Manyara: Polisi watumia mabomu kutawanya wananchi waliozingira kituo cha Polisi wakimtaka mtuhumiwa aliyebaka na kumchinja mtoto wa miaka 6

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limelazimika kurusha mabomu ya machozi kutawanya wananchi wa Magugu waliokuwa wanataka kuchoma kituo cha Polisi kwa madai ya kumtoa mhalifu aliyedaiwa kubaka mtoto wa miaka sita kisha kumchinja

Baada ya mtuhumiwa kuokolewa na Polisi na kupelekwa kituo cha Polisi magugu wananchi hao wamevamia kituo na kutaka kumtoa mtuhumiwa kwa nguvu hali iliyofanya Jeshi hilo kuchukua masaa kadhaa kuwatawanya huku magari na abiria kutoka Arusha yakilazimika kupaki baada ya wananchi kuchoma matairi.



MWANAFUZI wa Chekechea mwenye umri wa miaka saba mkazi wa kijiji cha Mapea kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara ameuwawa kwa kuchinjwa na mtu asiyejulikana.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mapea Filmon Mbogo, amekiri kutokea kwa tukio hilo leo Februari 20, 2024 katika kijiji chake na kusema baada ya kupata taarifa hizo ameliarifu jeshi la polisi ili kupata maelekezo kuhusu mwili huo.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mapema wamesema mtoto huyo alikuwa anasoma katika shule ya msingi Mapea, na wakati wakitoka shule walikutana na mtu wasiomfahamu ambaye aliwadanganya anakwenda kuwachumia mazambarau ambapo alimchukua mtoto huyo na kwenda kumchinja shambani kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.

Aidha, kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, George Katabazi amethibitisha kutokea kwa tukio nakusema atatolea ufafanuzi baada ya kupata taarifa kamili.
 
Hii habari nimetoka kuiangalia kwa Millardayo. Wananchi wanasema akifa Pundamilia polisi wanajaa kijijini kutafuta muuwaji. Lakini hii issue ya mtoto kuuliwa wamekaa kimya.

Ni huzuni kwakweli
 
Hîi Nchi Sasa ilipofikia bila kujichukulia Sheria mkononi mambo hayataenda mana Serikali ni kama imekula yule samaki aitwae pono
 
Back
Top Bottom