DOKEZO Serikali iweke wazi Ugonjwa uliopo Kijiji cha Kisangaji, Babati (Manyara) kama ni kipindupindu watu wachukue tahadhari

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Huku mtaani kwetu kuna mlipuko wa magonjwa ya tumbo ambayo wataalamu wa mambo wanadai ni mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu.

Nina ndugu zangu kadhaa hapa Mkoani Manyara, Wilaya ya Babati, Kata ya Magugu, Kijiji cha Kisangaji tangu wiki iliyopita kumekuwa na idadi kubwa ya waathirika wa kuumwa tumbo na wengine wanahamishwa kutoka Zahanati ya hapa Mtaani kuelekea Hospitali ya Wilaya kwa ajili ya matibabu zaidi.

Zahanati hiyo ilikuwa na wagonjwa wawili baadaye wakaongezeka hadi kufikia 25 na zaidi.

Kinachonifanya niamini inawezekana kweli ni Kipindipindu, Serikali ilitangaza kuufunga mnada ambao huwa unafanyika mara moja kwa wiki katika Kijiji mikoja cha jirani na hapa tulipo sisi.

Mnada huo huwa unafanyika kila Jumatano, wiki iliyopita Machi 6, 2024, haukukuwa na mnada huo kwa sababu za kiafya lakini hakukuwa na ufafanuzi zadi, hivyo hatujui kama keshokutwa Mnada utaendelea.

Serikali inaingiz mapato mengi kupitia Minada, hivyo uamuzi wa kusitisha Mnada inamaanisha hata wao wanapoteza mapato kwa wingi pia, hivyo hawawezi kufanya maamuzi hayo kama jambo ni dogo.

Ushauri wangu kama kuna Kipindupindu Serikali iseme na iweke wazi ili tahadhari zichukuliwe zaidi, kwani sijapata taarifa ya kifo lakini pia sijui wagonjwa wanaendeleaje.

Majibu ya Mkuu wa Mkoa - Mkuu wa Mkoa wa Manyara: Baadhi ya Wananchi wa Kisangaji (Babati) hawataki kujenga vyoo wanajisaidia porini
 
Back
Top Bottom