Lema: Mange ni 'Project' anataka kuigawa CHADEMA

Lema: Mange ni 'Project' anataka kuigawa CHADEMA

tucker carlson

Senior Member
Joined
Oct 5, 2025
Posts
182
Reaction score
762
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amemtuhumu mwanaharakati Mange Kimambi kuwa anatumika kuleta mgawanyiko ndani ya chama hicho, akipinga madai yanayotolewa dhidi yake kuwa yeye ni mradi wa kukigawa chama.

Lema amesema hayo leo Novemba 1, 2026 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha. Amesema anasikitishwa na baadhi ya wanachama wa CHADEMA wanaosikiliza kauli za Mange Kimambi na kuanza kugawanyika kwa misingi ya madai kuwa yeye ni mradi, akisisitiza kuwa madai hayo si ya kweli.

Ameeleza kuwa hawezi kuwa sehemu ya mpango wa kukigawa chama na uongozi wake, wakati yeye mwenyewe ni sehemu ya uongozi wa CHADEMA, akisisitiza kuwa hana nia ya kukidhoofisha chama hicho.

 
Kuna baadhi ya taarifa anapenyezewa Mange zikiwa na vimelea vya dola kuihujumu Chadema bila yeye kugundua kuwa anatumika. Hasa hili suala la Lemma na familia ya Lissu Mange alilishwa matango pori na akayafakamia hivyo hivyo.
 
Inawezekana Lema akawa sahihi, kama wanaharakati humshambulia wakikihusisha Chadema kwamba anataka kukigawa, basi sio vibaya nae akiwajibu kwa kuihusisha Chadema.

Binafsi sioni sababu Lema kuhangaika kuwajibu wanaharakati, wale wataongea kuwajibu ni kuwapaisha tu ikiwa wengine wao wamejipatia sifa kupitia mambo ya umbea, anachokifanya Lema ndicho wanachokipenda wataendeleza ligi.

Kama Lema anajiamini ni msafi awaachie hao wanaharakati kazi ya kuleta ushahidi kuonesha uchafu wake, asihangaike nao.

Kwa sasa arudi msibani.
 
Tatizo Chadema kumejazana Mayumbu nyumbu vichwani weupe
wenye kupenda umbeya kuliko ukweli

Pengine ndio nguvu ya umma yenyewe umbeya umbeya tu ✍️
 
Kweli kabisa. Mange Hana mamlaka ya kiuongozi, Sasa kauli za mange hazina binding powers kwa CHADEMA.
Hazina binding power lakini zinaheshimika,zinafanyiwa kazi na kukubalika..SIJUI KAMA ILI MNALIJUA
 
Bahati mbaya sana Mange alikuwa blackmailed nyakati fulani na mamlaka fulani ili kumfix mtu fulani.
Kwa sasa ni sehemu ya bargaining chip kwa watu walewale maana ndio pekee wanaweza kuhakikisha usalama wake amejikuta hana namna zaidi ya kufanya kazi yao.

Huwezi kuwa mwanaharakati ukiwa hauna mbinu zaidi ya kutegemea huruma ya adui yako, kuwatoa mhanga watu wako aka kusukuma boya baharini, kutegemea wakoloni wambane mbavu adui yako ilihali na wao focus number moja ni maslahi...kifupi ni harakati za kitoto zinazoweza kugharimu maisha ya watu wengi ( waliomo na wasiokuwemo).

Lema is one of the smart Gentleman aliyejichanganya awamu ya tano ya Ngosha na kupelekea naye kuwa blackmailed.

ndani ya viunga vya Hodeidah port - Yemeni
 
Mbona kma Lema Anastasia credibility yake kwa press hii bora angekubali ushauri alio ambiwa asifanye press
 
Mange ni mwanaharakati sio Kiongozi wa CHADEMA, anawezaje kukigawa chama. Mbona Lema ni kama anataka kukidharilisha chama?
Inashangaza kuona mjumbe wa kamati kuu ya chama anamlalamikia mwanaharakati ambaye siyo mwanachama wala kiongozi ndani ya chama.
 
Moja ya watu wasiokua na akili pale Chadema ni yule Hilda Newton
 
Back
Top Bottom