Mkutano wa Mwigamba na vyombo vya habari

Mkutano wa Mwigamba na vyombo vya habari

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
Wakuu kama mnavyojua leo Mwigamba aliahidi kuzungumza na waandishi wa habari.... ... Nitakuwa nawaletea live kutoka eneo la tukio....... Niko hapa Premier Palace Hotel..... Mda wowote kuanzia sasa Mwigamba ataanza kuzungumza.....


Nawakilisha
====================

Mwingamba ndiyoanaingia..

Awali ya yote napenda kuongea na watanzania na wanaoipenda chadema wanaoipenda chadema na wenye imani na chadma wanao amini kuwa chadema ndiyo mkombozi wao, imani yao hiyo ni sahihi kabisa hata mimi ninaimani hiyo na wale wale wanoamini kuwa yaliyotokea juzi kuwa yataisambalatisha chadema wanakosea, chadema ni taasisi ambayo ni mjumuiko wa watu wengi wenye mitazamo tofauti, ndugu wana habari mimi ndiyo samson Mwigamba mwanachama wa chadema nilijiiunga nikiwa usa river 2004 nikifundisha ukidoma sec...machi 2012 nilichaguliwa kuwa kuwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha.Mabadiliko tunayo hitaji yatapatikana kupitia chadema kama wote mjuavyo ni kiongozi pekee niliye andika makala nyingi kuliko kiongozi yoyote pamoja na kutishiwa akiwemo katibu wa bunge na baadae kukamatwa na leo hii nina kesi mahakama ya kisutu, siyo hayo tu baada ya maandamano ya mwaka 2011 mwajiri wangu aliniambia nichague moja kazi au chadema nilichagua chadema bila kujali mshahara wa 1,900,000 niliokuwa nalipwa. nilifanya hivyo kwa mapenzi yangu niliyo nayo chadema na nina amini niko sahihi..

==============

Sasa Mwigamba anaelezea namna ilivyokuwa siku hiyo anasema Lema aliingia kwenye ukumbi akamkuta mwenyekiti akitoa speech lema akiw na IPAD mkononi akaa sehemu yake lakini baada ya muda akasimama na kumwambia mwenyekiti samahani kuna jambo la dharua.. lema akaanza kuelezea alichokiona kwenye mitandao, Selesini akanyosha mkono kumuomba lema asome kilicho bandiko husika. alipo maliza wakatoa pendekezo kuwa laptop ikabidhiwe meza kuu akiwa bado hajawaambia anakadhidhi ama laah lema alifika na kumnyakua ile laptop na kumwita mwenyekiti wa chadema mkoa wa manyara mabae ni mtaalamu wa IT akaiwasha wakagundua inapassword Mwigamba hakuona tatizo kutoa password akatoa wakaanza kulinganisha path na kujiridhisha kuwa ilitoka kwake basi ile laptop ikarudishwa meza kuu

=========================

Nasema hivi kiongozi aliemaliza muda wa uongozi anahaki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza mashariti katika cheo kimoja hii iko kwenye ibara moja ya toleo la 2004 mwaka 2006 tulifanya renovation mwaka huo huo tulikubaliana kubadilisha baadhi ya vipengele mimi nilikuwa katibu wa wilaya na hiki kipengele hatukiozungumzia juzi wakati napitia katiba nikitaka kujua kwanini mbowe na zitto wanagombana nikaona hiki kipengelee hakipo, nikasema kwanini hatukuambiwa wajumbe wakati kinaondolewa...MBOWE, ARFI - bara, MOHAMEDI ISSA - zanzibar, DR SLAA, Naibu katibu mkuu MOHAMEDI YUSUF- zanzibar, ZITTO –Bar hawa mimi ndiyo nawapinga kuendelea kugombea.....

Mwigamba: Sikupigana na Mbowe
CHADEMA yadai kompyuta yake ina siri zitakazogusa wengi

na Grace Macha, Arusha

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha ambaye amesimamishwa uongozi kwa tuhuma za usaliti, Samson Mwigamba, amesema kuwa hakupigana na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, kama ilivyodaiwa na baadhi ya magazeti.

Mwigamba alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kuelezea kile kilichojiri mwishoni mwa wiki hadi akapigwa na baadhi ya wajumbe wa kikao, wakimtuhumu kwamba aliandika taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums akizungumzia masuala ya uongozi ndani ya chama.

Mwigamba alisema kuwa hata wakati akivutana na walinzi wa chama Mbowe hakuwa ndani ya chumba cha mkutano, hivyo akadai kuwa anashangazwa na wale waliosambaza taarifa hizo kwamba alipigana na kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Aliwataja wale aliodai walimpiga kuwa ni Katibu wa Bavicha Wilaya ya Arusha, Noel OLovaroya, walinzi wa chama pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kwamba alijaribu bila mafanikio kumpiga na kitofali ambapo alikikwepa kwa kujiangusha chini na kujigonga kisogoni.

"Wakati vurugu zikianza Mbowe hakuwa ukumbini, nilimuona akija Lema na Olevaroya, ambapo Lema alishikwa kabla hajanifikia huku Olevaroya akiruka juu ya meza na kuja kunipiga ngumi, mimi kwa kujitetea ilibidi nimpige ngumi kabla hatujaamuliwa," alisema.

