Huyu unayemuona hapo juu sio mwanamke, bali ni baba wa familia yenye watoto wanne ameamua kubadili muonekano wake ili kukwepa asiuliwe wakati wa vita.
Jina lake ni MINANI SAMUEL maarufu kwa jina la BABY kwa zaidi ya miaka 26 ameamua kuishi kama mwanamke anavaa nguo za kike, anasuka kama mwanamke na pia anavaa mapambo ya kike endapo ukikutana naye kwa mara ya kwanza itakuwia vigumu kugundua kuwa huyu ni mwanaume.
Miaka 25 iliyopita nchini Burundi zilitokea vita za wenyewe kwa wenyewe na wanaume ndio waliokuwa waathirika wakubwa, Wauaji walikuwa wakifanya msako kila nyumba na kuuwa mwanaume yeyote yanayemkuta,
Siku moja bwana MINANI alisikia sauti ya Mungu ikimueleza kuwa avae kama mwanamke ili asiuawe alipoitii sauti hiyo ghafla walivamiwa na wauaji walifanya msako katika nyumba yao bila ya mafanikio kwani wote waliowakuta waliamini kuwa ni wanawake.
Tangu siku hiyo MINANI hakuwahi kuvaa kabisa nguo za kiume kabati lake limejaa nguo za kike tu, Licha ya kuwa ni baba wa familia lakini hajaacha kuvaa nguo za kike.