Mkutano wa Mwakyembe na Hoja za Mgongano wa Maslahi

Mgongano wa kimaslahi hapa ni baina ya watu ndani ya ccm, na kifupi ni mgongano wa maslahi kati ya ccm na public ya Watanzania, na si Mwakyembe vs public,na ndio maana hiyo definition ya conflict of interest haiwezi kuwa aaplied against Mwakyembe. Mpo?
 
Kwa Tanzania ya leo kama ni mpiganaji dhidi ya mambo yoyote mabaya, lazima uwe tayari kuishi kwa maadili maana vinginevyo utakuwa unawapa maadui zako silaha wakumalize. Dr. sio wa kwanza wala hatakuwa wa mwisho. Kama tulivyowajadili akina Mzee Warioba, Ballali, JK na wengine wengi, bado tutaendelea kukamata samaki mmoja mmoja.

Mtanzania unataka kumjadili nini Mwakyembe? Amevunja maadili gani?
 
wandugu,

..Dr.Mwakyembe aamue ama kuendelea na uwekezaji wake, au kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. natarajia kuona uamuzi huo ktk press release.
 
Rostam amekuwa anaandamwa na baadhi ya watu na Viongozi huyu jamaa hana makosa katika utendaji wake ni Baadhi ya viongozi na watu binafsi ambao wamekuwa wanafiki ndani ya serekali au CHAMANI , kama kweli jamaa amefanya makosa ndani ya serekali au chama hao viongozi au wananchi kinacho washinda nini wasimchukulie sheria zinazo stahiki jamani mwachie jamaa afanye kazi zake wacheni fitna zenu kama mmeshindwa nakupigania maendeleo na maishakaeni pembeni wenye uwezo wa kufanya hivyo wafanye wacheni hayo majungu na ubaya uliyomo ndani ya nafsi zenu kama kweli huyo Mwakyembe alimtaja Rostam katika hutuba yake na kusema aliyo yasema kuhusu Rostam inaonesha dhahiri amesha anza filisika na hofu imemuingia Mwakyembe ni mnafiki kama wanafiki wengine waliokuwemo ndani ya chama au serekali ROSTAM KAMATA KAMBA HIYO HIYO USIKUBALI KUYUMBISHWA NA TAKA TAKA HIZO
Oops....Here we go again!Kweli shibe mwana malevya,njaa.....
Nway,huenda sio kosa lako kutoyaona hayo yanayozungumzwa bout that Rostam,na jinsi yanavyokuwa validated.
 
Wakuu, heshima zote... mi naona kama tunazunguka sana, lakini mpaka sasa hivi sijaelewa CONFLICT OF INTEREST ya Mwakyembe iko wapi.

Naomba mkuu Mtanzania unifafanulie maana inawezekana sijaelewa. Ninachoona ni kwamba baadhi ya wachangiaji wanajaribu ku-prove kwamba alianzisha kampuni hii ya uzalishaji wa umeme, na bado anaendelea kumiliki hisa.

Whether it is true or not mi naona hii siyo point, yeye ana haki ya kuwa na biashara na hata kimaadili sioni tatizo lolote kwani hajachukua mkopo, hakucheza upatu etc. Ni investment halali iliyofuata sheria zote za nchi.
Uzalishaji wa kampuni yake haijaanza na hajaenda serikalini kuomba kwamba apewe mkopo au advance au mitambo yake inunuliwe(kama Richmond na Dowans). Hivyo hatuwezi kuzungumzia ufisadi hapa.
So what is the point ya kutaka kujua eti ana hisa au hana?

Narudia tena UFISADI sio sawa na UWEKEZAJI. Chonde chonde watanzania tusije tukaanza kutumia neno hili kama tulivyofanya kwa wanyonyaji na walanguzi na kujikuta tunafanya upuuzi wa enzi za Nyerere za kumfunga mtu kwa kumiliki tube 2 za Colgate! Free entreprise ndo jibu pekee siyo ujamaa na ukomunisti!

Dr Mwakyembe has nothing to apologize for - for trying to invest in something that he believes in!!!

Hata mimi ni Mtanzania hivyo ngoja nikueleweshe pia japo hutaki kuelewa.

