Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,468
- 119,622
Hahahahahahaaaa.... Namuomba Mungu aniepushie mbali( watenda dhambi pia huomba Mungu na huwasikia)
Mdogo wangu angelita...tunaishi kwa neema ya Mungu tu. Hatupaswi kujivuna kwamba Mungu anatusikia pamoja na uovu wetu. Ofcourse mi sijaona kwenye biblia sehemu iliyoandikwa kwamba Mungu anasikia maombi ya wenye dhambi ila nimeona Mungu akiwaponya wenye dhambi pale wanapopondeka na kujutia uovu wao. Ukisoma Isaya 1:1-30Neno linasema waziwazi kuhusu maombi ya wenye dhambi. ......nakushauri ukasome. Mstari ule wa 15 anasema 'Nanyi mkunjuapo mikono yenu,nitaficha macho yangu nisiwaone;naam,mwombapo maombi mengi,sitasikia mikono yenu imejaa damu. Jiosheni,jitakaseni,ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu;acheni kutenda mabaya;jifunzeni kutenda mema...............'
Kwa kuongezea kasome na warumi 6
Moreover....u don't need to feel inferior kwa hilo ukajiona we ndo mtenda dhambi saana..... Mungu anakutazama kama anavyomtazama mtu yeyote anayetenda dhambi yoyote iwe ni uwongo,wizi,kiburi, uzinzi(rwgardless unazini na nani). Neema ya Mungu ituvutayo kwake ili tupate kutubu ipo sawa tu kwa wote. Ila sasa wewe unaweza kuwa pagumu kama huyo mama ataamua kumlilia Mungu kwaajili ya hayo mahusiano yenu...hasa kama huyo mama ni mtu wa haki. Trust me Mungu haoni hasara kuadhibu na kuangamiza maelfu kwaajili ya mwenye haki mmoja anayedhulumiwa. (kama wewe ni msomaji wa biblia hutabisha kuhusu hili) maana kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana kama akiomba kwa bidii.
Nilikuwa nakukumbusha tu mpendwa kama kuna mahali nimekukwaza nisamehe bure.....mimi ni binadamu tu ambaye pia nimepungukiwa utukufu wa Mungu.
Last edited by a moderator: