakuuliza swali unijibu hapa.

Tazama movie na miziki ya aina yoyote duniani........utakuta Mwanamke Character yuko Uchi ila kokote Mwanaume kavaa na kujistiri.

Huo ndio mfumo dume mbaya kupita yote.

Marekani kwenye mfumo unaodhaniwa ni Huru kwa Rika zote wana zaidi ya miaka 300 mpaka leo hakuna Rais Mwanamke.

Hata vyeo vya juu vya serikali wanawake ni wachache sana.

Sio kwamba hawana uwezo.

Tuna wanawake wengi wenye akili sana tu kuzidi Wanaume.

Tatizo ni vile mnatazama mfumo dume kama uadui na mnautumia vibaya.
Kama mfumo dume upo dunia nzima na hautaisha, hiyo si sababu ya kuuendekeza.

Ushawahi kukataa kula kwa sababu njaa ipo dunia nzima na haitaisha?

Na mfumo dume unaomlazimisha mwanamke awe mpishi apende asipende, bila kujali anafanya kazi nje ya nyumba au hafanyi, amechoka au hajachoka, bila ya kumlazimisha mwanamme kufanya hivyo, ni mfumo onevu na wenye dhamira mbovu.

Unakosaje kuliona hilo?
 
Unarudi kulekule kwenye dunia ya kijima ya gender roles kwamba kazi ya kupika ni ya mwanamke.

Wakati tunaishi kwenye dunia ambayo ina wanawake wameolewa na professional chefs.
Sawa mkuu naona wewe endelea huko nyumbani kwako uwe unamfulia mke wako nguo, uwe unampikia mke wako, uwe unapiga deki, uwe unampokeza kupika kwenye misiba yeye awe anaenda na wanaume kuchimba kaburi, pia wezi wakija liwe jukumu lake kukulinda wewe.
 
Back
Top Bottom