Mliooa mnastahili pongezi

Mliooa mnastahili pongezi

lazima kuna aina fulani ya stress itakuwa inakusonga....hao rafik zako wanachangia sana ww kuwa na mtazamo huu kwenye swala la kuoa,
Mmh
Kwahiyo hiko ndio kinakufanya usitamani kuoa
Habari za Jumapili.

Napenda kutoa pongezi kwa wwanaume wenzangu mliooa. Kuamua kuoa si jambo rahisi hasa ukifikiria unakabidhi UHURU na MALI ZAKO kwa mtu ambae huna undugu nae!!

Mawazo kama haya huwa yananijia Jumapili ambayo ni siku ninayofurahia sana wiki nzima. Jumapili njema jamani mimi nasikiliza Easy Sunday Clouds Fm huku nikisoma kitabu taratibu.
Sijui nini kinawafanya mje na conclusion kuwa SITAKI KUOA. Ninachotoa hapa ni pongezi kwa waliooa kwasababu si uamuzi rahisi. Muda ukifika nitaamua kuchukua maamuzi magumu.
 
Kukabidhi Mali zako kwa mwanamke asiye ndugu yako kauli ya kibinafsi

Uoga huwa upo ukiamua unaweza muda ukifika utaoa lkn usitangulize Mali zako atazifaidi mke tena asiye nduguyo je unataka uoe nduguyo ni hayo tu jpili njema
Umenishangaza tu uliposema eti napondaga kuoa.
 
Nimechunguza marafiki zangu waliokimbilia ndoa hawana maisha ya furaha...
Hawanishawishi kuingia huko...
Sawa sawa vizuri changamoto zinafanana km za upinzani km ni mvulana lazima uhamie chama tawala na km unaona kuja huku ni teso endelea kubachelika mkuu
 
Sijui nini kinawafanya mje na conclusion kuwa SITAKI KUOA. Ninachotoa hapa ni pongezi kwa waliooa kwasababu si uamuzi rahisi. Muda ukifika nitaamua kuchukua maamuzi magumu.
Kila la heri Mungu akusaidie upate mke wa kufanana nae
 
Kuamua kuoa si jambo rahisi hasa ukifikiria unakabidhi UHURU na MALI ZAKO kwa mtu ambae huna undugu nae!!

Ni kweli wanastahili pongezi kwa kuwa kuna faida nyingine nyingi wanazipata katika ndoa zinazozidi umuhimu wa UHURU na MALI ZAO.
Umeshawahi kufikiria ikitokea ukaumwa sana kiasi cha kushindwa hata kujiogesha, sio uhuru wako wala mali zako zitakazo kusaidia?
UTU ni bora kuliko UHURU na MALI.

Hatahivyo, ukiona mtu anajutia ndoa yake jua alikosea kuoa,ila ukipatia kuoa hutahofia UHURU wala MALI ZAKO.
 
Daah... hongera saana mkuu kwangu wewe ndiye unastahili pongezi ni Wanaume wachache wanaofanya uamuzi kama huu.
 
Hivi wewe unafikiri mungu hana akili eeeh......unadhani kwa nini alipomuumba adamu akagundua kuna kitu hakipo sawa akaamua kumuumba mwenza wake.......sasa wewe usioe ubaki hivyo hvyo .......halafu naskia harufu ya roho mbaya kutoka kwako
 
Back
Top Bottom