Mwigamba alimtuhumu Lema kuwa amekuwa akimtishia kumuua kwa kipindi kirefu, ambapo siku ya tukio alirudia kauli hiyo kabla hajaenda kuchukua kitofali na kujaribu kumpiga nacho ambapo alikikwepa.

Alisema kuwa tayari alishatoa taarifa polisi na kupewa kumbukumbu: AR/RB/1759/2013 aliyoifungua Februari 12, mwaka huu, baada ya kuwa anapokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa Lema kupitia simu yake ya kiganjani.

Kuhusu kusimamishwa uongozi, Mwigamba alisema kuwa ametii licha ya kuwa kikao kilichomsimamisha hakina mamlaka kisheria, huku akiweka wazi kuwa hayuko tayari kukihama chama hicho, kwani bado anaamini ndicho chenye uwezo wa kuleta mabadiliko nchini.

Hata hivyo, tuhuma za Mwigamba zilikanushwa na Katibu wa CHADEMA wa mkoa, Amani Golugwa, akisema ni uongo dhidi ya Lema, kwani kwenye taarifa yake aliyowasilisha juzi kwenye kikao cha uongozi wa kanda alimsifu mbunge huyo kwamba ameongoza harakati mbalimbali za ujenzi wa chama kwa mafanikio makubwa, zikiwamo kampeni za ushindi wa kata nne zilizofanya uchaguzi mdogo hivi karibuni.

"Kwa kipindi chote ambacho amekuwa hayuko kazini Lema amekuwa akimsaidia hata kukamilisha ujenzi wa nyumba yake maeneo ya Sokon 1, hata anavyokwenda kwenye kesi zake Dar es Salaam ni Lema amekuwa akimsaidia gharama.

"Hicho alichokizungumza kwenye mkutano wake juu ya malalamiko ndiyo anatudhihirishia kuwa amekuwa nyoka na mnafiki ndani ya kundi letu," alifafanua katibu huyo huku akisema hakuna malalamiko yoyote juu ya suala hilo ndani ya chama.

Golugwa aliongeza kuwa baada ya kupitia kompyuta ya Mwigamba wamebaini mambo mengi machafu na ya hatari kwa mustakabali wa chama ambayo yanawagusa watu wengi.

Hata hivyo hakutaka kuingia kwa undani wala kuyafafanua akisema yatakisaidia chama katika uchunguzi wake zaidi, na kwamba tayari kikao cha Baraza la mkoa kimeshakaa na kimemwandikia Mwigamba barua ya ajieleze ni kwa nini asivuliwe uongozi ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kulifikisha suala hilo mbele ya kikao cha Kamati Kuu ya Taifa.
 
Hana jipya zaidi atajikita kwenye kutafuta huruma yetu kwa visingizio vya kuonewa!
 
Pamoja wakuu.... Msijali .... Siwezi kupotea
 
Jamaa alipigwa sana na vijana wa Chadema.
 
Atasema kuwa aliondolewa makao makuu kwa hila.

Atasema aliombwa kufanya kazi pale lakini mambo yakaenda ndivyo sivyo.

Atasema hakuna uhuru wa kutoa maoni. Atasema kuna ukabila na udini.

Atasema yeye ni msomi hawezi kutumika. Kisha atasema anaipenda Chadema na kambi ya upinzani na ni muumini wa mabadiliko.

Atasema anakusudia kukata rufaa. Atasema anaenda mahakamani.

Hakuna mapya!
 
Saa nne na nusu mwigamba ataingia wakuu
 
Atasema kuwa aliondolewa makao makuu kwa hila.

Atasema aliombwa kufanya kazi pale lakini mambo yakaenda ndivyo sivyo.

Atasema hakuna uhuru wa kutoa maoni. Atasema kuna ukabila na udini.

Atasema yeye ni msomi hawezi kutumika. Kisha atasema anaipenda Chadema na kambi ya upinzani na ni muumini wa mabadiliko.

Atasema anakusudia kukata rufaa. Atasema anaenda mahakamani.

Hakuna mapya!
intelijensia, teh, teh
 
Wakuu kama mnavyojua leo Mwigamba aliahidi kuzungumza na waandishi wa habari.... ... Nitakuwa nawaletea live kutoka eneo la tukio....... Niko hapa Premier Palace Hotel..... Mda wowote kuanzia sasa Mwigamba ataanza kuzungumza.....

Nawakilisha

Tunasubiri akibwabwaja...
 
Atasema kuwa aliondolewa makao makuu kwa hila.

Atasema aliombwa kufanya kazi pale lakini mambo yakaenda ndivyo sivyo.

Atasema hakuna uhuru wa kutoa maoni. Atasema kuna ukabila na udini.

Atasema yeye ni msomi hawezi kutumika. Kisha atasema anaipenda Chadema na kambi ya upinzani na ni muumini wa mabadiliko.

Atasema anakusudia kukata rufaa. Atasema anaenda mahakamani.

Hakuna mapya!

Ndoto za kuwa mwenyekiti wa bavicha zinakufanya utumike sana
 
Back
Top Bottom