Mkuu wa Mkoa wa Manyara: Baadhi ya Wananchi wa Kisangaji (Babati) hawataki kujenga vyoo wanajisaidia porini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sengida amejibu hoja ya Member wa JamiiForums.com aliyedai Wilaya ya Babati, Kata ya Magugu, Kijiji cha Kisangaji kuna Ugonjwa wa Mlipuko wa Kipindupindu lakini Serikali haisemi.

Kusoma hoja ya member ipo hapa - Serikali iweke wazi Ugonjwa uliopo Kijiji cha Kisangaji, Babati (Manyara) kama ni kipindupindu watu wachukue tahadhari

Majibu ya Queen Sengida
Kwanza nimesoma hoja ya Mdau, inavyoonekana si mfuatiliaji wa taarifa za habari za Babati kwa jumla, pia hoja yake ilikuwa ni gulio kufunga.

Alilalamika gulio kufungwa bila kutolewa taarifa, pia nilipitia comments nikaona watu walivyomjibu, nielezee kuwa mimi mwenyewe Machi 8, 2024, nilienda kwenye local media mbili na moja ya ujumbe nilioutoa ni kuhusu habari ya Ugonjwa wa Kipindupindu.

Hakuna usiri, kulikuwa na visa kadhaa vya kipindupindu, tulivitangaza na vimeondoka, na jana (Machi 17, 2024) tulifungilia magulio kuendelea na kazi.

Kule kwao kuna changamoto sana ya suala la afya, hawataki kujenga vyoo wanajisaidia porini.

Tumekuwa tukiwapa elimu mara nyingi, sijui wakiambiwa choo wanajua ni choo cha kuvuta. Choo kinaweza kuwa cha kitobo, kitunzwe vizuri kwa kuwekwa majivu ili kuua vijidudu na pale kwenye tundu kinawekwa kibao kuzia nchi wasiingie na kutoka.

Pamoja na yote tunaendelea kutoa elimu kwa kuwa tulikuwa na mvua kubwa tukaamini changamoto ya kipindupindu itakuwa kubwa lakini haikuwa kubwa kiwango kama tulivyotegemea.

Pia kuendelea kutoa elimu tumeongeza huduma ya Wataalam wa Afya ya Misingi wanaopita nyumba kwa nyumba kutoa elimu, mbali nah apo watuletee ripoti kamili ya kujua tuna changamoto kiasi gani ya uhaba wa vyoo kutokana na mvua zilizoendelea kuharibu baadhi ya vyoo.”
 
Wapongezwe watu wa Manyara kwa kujisaidia porini

Sasa hivi dunia inahangaika utunzaji wa mazingira ikiwemo kupanda miti na kuhakikisha inastawi.Sasa wao ili kuhakikisha miti inastawi wanaiongezea virutubisho kwa kuipa mbolea wanapojisadia huko porini ili istawi vizuri.

Mikoa mingine iige watu wa Manyara ili muda sio mrefu tufikie kwenye Tanzania ya kijani yenye miti.na mapori yaliyostawi hasa na kijani kila sehemu

Watu wa mazingira wanatakiwa wawalipe watu wa manyara kwa kujali.miti pori na kuiwekea mbolea original toka tumboni mwa binadamu.
Hata mkuu wa mkoa na viongozi wengine wa mkoa wa Manyara waunge mkono juhudi za wananchi kwa kushirikiana nao kwenye hilo na wananchi wa Manyara
 
Hahaha
 
Hili la kujisaidia porini ni sawa na Tanga wanajisaidia kando ya bahari, hawataki kutumia vyoo hata ukiwajengea mwaka mzima haingii mtu.
 
Back
Top Bottom