Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,355
Nimesikitishwa sana na haya yaliyotokea arusha naanza kupata mashaka kama ukombozi wa kweli tuliokuwa tunautafuta kupitia CDM utapatikana. Ninasema hivyo kwa kuwa kilichotokea arusha ni ishara mbaya kwa chama ambacho kimekuwa kipenzi cha watu wengi na sasa inaonekana dhahiri kuna vita ya madaraka imeanza ndani ya CDM. Pia hakuna kuaminiana tena huyu jamaa inadaiwa alipigwa kwa sababu ya kudaiwa kuwa anatumiwa na Zitto kukihujumu chama kwa mantiki hiyo wanachadema hawana imani na zitto ambaye ni mmoja wa viongozi wakuu wa chama na amekuwa ktk chama kwa muda mrefu. Nina dhani kwa mtazamo wangu CDM ingefocus kwenye kujenga chama wakati huu tunapokaribia uchaguzi mkuu wa 2015 na si kujikita kwenye malumbano ya kuwa fulani anahujumu chama kama ushahidi upo huyo anayehujumu chama aondolewe na chama kisonge mbele. Huku tuendako si kunzuri naanza kuiona CDM ikijijengea taswira mbaya machoni pa wananchi ambao tuliamini kuwa CDM ndiyo mkombozi wetu. Tunaanza kupata taswira ya tofauti kuwa si chama cha ukombozi tena wa tanzania bali ni kichaka cha kutafuta madaraka kwa maslahi binafsi kama ilivyo CCM.
Wenzako wapo field tangu asubuhi wanajenga chama mkuu. Wewe tu ndo una hofu. Usiogope uko chama kubwa. CDM ingekuwa inapuuzia watu kama hawa ungekuta kilishakuwa NCCR/TLP/CUF siku nyingi. Uzuri wa CDM wanamkunja samaki akiwa bado kifaranga, wanamsweka kwenye ndoo, safari inaendelea...