Nikiwa nina duka la dawa linalouza dawa za kutibu magonjwa nyemelezi na nina mpango wa kujadiliana na Muhimbili kuhusu zabuni ya kuwauzia dawa na wewe ukiwa na duka la kuuza madawa ya kurefusha maisha na ulipata zabuni ya kuizua Muhimbili katika mazingira tata basi maslahi yangu ni kuuza dawa na maslahi yako ni kuuza dawa kwa mteja mmoja. Hivyo, siwezi kukuchunguza wewe maana maslahi yetu ni ya aina moja - kuuza dawa. Maana nikikuchunguza huenda nikakuharibia ili na mimi siku moja nimuuzie Muhimbili madawa kama unayomuuzia wewe hasa ukizingatia tuko kwenye sekta mmoja na nina uwezo wa kuuza dawa kama zako pia maana MEMART inaruhusu.

Kwa ufupi, chungwa na embe yote ni matunda - hayawezi kuchunguzana kwa haki; nyani na ngedere wote ni wadau wa kula matunda - hawawezi kuchunguzana bila kuzua hisia za uonevu kwa mmoja wao hivyo wa kumchunguza mmojawao ni sungura au mnyama mwingine. Mgongano wa kimaslahi ni kitu cha wazi kabisa kwa mtu yoyote anayejali maadili na haki.
 
Zitto kama Dk. Kabourou!!!!! Mungu wangu tumekwisha

Yeye anakwambia “Sakata la Dowans, zitto kama Obama”

Nimeumia kuona kijana mwenzetu anajiunga na Rostamania Fisadism College na anahitimu kwa muda mfupi kiasi hiki! Within few weeks tayari anaweza kujiandikia praising articles na kujifananisha na Obama! Rejea Tanzania Daima ya leo pg12-13
 
Mimi nadhani kuna kitu zaidi ya hayo maslahi binafsi. Kwa mazingira ya Tz suala la conflict of interest liko sana (ingawa hiyo haitoa fursa mtu kutenda makosa au kuhalalisha makosa). Kama kweli Mwakyembe analo kosa la namna hiyo, je kwa sasa huyu bwana kafisadi amana zetu? Kama na yeye ni fisadi basi wote manzi ga nyanza (kama alivyowahi kusema Nyerere) i.e wote watoswe. Ila kama yeye siyo fisadi lakini pia si mkweli basi tumpe hukumu yake ili twende mbele. Naona tutachelewa hapa kujadili hili suala suala hili wakati huo tunawapa nafasi mafisadi kulegeza kitanzi. Ndege akituponyoka tutamlaumu nani? Sidhani kama huu ni muda muafaka kutumia muda mwingi kujadili contextual issues badala ya kuwabana mashetani waliokula pesa zetu zaidi ya 1bn, na bado wanataka kukomba nyingine.
 
Wakuu, heshima zote... mi naona kama tunazunguka sana, lakini mpaka sasa hivi sijaelewa CONFLICT OF INTEREST ya Mwakyembe iko wapi.
Naomba mkuu Mtanzania unifafanulie maana inawezekana sijaelewa. Ninachoona ni kwamba baadhi ya wachangiaji wanajaribu ku-prove kwamba alianzisha kampuni hii ya uzalishaji wa umeme, na bado anaendelea kumiliki hisa.
Whether it is true or not mi naona hii siyo point, yeye ana haki ya kuwa na biashara na hata kimaadili sioni tatizo lolote kwani hajachukua mkopo, hakucheza upatu etc. Ni investment halali iliyofuata sheria zote za nchi.
Uzalishaji wa kampuni yake haijaanza na hajaenda serikalini kuomba kwamba apewe mkopo au advance au mitambo yake inunuliwe(kama Richmond na Dowans). Hivyo hatuwezi kuzungumzia ufisadi hapa.
So what is the point ya kutaka kujua eti ana hisa au hana?

Narudia tena UFISADI sio sawa na UWEKEZAJI. Chonde chonde watanzania tusije tukaanza kutumia neno hili kama tulivyofanya kwa wanyonyaji na walanguzi na kujikuta tunafanya upuuzi wa enzi za Nyerere za kumfunga mtu kwa kumiliki tube 2 za Colgate! Free entreprise ndo jibu pekee siyo ujamaa na ukomunisti!

