Chadema inakufa soon
Muajiri yupi mbona hajamtaja anataka kutupaisha,kila neno analotamka linafanyiwa kazi..Mkuu, Hujasoma vizuri: mwaka 2004 alikuwa akifundisha Mukidoma. mimi namfahamu huyu jamaa; 2011 hakuwa mukidoma! 1900k ilikuwa ni kutoka kwa mwajiri mwingine ambaye hakumtaja!
Kamanda Ben kumbe huyu jamaa yako ndiye mwenyekiti wa UVCCM pande za home?
Basi huko UVCCM hakuna vijana Makini. Kwakuwa jamaa kila akigusa keyboard yani anatema pumba za hatari.
Vipi madiwani wanne wa Arusha akina Bayo?
Vipi Kisandu?
Vipi Mwampamba?
Vipi Shonza?
Vipi aliyekuwa mbunge wa Rombo 2005-2010 (CDM) Mh Salakana?
By the way, hawa watu wako wapi siku hizi?...
Viongozi wa chadema kanda ya ziwa meshashtuka ndiyo maana wananyamazishwa na kupewa kibano. Mbeya-Iringa wanacheza ngoma wasiyoijua. Moshi-Arusha wanakula keki peke yako ukileta hoja hata kama ya msingi ni OUT.
Unajipendekeza tu Nyie akina Mwita Maranya hamtakiwi Chadema wachie wa Moshi-Arusha.
Mwigamba yupi alifukuzwa CHADEMA jamaa? Umekula mchana?
Nikiisoma hiyo press release yake naona kama vile anakili kufanya huo ujinga na anajutia.
Jiulize kwanza walioondoka waliibua kashfa zipi?Lakini pia msisahau kuwa CHADEMA inaandamwa na kashfa za Ukanda na Ukabila huenda mnaoshinda humu katika mitandao ya kijamii hamlielewi hili lakini Watanzania wanafuatilia hatua kwa hatua.Kufukuzwa kwa Mwigamba CHADEMA kama wengi wenu mnavyodanganyana humu kutafuatiwa na serious consequences.Watanzania watajiuliza mbona ni wa huku tu na si wa kule ndio wanaoonekana hawafai.
Democratization seems to be an impossible mission in Africa. Vyama vyenyewe ni very undemocratic hapo hapo vinadai ati kuleta na kutetea democracy.
mwanachama kwa kadi ipi? Nenda zako hata CCM kwani lazima CDM tu?
Atasema kuwa aliondolewa makao makuu kwa hila.
Atasema aliombwa kufanya kazi pale lakini mambo yakaenda ndivyo sivyo.
Atasema hakuna uhuru wa kutoa maoni. Atasema kuna ukabila na udini.
Atasema yeye ni msomi hawezi kutumika. Kisha atasema anaipenda Chadema na kambi ya upinzani na ni muumini wa mabadiliko.
Atasema anakusudia kukata rufaa. Atasema anaenda mahakamani.
Hakuna mapya!