Madai ya Mlipuko wa Kipindupindu Simiyu, RC asema ‘Ni Ugonjwa wa Matumbo, tumewapiga faini Wananchi wasio na vyoo’

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda amezungumzia madai ya uwepo wa mlipuko wa maambukizi ya Kipindupindu katika Wilaya ya Bariadi Mkoani hapo akisema kuwa kilichotokea ni magonjwa ya tumbo na tayari Serikali inachukua hatua kisha akatoa ushauri kwa Wananchi.

Amesema hayo siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums kuandika kupitia Fichua Uovu juu ya ukimya wa Serikali juu ya suala hilo akidai kuwa wagonjwa aliowashuhudia katika Mitaa ya Majaida na Imalilo, Kata ya Buhnamala ameonesha dalili za kuwa na maambukizi ya Kipindupindu.

Dkt. Yahaya amesema “Tumepata kesi za Wagonjwa wanne wenye matatizo ya magonjwa ya Tumbo, hivyo nawaomba Wananchi kipindi hiki cha mvua wachemshe maji ya kunywa, wale ambao hawana vyoo na wanajisaidia kwenye vyanzo vya maji wahakikishe wanakuwa na vyoo na wavitumie.

“Nimewaelekeza Wakuu wa Wilaya kuwachukulia hatua watu wote ambao hawana vyoo na wamekuwa na tabia ya kujisaidia maeneo ya wazi, vichaka na vyanzo vya maji, kwani wao ndio chanzo cha magonjwa ya Tumbo.

“Tumeshapiga faini Watu 10 ambao hawana vyoo kabisa, nimeagiza Wakurugenzi kuwa hilo zoezi liwe endelevu, pia ndugu zetu wa Wizara ya Afya wametutembelea wakiwa katika ziara yao ya Kanda ya Ziwa.

“Sampuli zimeshachukuliwa kwa ajili ya vipimo lakini kilichobainika katika hatua za awali ni magonjwa ya tumbo ambayo yanaweza kusababishwa na mambo mengi, muhimu ni kuchukua tahadhari ya kuzingatia usafi wa mikono yetu na vyakula tunavyokula.

Hoja ya awali ya Mdau hii hapa - Bariadi yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu
 
Kwa hiyo Masikini asipokuwa na choo ni moja ya vyanzo vya mapato vya Serikali


Kweli inabidi tutafute Pesa kwa kasi sana hadi DPP awe hana nia ya kuendelea ma mashauri yako ya jinai
 
Kipindupindu miezi hii ya December hadi February ndiyo huwa miezi yake ya kulipuka.

Elimu iendelee kutolewa kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa na vyoo bora pamoja na matumizi sahihi ya vyoo.

Kampeni ya nyumba ni Choo ipelekwe huko.

Najua Mkuu wa Wilaya Mhe. Simon Simalenga hawezi kushindwa hili
 
Dahh....
Au basi, ngoja niishie hapa tu nisije nikashtakiwa na jamuhuri ya watu wasio jielewa.
 
Yaani MTU anajenga nyumba choo anaacha 😂😂😂😂mazafaka huyo apigwe fain achimbishwe na choo under police
 
Back
Top Bottom