Dr Mwakyembe has nothing to apologize for - for trying to invest in something that he believes in!!!

Susuviri,

Sidhani kama huu mjadala ni kuhusu Dr. Mwakyembe kuwa fisadi. Kama kuna watu wamesema hivyo ni wachache sana.

Pia sioni kosa kwa Dr. kuwa na kampuni yake, sheria zetu na sheria karibu za dunia nzima zinaruhusu.

Kosa ambalo wengine tunaliona ni kwamba kwa yeye kushiriki kwenye ile kamati muhimu sana ya kuchunguza matatizo ya mkataba wa Richmond na Tanasco, alitakiwa aweke wazi kwamba hata yeye anamiliki kampuni ya kufua umeme hata kama haijaanza.

Kama hujui, through ile kamati Dr. alikuwa na nafasi za kuangalia habari zote nyeti za Tanesco na nishati kwa ujumla. Sasa hapo ni tatizo.

Hata ukisoma utangulizi wa ile report, ni pamoja na kuwashukuru baadhi ya watu wakiwemo
hao ambao yuko nao kwenye hiyo kampuni. Sasa hapo mtu anajiuliza ni kweli walisaidia au ndio njia ya kubebana. Lakini angeweka kila kitu toka mwanzoni, haya maswali yanakuwa hayana nguvu tena.

Mimi naona ambacho alitakiwa kufanya ni kumjulisha Spika juu ya ushiriki wake kwenye sector ya nishati na kama wangeona kila kitu kiko OK, hapo angeweza kuendelea na hiyo kamati na ingelikuwa fair hata kwa wale ambao walikuwa wanatuhumiwa na hiyo kamati.

Je hii habari inapunguza kazi nzuri ya Dr kwenye uchunguzi wa Richmond, mimi naamini hapana, ingawaje kama Dowans au Richmond wataenda mahakamani, wanaweza kutumia hii kama sababu moja wapo ya kwamba hawakutendewa haki. Na kwa case inayofanyika Paris, huku nje kila mtu anajua jinsi walivyo serious na haya mambo ya conflict of interest.

Kwa wengine huu ndio mjadala tunaojadili.
 
wandugu,

..Dr.Mwakyembe aamue ama kuendelea na uwekezaji wake, au kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. natarajia kuona uamuzi huo ktk press release.

Hoja nzuri lakini mbona ameshasema kuwa hayumo tena kwenye hiyo kampuni?

Ila kwa hoja yako, inabidi kuanzia sasa viongozi wote wenye nyadhifa zenye conflict na biashara zao, wang'atuke.
 
Mtu aliyemshauri Dr. Mwakyembe katika hili suala , nasikitika kusema ya kuwa hakumshauri vizuri . Kuzungumzia kuhusu Rostam badala ya kujikita kwenye ishu mama ni kosa kubwa, Rostam huko halipo anacheka kwani sasa amejiingiza kwenye mtego.

Pili, Mimi napenda kuwashauri wanajf wenzangu tusi-invest sana kwa wanasiasa bali tusimamie sheria na kanuni za nchi . Wanasiasa hawa ni wanadamu tuu, kama Mwakyembe alivyosema "SINA MKATABA NA BUNGE." Statement hiyo ni kubwa sana na zaidi speaks for itself !
 
Mimi nadhani kuna kitu zaidi ya hayo maslahi binafsi. Kwa mazingira ya Tz suala la conflict of interest liko sana (ingawa hiyo haitoa fursa mtu kutenda makosa au kuhalalisha makosa).

Kosa lake kubwa ni kuimaliza hoja ya Tanesco ya kununua Generator na madeni ya Dowans. Full Stop.

Spika ana bahati kuwa Dr. Mwakyembe ndiye kafara wa msimu huu, sio ajabu RA anamchimba na Spika ili naye amtoe kwenye vigazeti vyake ASAP.
 
Hoja nzuri lakini mbona ameshasema kuwa hayumo tena kwenye hiyo kampuni?

Ila kwa hoja yako, inabidi kuanzia sasa viongozi wote wenye nyadhifa zenye conflict na biashara zao, wang'atuke.

