Msaada: Familia inahangaika namna gani watawasadia watoto wawili wa nje wa marehemu

Moronight walker

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
3,105
4,635
Habari wa JF,

Kuna msiba wa ndugu mmoja jirani hapa. Sasa siku ya msiba walikuja watoto 2 wana umri wa miaka 5 na mama yao wanafanana sana na watoto mapacha wa kiume aliyozaa na mkewe wake ambao wana umri wa miaka 6. Ina maana jamaa alizaa nje watoto wamefanana na Baba yao ukiwaona ni kama watoto 2 wa ndani ya ndoa aliyezaa na mkewe.

Mkewe marehemu hajui nini cha kufanya hapo msiba ushaisha mpaka sasa. Familia wanajua hao watoto wanahitajika kutuzwa na kuishi. Marehemu kaacha nyumba moja aliyokuwa anaishi na mkewe na gari moja Toyota ICT na duka la madawa ya binadamu aliyokuwa anasimia mkewe, pesa za benk sijajua.

Sasa familia imeingia na kiwewe kuhusu hawa watoto 2 wa nje maana ni watoto wa ndugu yao kabisa. Kuna mtu mmoja amesema kama mama wa hao watoto anatafuta kusaidiwa malezi ya watoto aende ustawi wa jamii au akafungue shauri mahakamani, sasa inawezekana hio kweli.

Vipi kuhusu hapo watoto nani awapokee na ni nani awahudumie? Mke wa marehemu yeye ana kazi yake japo ni ya kawaida. Msaada jamani.
 
Cha kwanza ni kujua kama marehemu aliacha wosia au la baada ya kujua zoezi linalofata ni kumteua msimamizi wa mirathi na kuwatambua warithi ambapo na hao watoto wawili watajumuishwa kama warithi, kabla msimamizi hajaenda mahakamani kupata barua za kumteua.

Mkishindwa kuwajumuisha kama warithi wa mirathi ya baba yao wakienda mahakamani mapema tuu wanapewa chao, kesi ya Judith Patrick Kyamba and others vs Tunsuume Mwimbe Mahakama kuu iliyokaa Mbeya ilishasema kuwa watoto wa nje ndoa wana haki sawaa na watoto waliozaliwa ndani ya ndoa.
 
Cha kwanza ni kujua kama marehemu aliacha wosia au la.. baada ya kujua zoez linalofata ni kumteua msimamizi wa mirathi na kuwatambua warithi... ambapo na hao watoto wawili watajumuishwa kama warithi... kabla msimamizi hajaenda mahakamani kupata barua za kumteua

Mkishindwa kuwajumuisha kama warithi wa mirathi ya baba yao wakienda mahakamani mapema tuu wanapewa chao..kesi ya Judith patrick kyamba and others vs Tunsuume mwimbe Mahakam kuu iliyokaa mbeya ilishasema kuwa watoto wa nje ndoa wana haki sawaa na watoto waliozaliwa ndani ya ndoa
Hakuna wosia mkuu
 
Mbona hakuna mjadala hapo wote ni watoto wa marehemu. Kama wakiamua kagawa mali wanazo haki zote ni suala la familia.

Kuhusu malezi ya watotobado watakuwa chini ya mama yao(wako under 18). Isipokuwa kama mke wa marehemu ataridhia kuwalea wote kwa pamoja.
 
Mbona hakuna mjadala hapo wote ni watoto wa marehemu. Kama wakiamua kagawa mali wanazo haki zote ni suala la familia.

Kuhusu malezi ya watotobado watakuwa chini ya mama yao(wako under 18). Isipokuwa kama mke wa marehemu ataridhia kuwalea wote kwa pamoja.
Mali ipo moja tuu nyumba ambayo marehemu alijenga na mkewe kwa pamoja
 
Hivi, pamoja na kwamba hii story ni changamsha jukwaa, lakini ina vitu vya kujifunza.

1. Mwanaume, umeoa au niseme una familia. Hutambui kuna wanawake hawapendi hata ndugu zako?

2. Haya, umechepuka, umezaa. Watoto umekaa kimya. Maana unajua umeshavuruga. Unategemea ikitokea ukatangulia huko wakienda hawarudi, unaacha hali gani huko nyuma?

3. Ndo maana wanawake wengi ni makatili. Mmoja ataona mwenzie anataka amchukulie mali alizomuachia mmewe.

4. Mwingine ataona hajatendewa haki kutopewa kiasi kwenye mali za aliemzalisha. Wakati anashusha ka nguo kake kadogo, hajawahi kuwaza nini kitatokea? Au ni ile wanatulizwa akili kwa jambo sogo kwamba mi mwanaume ntayamaliza?!

5. Hao watoto, ambao tayari ni ndugu, watakaa waelewane? Sasa kama ndugu hawaelewani si ndo chuki na ugomvi vinaanza? Wengine watamani kulipiza kisasi kwa mateso ya mama yao? Af kwa wale wanawake wenye degree, wataanza ohh marehemu hajaniachia kitu ndo maana hali ngumu.

Wanaume, kama unaona mke mmoja hatoshi, elewana nae mapemaaa, bi mdogo mtambulishe ijulikane. Na kiukweli inauma na si haki, umehangaikia wanao na familia yako, kesho unaambiwa kuna watoto, unatajiwa na idadi, wanapata urithi hapa. Dadeki.
 
Back
Top Bottom