Mmachinga Atakapouawa...

Mmachinga Atakapouawa...

Wewe umesema wanapangiwa maeneo, ndiyo nimeuliza wamepangiwa wapi ?
Ndo mana nimekuuliza wale waliohama bila shida kwani wamepangiwa wapi?

Hao waliohama Mbona hawajalalamika kuwa Hakuna maeneo waliyopangiwa?

Nani hawajui watanzania? Wengi wanapenda ulalamishi! Hata wakiambiwa wasajili simu zao hawaendi hadi deadline ifike!

Maeneo waliyopangiwa yapo na yametangazwa fuatilia clips za Wakuu wa wilaya kama Jokate na hata Mkuu wa Mkoa Amos Makalla wametangaza hayo maeneo huko Temeke, Mbagala, ILALA, Mbezi n.k
 
Mama pia awe makini maana hawahawa ndio wanaweza wakaanzisha maandamano ya kumtoa madarakani.

Na uhakika hawa jamaa wakisimama kidete, polisi hawawezi fua dafu, na hapo ndipo awamu ya sita tutaanza kuona mapichapicha ya ajabu.

Ustaraabu ufuatwe.
Hakuna cha Maandamano andamana Basi uone....ujenge katikati ya barabara uanzishe uasi?? Hilo halipo..Anzisheni Uasi muone.
 
Kama mwenyekiti kakimbia fimbo za askari mimi ni nani? Wa kuanzisha maandamano 😅😅
 
Hili linaweza kutokea...tusipokuwa waangalifu tunatengeneza adui asiyekuwepo. Kuua nzi kwa gobole si uhodari na kuua sisimizi kwa bomu si ushujaa. Hatujalifikiria vizuri kwani tukiwalazimisha vijana wafike kwenye gema la kukata tamaa taifa litalipaaa.. tulifikirie vizuri...
Unashauri nini kifanyike ?
 
Well said Mwanakijiji, watu wanasema eti wamachinga waondoke, ukiwauliza waende wapi hatuna majibu
Tukiwauliza serikali imetenga sehemu gani ili wamachinga wakafanye hughuli zao wapate rizki hatuna majibu!
Usafi wa miji hawezi kuwa na priority kuliko matumbo ya watu!
Kupenda uchafu ni dalili ya umaskini.
 
Hakuna mmachinga aliyeama kwa hiyari muda wowote kitanuka ndio maana kila kona wamemwaga mapolisi.

Vibanda vinavunjwa usiku asubuhi unakuta mtaa wote msafi....machinga gani wanahama usiku wa manane.

Jazaneni ujinga tu soon mtakipata mnachokitafuta watu wana hasira sana kumnina
Suala la Machinga limeshamalizwa kistaarabu, endelea na maombi yako mfu
 
Hili linaweza kutokea...tusipokuwa waangalifu tunatengeneza adui asiyekuwepo. Kuua nzi kwa gobole si uhodari na kuua sisimizi kwa bomu si ushujaa. Hatujalifikiria vizuri kwani tukiwalazimisha vijana wafike kwenye gema la kukata tamaa taifa litalipaaa.. tulifikirie vizuri...

Who got us here in the first place? Tulipo sasa lazima kuwe na majawabu ya hili tatizo. Na gharama zake zipo. Zinalipwaje?
Tumekosa diversification ya uchumi wetu? Nguvu kazi iliyopo haiwezi kuajiriwa rasmi yote. inakwenda wapi?
Kuwa wachuuzi bado sio jawabu
 
Well said Mwanakijiji, watu wanasema eti wamachinga waondoke, ukiwauliza waende wapi hatuna majibu
Tukiwauliza serikali imetenga sehemu gani ili wamachinga wakafanye hughuli zao wapate rizki hatuna majibu!
Usafi wa miji hawezi kuwa na priority kuliko matumbo ya watu!
Hakuna jambo lisilofanyika kwa mipango. Hata hiyo njaaa inadhibitiwa kwa mipango sio uholela. Zama za uholela kaondoka nazo muuza vitambulisho visivyo na picha ya mmiliki
 
Yeye ni mwanamke. Haya wewe mwanaume ingia mtaani uwatetee machinga.
Wamachinga hawaitaji support ya yoyote kupambana wewe kaa hapo usubiri kama unafikiri haya mambo yataisha kirahisi.
Wamachinga wanasimama wenyewe na wataisimamisha nchi ndio maana hawajomba back up ya mwanasiasa yoyote coz wanajua hao ni wachumia tumbo.
 
Hili linaweza kutokea...tusipokuwa waangalifu tunatengeneza adui asiyekuwepo. Kuua nzi kwa gobole si uhodari na kuua sisimizi kwa bomu si ushujaa. Hatujalifikiria vizuri kwani tukiwalazimisha vijana wafike kwenye gema la kukata tamaa taifa litalipaaa.. tulifikirie vizuri...
What a shame mkuu.

Miaka 60 sasa tunaendelea kujenga Taifa la wauza vitumbua, chapati, mandazi, mihogo kwenye beseni, karanga.

Tulikosea, tumekosea na tunaendelea kukosea. Kibaya ni kwamba hatukotayari kujifunza.
 
Ndo mana nimekuuliza wale waliohama bila shida kwani wamepangiwa wapi?

Hao waliohama Mbona hawajalalamika kuwa Hakuna maeneo waliyopangiwa?

Nani hawajui watanzania? Wengi wanapenda ulalamishi! Hata wakiambiwa wasajili simu zao hawaendi hadi deadline ifike!

Maeneo waliyopangiwa yapo na yametangazwa fuatilia clips za Wakuu wa wilaya kama Jokate na hata Mkuu wa Mkoa Amos Makalla wametangaza hayo maeneo huko Temeke, Mbagala, ILALA, Mbezi n.k
Ilitosha kujibu wamepangiwa wapi,
Kama hujui wamepangiwa wapi unatulia usilete siasa za kitoto kwenye kula ya watu.
 
Ulipouliza swali Mbona haukujiuliza wale waliohamisha vitu vyao bila shida wameenda wapi?

Hakuna maisha yasiyo na utaratibu! Hata kwenye kula kuna utaratibu
 
Wewe mwenyewe ulisema wamepangiwa maeneo nimekuuliza wamepangiwa wapi ?
 
Hili linaweza kutokea...tusipokuwa waangalifu tunatengeneza adui asiyekuwepo. Kuua nzi kwa gobole si uhodari na kuua sisimizi kwa bomu si ushujaa. Hatujalifikiria vizuri kwani tukiwalazimisha vijana wafike kwenye gema la kukata tamaa taifa litalipaaa.. tulifikirie vizuri...
Futilia mbali hao wapiga kura
 
Back
Top Bottom