Hapo umenena. Naamini itakuwa patashika ndani ya CCM. Kwanza JK ameshindwa kabisa na hoja yake ya biashara au siasa. Na BWM itakuwaje? Alianzisha kampuni akiwa Ikulu na akununua mali ya umma pale Kiwira.
 
Nataka nisikie kauli za hao wanaowapenda sana watanzania na kuwaonea huruma dhidi ya Mwakyembe...Hatuwezi kujidai eti tunajiweka kwenye standards ambazo hata chembe hatuna...Bottomline maslahi ya wananchi ndiyo yazingatiwe na si vijisheria vya kibepari vinavyopigiwa debe mitandaoni na watu wanaojidai wanataka perfectionism ya utawala wa kisheria na kusahahu reality kwamba sheria zetu ni more than mbovu. Na ndio maana nikasema toka awali kuwa Mwakyembe will prevail...Kuwa ndani ya system na kuwa mzalendo at the same time ni ngumu chini ya current political status.
Mwalimu aliwahi kusema "I cant let my country go to the dogs" Alijuwa kabisa si sahihi kuletwa mizengwe,njia sahihi ni kuachia demokrasia itake its course,lakini aliona loophole na akajuwa ni muhimu kusimamia hata kama kutakuwa na malalamio ya mizengwe,kutaka Mwakyembe ashindwe dhidi ya Dowans kwa kigezo weak cha conflict of interest hakuna tofauti na ku let the country completely go to the dogs....
 
wandugu,

..Dr.Mwakyembe aamue ama kuendelea na uwekezaji wake, au kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. natarajia kuona uamuzi huo ktk press release.

Joka kuu,

Dr Mwakyembe ni MJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI? Hizi habari ni za kweli?
 
Makaayamawe said:
Hoja nzuri lakini mbona ameshasema kuwa hayumo tena kwenye hiyo kampuni?

Ila kwa hoja yako, inabidi kuanzia sasa viongozi wote wenye nyadhifa zenye conflict na biashara zao, wang'atuke.

Makaayamawe,

..inabidi ipatikane taarifa rasmi inayoelekeza hivyo.

..hawa wanaodai walikuwepo kwenye hiyo press conference wanatuchanganya tu.

..pia tukishapata kauli yake kwamba amejitoa, itabidi tukajiridhishe kwa kuangalia nyaraka zilizoko kwa msajili wa makampuni.

..viongozi wakiamua kufanya biashara wawe waungwana kwa kufanya zile biashara zisizo na mahusiano ya moja kwa moja na sekta wanazoziongoza.
 
Mkuu,

Hiyo kampuni ni NGO? Utasemaje a private company haina maslahi ya kifedha? Kwanini unaanzisha a private company kama sio kupata faida?

Naona hiyo argument ni very weak!

I wish you were there. Dk. Mwakyembe kajieleza vizuri kinyume cha wengi tulivyofikiria. Waliopwaya ni waandishi kuuliza feeble questions na kushindwa kumbana kwenye masuala ya msingi ingawa vilevile jamaa alikuwa kajiandaa barabara.
 
Kwanini uchaguzi huo apewe Mwakyembe peke yake?

MKJJ mabadiliko yanatakiwa yaanzie kwenye fikra za wadanganyika,maybe hizi mbegu zitasaidia kwa next generation lakini si the current one, kwasababu nashangazwa sana na uelewa wa watanzania walio wengi,kuna watu wamejiuzia rasilimali za Taifa mfano Kiwira,lakini watu wala hawataki kuona haki ikitendeka badala yake wanasahau mapema mno...Kwa hivyo lile jalala ulilodai Taifa limepiga kambi itakuwa vigumu sana kutoka hapo maana ni ama fasheni,watu kupendelea harufu mbaya mbaya na pia kukoga na maji taka.
 
Next Level said:
Joka kuu,

Dr Mwakyembe ni MJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI? Hizi habari ni za kweli?

Next Level,

..kulingana na taarifa zilizoko ktk website ya Bunge la Tanzania Dr.Harrison Mwakyembe ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

..actually binafsi nina matatizo zaidi na Victor Mwambalaswa ambaye ni mjumbe wa kamati ya bunge, mjumbe wa board ya Tanesco, na mwanahisa ktk kampuni ya Mwakyembe.
 
Back
Top Bottom