Je, Watoto wako wanamuheshimu Dada wa Kazi Nyumbani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Inafikirisha unapokuta mtoto anakosa heshima kwa dada anayemlea na kukaa naye nyumbani pale wazazi wanapokuwa kazini. Na mara nyingine mzazi anaona ni sawa tu na wala hamkemei mtoto wake kwa tabia hizo.

Unakuta mtoto anamuona dada wa kazi kama mtu asiye na thamani na wa kudharaulika. Na mara nyingine mzazi anaona ni sawa tu na wala hamkemei mtoto wake kwa tabia hizo.

Akiamka asubuhi wala hamsalimii, anatupatupa vitu ovyo, akijua kuna mtu wa kuviokota. Akila anaacha vyombo hapohapo mezani na kumuamuru dada wa kazi avitoe na anaongea naye kwa lugha ya dharau.

Yaani mtoto mdogo anaweza kumgombeza dada wa kazi kama wamelingana vile, hali ambayo si sawa.

Mtoto akiachiwa kuendelea kuonyesha dharau kwa msichana wa kazi ambaye anakaa naye kila siku na kumlea, atajenga tabia ya ukorofi na kudharau mtu yeyote anayehisi yuko chini yake.

Hii itampelekea kuwa na mahusiano mabaya kuanzia shuleni, kazini hadi kwenye familia yake huko mbeleni. Ni vizuri mtoto tangu akiwa na umri mdogo afahamu kuwa watu wote ni sawa na hakuna mtu bora zaidi ya mwingine.

Jinsi mtoto anavyoishi na dada wa kazi inategemea kwa kiasi kikubwa na mfano anaoupata kutoka kwa mzazi wake. Je, unawapa dada wa kazi heshima stahiki? Unawapa ujira wao vyema? Unakumbuka kuwanunulia nguo? Anapata muda wa kupumzika? Akiugua unajali?

Kama hufanyi hivi vitu vyote usitegemee mtoto wako kufanya vinginevyo. Mara nyingi familia ambazo huishi na dada wa kazi kama mmoja wa familia huwa na watoto wanaoonyesha upendo na kuwaheshimu wafanyakazi hao.

Tukitathmini, kuna mambo madogo madogo huwa tunajisahau hasa yanayowahusu hawa mabinti.

Mfano, unakuta familia ina watoto wadogo wengi, hiyo adha ya kuwahudumia wote, kusafisha nyumba, kupika, kufua halafu tukirudi nyumbani muda wote tunawafokea.

Ama unakuta familia imekwenda matembezi, wamevaa kwa kupendeza na watoto wao, halafu msichana wa kazi anayekulelea watoto kavaa kama chokoraa. Hii siyo sawa.
 
Hili ni janga la wajinga waliojaa katika zama hizi za wanaojiona wasomi huku wakishindwa kuviongoza vitoto vyao tu.Kifu watoto wanaodharau dada wa kazi,ni 90% wanawadharau hata wazazi wao wenyewe.Mtoto mwenye nidhamu kwa wazazi wake hawezi kuwa na dharau kwa dada wa kazi.
 
Mada nzuri sana na yakujenga, watoto wengi wanaowadharau dada wa kazi huwadharau pia wazazi wao ila haionekani kwa sababu baadhi ya wazazi ni hovyo kimalezi. Mzazi anaetimiza jukumu lake vyema la malezi ni lazima amfundishe mtoto kuheshim kila mtu.

Kufupisha, mtoto mdogo mwenye vitabia vya hovyo na dharau ni picha halisi ya tabia za wazazi/walezi wake kwa sababu kwa % kubwa anajifunza kwao. Tunda huwa halianguki mbali na mti.
 
Watoto wanajifunza yale ambayo wazazi wanatenda,,,kama mama hamuheshimu dada ,, watoto wataanzaje kumuheshimu.
 
Mada nzuri sana na yakujenga, watoto wengi wanaowadharau dada wa kazi huwadharau pia wazazi wao ila haionekani kwa sababu baadhi ya wazazi ni hovyo kimalezi. Mzazi anaetimiza jukumu lake vyema la malezi ni lazima amfundishe mtoto kuheshim kila mtu.

Kufupisha, mtoto mdogo mwenye vitabia vya hovyo na dharau ni picha halisi ya tabia za wazazi/walezi wake kwa sababu kwa % kubwa anajifunza kwao. Tunda huwa halianguki mbali na mti.
Kimsingi watu ambao wamefanikiwa huwa wanawazarau sana wasaidizi wao wa ndani
 
Aisee mtoto ni lazima aheshimu mtu yeyote awe wa nyumbani kwao au hata wa nje. Ukiwajengea hivo ni lazima atamuheshimu huyo house maid. Maswala ya mtoto kumaliza kula na kuacha sahani mezani kwangu siviruhusu. Mtoto wangu mdogo ana miaka minne tangu akiwa na miaka miwili nlikua namwelekeza kushukuru kwa chakula na kutoa sahani yake mezani.
 
Ukiona Mzazi anaruhusu hayo kwa mwanae, basi tambua kuwa Mtoto wa Nyoka ni Snake.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom