Mkutano wa Mwigamba na vyombo vya habari

Mkutano wa Mwigamba na vyombo vya habari

Haijawa vipande vipande lakini chama kiko mapande mawili ndiyo maana karibu wote walionyanyasika ni wa kanda ya ziwa baadhi ni hao uliowataja hapo juu pamoja na Shibuda, Zitto, Kabouru, Wangwe, Mwigamba nk. lakini wa Moshi-Arusha wanakula kuku.

Unataka kusemaje?dar-moro pamoja mbeya na iringa unawafikishia ujumbe gani wana chadema?Shibuda huyu huyu au mwingine?Wangwe?
 
Huko nyuma walishazuka Mwigamba wangapi but CDM inazidi kukua?... Mawazo ya Mwigamba ni sawa na mpo kwenye mashindano ya magari kutoka Dar hadi Moro, mmefika Chalinze, CCM mmeshamuacha Mlandizi huko halafu Mwigamba anasema "simamisheni gari, hii JEEP sio nzuri, twendeni turudi Dar najua kuna jamaa ana Vogue yake nzuri sana atatuazima tukamalizie nayo mashindano"!!!

Jiulize kwanza walioondoka waliibua kashfa zipi?Lakini pia msisahau kuwa CHADEMA inaandamwa na kashfa za Ukanda na Ukabila huenda mnaoshinda humu katika mitandao ya kijamii hamlielewi hili lakini Watanzania wanafuatilia hatua kwa hatua.Kufukuzwa kwa Mwigamba CHADEMA kama wengi wenu mnavyodanganyana humu kutafuatiwa na serious consequences.Watanzania watajiuliza mbona ni wa huku tu na si wa kule ndio wanaoonekana hawafai.
 
Jiulize kwanza walioondoka waliibua kashfa zipi?Lakini pia msisahau kuwa CHADEMA inaandamwa na kashfa za Ukanda na Ukabila huenda mnaoshinda humu katika mitandao ya kijamii hamlielewi hili lakini Watanzania wanafuatilia hatua kwa hatua.Kufukuzwa kwa Mwigamba CHADEMA kama wengi wenu mnavyodanganyana humu kutafuatiwa na serious consequences.Watanzania watajiuliza mbona ni wa huku tu na si wa kule ndio wanaoonekana hawafai?Labda wanataka kututumia tu kisha watugeuke huko mbele ya safari halafu waanze kupeana wao kwa wao.Tafakarini juu ya jili.Siasa ni mchezo unaohitaji kuchezwa kwa akili na umakini mkubwa sana.
 
Mkumbushe pia, Aige wenzake wanaojua mambo ya siasa vizuri!

Mkumbushe pia , Tabia zake/ kiherehere/ Sumu / Tindikali zina mwisho wake!

Mkumbushe pia aongeze ELIMU ya uraia na maarifa mengine ya Siasa.

Ungekua na sifa hizo ungezamia mishikaki mondoli.Punguza uroho.Mwenyekiti mzima wa UVCCM mkoa unazamia mishikaki unaita ni mojawapo wa mbinu za kisiasa?Grow up!
 
Unataka kusemaje?dar-moro pamoja mbeya na iringa unawafikishia ujumbe gani wana chadema?Shibuda huyu huyu au mwingine?Wangwe?
Viongozi wa chadema kanda ya ziwa meshashtuka ndiyo maana wananyamazishwa na kupewa kibano. Mbeya-Iringa wanacheza ngoma wasiyoijua. Moshi-Arusha wanakula keki peke yako ukileta hoja hata kama ya msingi ni OUT.
 
Mwaka 2011, Mwalimu Secondary na mshahara wa Tsh. 1,900,000/= mbona inaonyesha wazi huyu jamaa ni muongo? yaani hata mkuu wa Idara Secondary wakati huo alikuwa hapokei kiasi hicho cha fedha.
Mkuu, Hujasoma vizuri: mwaka 2004 alikuwa akifundisha Mukidoma. mimi namfahamu huyu jamaa; 2011 hakuwa mukidoma! 1900k ilikuwa ni kutoka kwa mwajiri mwingine ambaye hakumtaja!
 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, amesimulia namna alivyovamiwa na kupigwa na Wanachadema wenzake mithili ya mwizi.

Mwigamba alipata kipigo hicho mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya uongozi wa juu wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei katika ukumbi wa Hoteli ya Coridal Spring, jijini Arusha wakati wa Mkutano wa Baraza la Uongozi la Chadema, Kanda ya Kaskazini.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Mwigamba ambaye ameahidi kuweka kila kitu wazi leo, alisema yeye hakupigana bali alipigwa na anamtuhumu kiongozi wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), aliyemtaja kwa jina la Noel Olewaroya, kuwa ndiye aliyeanza kumpiga.

Kiongozi huyo anayesubiri barua ya kusimamishwa uongozi, baada ya kupata taarifa za hatua hiyo katika vyombo vya habari, alidai kuwa kijana huyo na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ndio walioanza kumshambulia wakilenga kumnyang’anya simu na kompyuta yake ya mkononi ndani ya mkutano huo.

Kwa mujibu wa madai ya Mwigamba, Lema alikuwa akisema nataka simu na yeye akamjibu kuwa hatampa na wakati akienda kumnyang’anya, kuna mmoja wa wajumbe aliwahi kumshika Mbunge huyo.

“Wakati Lema ameshikiliwa, huyu Noel ambaye hakuwa mjumbe wa kikao nadhani ni mtandao wa Lema, alitokea huko akanikwida akanipiga ngumi ndio na mimi nikalazimika kujibu.

“Nilitoa simu kwa Katibu wa Kanda, Aman Golugwa, na hali ikawa imetulia lakini kumbe Lema alikwenda nje kuchukua jiwe linalotumika kupanga barabarani akanirushia kichwani…nilikwepa na kwa bahati mbaya nikaanguka nikapiga kichwa nikaota nundu…si kubwa sana,” alisimulia Mwigamba.

Baada ya hapo, kikundi cha vijana wa Chadema maarufu Red Brigades, kwa mujibu wa Mwigamba, kilimvamia na kumbeba na kumtoa nje ya ukumbi kama mwizi huku wakimpiga mateke.

“Unafahamu Tanganyika Jeki? Ndivyo walivyonibeba huku wakinipiga mateke mpaka nje…wakati huo Mbowe alishatoka nje na ninadhani kompyuta yangu na simu walikuwa wakipeleka kwake,” alidai.

Alidai alipofikishwa nje, alimuona Mbowe akiwa katika gari lake amefunga vioo na vijana hao walimbeba kwa mtindo huo wa Tanganyika Jeki mpaka mbele ya gari hilo, wakamsimamisha kisha wakampiga mtama akadondoka chini.

“Nilimwambia Mbowe aliyekuwa akishuhudia kuwa anachofanya si vizuri, lakini hakujibu mpaka Katibu wa Kanda, Golugwa, alipokuja wakanitoa na kuniweka pembeni,” alisema. Muda mfupi baada ya hapo, alisema gari la Polisi lilifika ndipo akaingizwa ndani yake na kupelekwa Polisi.

Gazeti hili lilimtafuta Mbowe kuhusu madai ya Mwigamba kupigwa mtama mbele ya gari lake huku akishuhudia, lakini akalalamika kwamba yeye si gari na kutaka aelezwe wapi gazeti hili, lilipata taarifa kwamba yeye amempiga ngumi Mwigamba.

Mwandishi alipomtaka asome vizuri gazeti la HabariLeo Jumapili, kwamba halijaandika taarifa za yeye kumpiga ngumi Mwigamba, alijibu kwamba suala hilo, kuna wasemaji wa chama, ndio wanaopaswa kulizungumzia.

Lema anayetuhumiwa na Mwigamba kuanzisha vurugu hizo, kumrushia jiwe, kuagiza vijana kumpiga, alipopigiwa simu, iliita bila majibu. Gazeti hili lilimtafuta Msemaji wa Chadema, John Mnyika, kuhusu pamoja na mambo mengine, hatua ambazo chama kitachukua dhidi ya kiongozi wa Bavicha, Noel anayedaiwa kumpiga Mwigamba ngumi na kuingia katika kikao ambacho hakuwa mjumbe, lakini simu yake iliita bila majibu kama ya Lema.

Baadaye Mnyika alipiga simu na kuagiza Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, atafutwe kwa kuwa alikuwa eneo la tukio, na alipotafutwa alipatikana kuomba muda apige mwenyewe.

Golugwa akizungumzia hali ilivyokuwa, alidai Mwigamba alitoa mada kuhusu hali ya uhai wa chama katika mkoa wake ambapo aliwapongeza viongozi wakuu wa chama hicho.

“Lakini tunashangaa tukiwa bado hatujamaliza kikao, Mwigamba alituma taarifa za uzushi katika mtandao wa Jamii Forum na kwa kutumia wataalamu wa Chadema wa teknohama, walifuatilia nani aliyetuma wakafanikiwa kumbaini kuwa aliyefanya hivyo ni Mwigamba,” alidai.

Mwigamba pamoja na mambo mengine, anadaiwa kutoa taarifa katika mtandao huo kuwashutumu Mwenyekiti wa Taifa na maofisa wengine wa chama, kwamba wanatumia fedha nyingi kuzunguka na kufanya vitu ambavyo havieleweki.

Alidai baada ya kuelezwa alichokifanya, awali Mwigamba alibisha kwa kutoa maneno ya vitisho kwa Lema kwa maneno ya uchonganishi.

“Tulimwonea huruma tu Mwigamba alikuwa mtu mwenye sifa nzuri ndani ya chama na alikuwa anapambana haswa, lakini hatuwezi kubeba mizoga, amedanganywa na watu ambao hawaitakii mema nchi,” alidai.

Chanzo: Habari leo.
 
Ungekua na sifa hizo ungezamia mishikaki mondoli.Punguza uroho.Mwenyekiti mzima wa UVCCM mkoa unazamia mishikaki unaita ni mojawapo wa mbinu za kisiasa?Grow up!

Kamanda Ben kumbe huyu jamaa yako ndiye mwenyekiti wa UVCCM pande za home?
Basi huko UVCCM hakuna vijana Makini. Kwakuwa jamaa kila akigusa keyboard yani anatema pumba za hatari.
 
Jiulize kwanza walioondoka waliibua kashfa zipi?Lakini pia msisahau kuwa CHADEMA inaandamwa na kashfa za Ukanda na Ukabila huenda mnaoshinda humu katika mitandao ya kijamii hamlielewi hili lakini Watanzania wanafuatilia hatua kwa hatua.Kufukuzwa kwa Mwigamba CHADEMA kama wengi wenu mnavyodanganyana humu kutafuatiwa na serious consequences.Watanzania watajiuliza mbona ni wa huku tu na si wa kule ndio wanaoonekana hawafai.

Kwa taarifa yako wewe humu kwenye mtandao ndiye unayewaza ukanda na ukabila. Mwananchi kule mtaani siku ya kupiga kura akiwa kwenye foleni atakuwa anawaza kuwa ni mara ya 4 au 5 anaenda kutumbukiza karatasi kwenye lile sanduku. Alafu atawaza jinsi alivyoenda hospitalini akakosa kitanda, jinsi anavyoishi gizani kwa kukosa umeme, jinsi mwanae alivyoishia kuwa mmachinga kwa kufeli form four kwenye shule ya kata, jinsi mazao yake yalivyoharibiwa na mifugo baada ya viongozi wa wilaya kula mlungula wa wafugaji, jinsi asivyokuwa na uhakika wa kula chakula jioni hiyo kutokana na ukosefu wa mvua japokuwa mto mkubwa umepita km chache tu kutoka shambani kwake. Atakuwa anawaza huku akiwaona watoto wakicheza jirani huku wapo ------ wazi, atawaza jinsi mkewe alivyofariki akijifungua katika ile zahanati baada ya kukosa ambulance ya kumpeleka kwenye ile hospitali ya "misheni"... then atakuwa amefikia zamu yake ya kuweka tiki kwenye ile karatasi...
 
Jiulize kwanza walioondoka waliibua kashfa zipi?Lakini pia msisahau kuwa CHADEMA inaandamwa na kashfa za Ukanda na Ukabila huenda mnaoshinda humu katika mitandao ya kijamii hamlielewi hili lakini Watanzania wanafuatilia hatua kwa hatua.Kufukuzwa kwa Mwigamba CHADEMA kama wengi wenu mnavyodanganyana humu kutafuatiwa na serious consequences.Watanzania watajiuliza mbona ni wa huku tu na si wa kule ndio wanaoonekana hawafai?Labda wanataka kututumia tu kisha watugeuke huko mbele ya safari halafu waanze kupeana wao kwa wao.Tafakarini juu ya jili.Siasa ni mchezo unaohitaji kuchezwa kwa akili na umakini mkubwa sana.

Mwigamba yupi alifukuzwa CHADEMA jamaa? Umekula mchana?
 
Jiulize kwanza walioondoka waliibua kashfa zipi?Lakini pia msisahau kuwa CHADEMA inaandamwa na kashfa za Ukanda na Ukabila huenda mnaoshinda humu katika mitandao ya kijamii hamlielewi hili lakini Watanzania wanafuatilia hatua kwa hatua.Kufukuzwa kwa Mwigamba CHADEMA kama wengi wenu mnavyodanganyana humu kutafuatiwa na serious consequences.Watanzania watajiuliza mbona ni wa huku tu na si wa kule ndio wanaoonekana hawafai.
Huo ndiyo msingi wa Chadema ndiyo maana hawatathubutu kufanya uchaguzi.
 
Kamanda Ben kumbe huyu jamaa yako ndiye mwenyekiti wa UVCCM pande za home?
Basi huko UVCCM hakuna vijana Makini. Kwakuwa jamaa kila akigusa keyboard yani anatema pumba za hatari.
Unajipendekeza tu Nyie akina Mwita Maranya hamtakiwi Chadema wachie wa Moshi-Arusha.

Wamempiga wamempora simu zake na laptop pamoja na pesa.
Hivo hivo.......jeuri dawa yake kibiri. Na mm nasema apigwe tu kwani hawezi kufanya dhambi ikubwa namna ile kwa chama alafu aachwe hivihivi.....
 
Mkumbushe pia, Aige wenzake wanaojua mambo ya siasa vizuri!

Mkumbushe pia , Tabia zake/ kiherehere/ Sumu / Tindikali zina mwisho wake!

Mkumbushe pia aongeze ELIMU ya uraia na maarifa mengine ya Siasa.
Vyuo1.JPG
 
hivi huyu mwanzilishi wa huu uzi ashatuona vilaza,live update tokea saa 4 mpaka sasa?ni semina au?
 
John Mnyika anasema katiba ya 2004 inakipengele cha uongozi wa vipindi viwili wakati huo huo Dr.Slaa anasema ya 2004 haina kipengele hicho, Sasa kamanda WHO IS TELLING THE TRUTH KATI YA HAWA WAWILI????

Muongoo mnyika hakutoa tafsiri unayosema,ila sio mbaya umeipata tafsri unavyotaka iwe
 
Haijawa vipande vipande lakini chama kiko mapande mawili ndiyo maana karibu wote walionyanyasika ni wa kanda ya ziwa baadhi ni hao uliowataja hapo juu pamoja na Shibuda, Zitto, Kabouru, Wangwe, Mwigamba nk. lakini wa Moshi-Arusha wanakula kuku.

Vipi madiwani wanne wa Arusha akina Bayo?
Vipi Kisandu?
Vipi Mwampamba?
Vipi Shonza?
Vipi aliyekuwa mbunge wa Rombo 2005-2010 (CDM) Mh Salakana?

By the way, hawa watu wako wapi siku hizi?...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom