Salma Kikwete ni Mwanamke wa Shoka, Mke, Mama, na Kiongozi. Ashusha hoja 10 za nguvu, aanza na Samia na kumaliza na Samia!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala hizi, "Kwa Maslahi ya Taifa" kuzungumzia jambo lolote lenye maslahi kwa taifa letu liwe ni jambo la kisiasa, kiuchumi au kijamii.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastori stori yaani story teller, naomba nianze kwa mastory ya ilikuwaje nikaibukia Burundi na kwa wasiopenda mastori, una weza ku jump kwenye mada kuu ya uzi huu.

Nianze tuu kwa kukumbushana, baada ya kushauriwa na kiongozi wetu mmoja fulani kuwa tuhamie Burundi, sisi wengine wenu, kwa hiyari yetu, tumehamia Burundi, sasa niko naishi jijini Bujumbura.

Kitu muhimu sana kwa Watanzania wenzetu muwapo ugenini, kitu cha kwanza ni kuutafuta ubalozi wetu wa nchi hiyo na kujitambulisha ubalozini, kuwa wewe ni Mtanzania, umekuja nchi hiyo kufanya nini, umefikia wapi na unapatikanaje, in terms of contacts, kisha unaendelea na mihanjo yako nchi za watu. Hivi ndivyo siku zote ninavyofanya kila niwapo safarini nchi za watu baada ya kukumbwa na kisa fulani nchini Italy, enzi za kutafuta maisha.

Hivyo baada ya kiongozi wetu fulani kutushauri tuhamie Burundi, mimi kweli nikahamia Burundi jiji la Bujumbura, na kujitambulisha ubalozini na tulipokelewa vizuri.

Faida za Mtanzania kujitambulisha ubalozini kwako uwapo ugenini ni nyingi lakini moja kubwa ni jina lako kuingizwa kwenye kanzi data (data base) ya Watanzania waishio nchi hiyo, kukitokea social events za Watanzania, unaalikwa mnakutana na ku socialize.

Umuhimu wa pekee wa kujitambulisha uwepo wako mahali fulani ni just in case of something, anything can happen to anybody anywhere, hapa ndipo utajua umuhimu wa kujitambulisha ubalozini.

Hivyo nikiwa jijini Bujumbura, nikajulishwa ujio wa kiongozi wetu huyu Tulioitika Wito Kuhamia Burundi, Tumefarijika Sana Kumuona Former First Lady, Mama Salma Kikwete. Kumbe Rais Akiwa Mwanamke, Nchi Haina First Lady!

Kwenye kada ya waandishi wa habari, tuko waandishi wa aina nyingi, kuna waandishi wa habari, watangazaji, ma presenter, ma producer, maripota, na kundi kundi ndogo la waandishi wahojaji, hawa kazi yao sio kuripoti bali kuhoji, hawa kwenye zile TV kubwa kubwa wanaitwa "anchorman" na wengi ni ma talk show hosts ambao kikawaida kwenye vituo vya Radio na TV hawa watu ndio wanapaswa kuwa top paid!. Kundi hili ndio wamo watu kama Larry King, Riz Khan, Christine Amampour, Tim Sebastia
Shaka Ssali, Jeff Koinage, na hapa bongo japo wengi hawakubali, lakini kwenye TV zetu za Bongo, kiongozi wao ni mimi na kipindi cha Mada Moto, ndio TV Talk Show ya kwanza Tanzania, kisha ikaja Kiti Moto, ndipo zikafuatia nyingine nyingine.

Siku hizi karibu kila TV, kila Redio zina Talk Shows na sasa watangazaji ma star wa talk shows wako kibao!, wengi ni watoto wa juzi, hawawezi kutujua wazee kama akina sisi!.

Waandishi maripota wakifika kwenye tukio kazi yao ni kuripoti tuu kile kinachotokea, kama ni press conference au mkutano ni kuripoti hotuba na kuondoka na press release speech etc

Waandishi wahojaji, huwa hawaridhiki na walichoitiwa tuu bali hupenda kufanya mahojiano ya ana kwa ana, uso kwa uso, one on one
Mjue Mhe. Salma Kikwete kwa karibu zaidi na kwa undani zaidi, Mhe. Salma Kikwete, kwanza ni mwanamke, ili sio mwanamke tuu kama mwanamke wa kawaida, bali ni mwanamke wa shoka haswa!, ni mke kwa mumewe, Dr. Jakaya Kikwete, ni mama wa familia yake, ni pia ni former 1st Lady na ni Mkurugenzi wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo Wama, na kwa sasa ni mwanasiasa na mbunge wa jimbo la Nchinga akiwa ni mmoja wa wanawake wachache wa shoka ambao ni majembe ya ukweli kwa kuwa mbunge wa jimbo.

Zijue hoja zake 10 alizozishusha kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Viongozi Wanawake wa Afrika ambao ni wake wa viongozi wakuu wa Afrika uliofanyika jijini Bujumbura Burundi hivi karibuni

Kwenye hoja zake 10, Mama Salma Kikwete alianza na Rais Samia na kumaliza na Rais Samia. Andamama nami kwenye makala hii, sio tuu kuzijua hoja zake bali pia kuzisikia kwa masikio yako mwenyewe kwa kumsikiliza huku ukimtazama na kumshuhudia kwa macho yako mwenyewe ila hapa ni kwa wenye bundle
  1. Salaam za toka kwa Rais Samia kwa mkutano huo
  2. Salma Kikwete auzungumzia umuhimu wa mkutano huo, huku akionyesha heshima ya mke mwema kuomba ruhusa kwa mumewe kabla ya kusafiri kwenda popote hata kwa safari za kikazi
  3. Awaasa wanawake wote hata walio olewa, wasiishie tuu kuwa wake wema ndani ya familia zao, au wamama wema kwenye kulea familia, bali wawe chachu ya maendeleo kwa kujishughulisha na shughuli nyingine zozote za kiuchumi kusupport familia. Huu ni ujumbe kwa wanawake walio olewa wasiishie kuwa ma 'golikipa'
  4. Salma Kikwete aitangaza vema Tanzania na mambo mazuri yetu, nje ya mipaka yetu hivyo kuendelea kuifanya Tanzania kuwa ni nchi ya kupigiwa mfano barani Afrika, kama mwanzo Tanzania tulivyoitwa Kisiwa cha Amani kutokana na juhudi mbalimbali za Tanzania kuleta amani eneo la Maziwa Makuu, sasa Tanzania inakwenda kuwa kitovu cha maendeleo ya ukanda huu.
  5. Salma Kikwete ainadi Tanzania kuwa nchi "shamba darasa" la kutetea haki elimu kwa mtoto wa kike
  6. Salma Kikwete Awaasa Viongozi Wanawake, Uongozi Usiwafanye ku abandon the traditional role ya mwanamke kwenye familia kuwa mke mwema na mama bora wa kulea familia.
  7. Salma Kikwete asisitiza ushirikiano baina ya wenza na kusisitiza umuhimu wa wenza kushikoshana kwenye kila jambo kwa Waume kuwashirikisha wake zao kwenye mambo yao, na wanawake kuwashirikisha waume zao kwenye mambo yao, na kujitolea mfano wa yeye na Jakaya.
  8. Salma Kikwete asisitiza umuhimu wa familia kujipangia utaratibu wa maisha na kuishi kwa kuufuata utaratibu waliojipangia ndio maisha!.
  9. Salma Kikwete apiga ukungwi wa maisha ya ndoa "akili ni nywele kila mtu ana zake" na "maisha ya ndoa, hayana shule"
  10. Salma Kikwete asisitiza suala la maadili, kwa watoto na vijana, ampongeza Rais Samia anavyosisitiza maadili kwa viongozi

Hii hoja ya 11 ni ya ziada, baada ya mahojiano na hizo hoja 10, nikamuuliza kama ana la kuongezo, ndipo akashuka na hoja kubwa zaidi na muhimu zaidi kuliko zote!, ni hoja ya upendo kwa majirani, mpende jirani yako kama ndugu yako.
Hoja hizi 10 za Mama Salma Kikwete, zimekuwa documented kwenye kipindi maalum cha TV, ambacho kitakujia hivi karibuni na kutangazwa kwenye vituo 6 vya TV, ITV, TBC, Star TV, Channel Ten, Clouds TV na Azam TV.

Ukiwa karibu na waridi lazima unukie!, mtu kukaa bennet na rais wa nchi kwa miaka 10, unakuwa na presidential qualities, ambazo unazipata kwa assimilation, mtu kama huyu akiwa groomed kidogo tuu, Tanzania tunaweza kujikuta tunampata Hilary Clinton wetu in near future!.

Nawatakia utazamaji mwema wa hoja hizi.

Natanguliza Shukrani

Paskali.
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala hizi, "Kwa Maslahi ya Taifa" kuzungumzia jambo lolote lenye maslahi kwa taifa letu liwe ni jambo la kisiasa, kiuchumi au kijamii.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastori stori yaani story teller, naomba nianze kwa mastory ya ilikuwaje nikaibukia Burundi na kwa wasiopenda mastori, una weza ku jump kwenye mada kuu ya uzi huu.

Mjue Mhe. Salma Kikwete kwa karibu zaidi, Salma Kikwete ni kwanza ni mwanamke, sio mwanamke tuu, bali ni mwanamke wa shoka!, ni mke kwa mumewe, Dr. Jakaya Kikwete, ni mama wa familia yake, ni mwanasiasa na kiongozi wa jimbo la Nchinga, ni former 1st Lady na Mkurugenzi wa Wama. Zijue hoja zake 10 alizozishusha kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Viongozi Wanawake wa Afrika ambao ni wake wa viongozi wakuu wa Afrika uliofanyika jijini Bujumbura Burundi hivi karibuni

Kwenye hoja zake 10, Mama Salma Kikwete alianza na Rais Samia na kumaliza na Rais Samia. Andamama nami kwenye makala hii, sio tuu kuzijua hoja zake bali pia kuzisikia kwa masikio yako mwenyewe kwa kumsikiliza huku ukimtazama na kumshuhudia kwa macho yako mwenyewe ila hapa ni kwa wenye bundle

Hii hoja ya 11 ni ya ziada, baada ya mahojiano na hizo hoja 10, nikamuuliza kama ana la kuongezo, ndipo akashuka na hoja kubwa zaidi na muhimu zaidi kuliko zote!, ni hoja ya upendo kwa majirani, mpende jirani yako kama ndugu yako.
Hoja hizi 10 za Mama Salma Kikwete, zimekuwa documented kwenye kipindi maalum cha TV, ambacho kitakujia hivi karibuni na kutangazwa kwenye vituo 6 vya TV, ITV, TBC, Star TV, Channel Ten, Clouds TV na Azam TV.

Ukiwa karibu na waridi lazima unukie!, mtu kukaa bennet na rais wa nchi kwa miaka 10, unakuwa na presidential qualities, ambazo unazipata kwa assimilation, mtu kama huyu akiwa groomed kidogo tuu, Tanzania tunaweza kujikuta tunampata Hilary Clinton wetu in near future!.

Nawatakia utazamaji mwema wa hoja hizi.

Natanguliza Shukrani

Paskali.

Amekulipa shs ngapi kumpromote?
 
Amekulipa shs ngapi kumpromote?
Mkuu Bejamini Netanyahu , kwanza uwe na heshima, heshima kitu cha bure, huyu ni mke wa rais, ni Mhe. Mbunge, anahitaji promo yq nini?!.
Pili, tuko wote humu kwa zaidi ya miaka 8, mpaka leo bado tuu hatufahamiani vilivyo?!. Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, nafanya kazi bure kwa kujitolea silipwi na mtu yeyote.
P
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala hizi, "Kwa Maslahi ya Taifa" kuzungumzia jambo lolote lenye maslahi kwa taifa letu liwe ni jambo la kisiasa, kiuchumi au kijamii.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastori stori yaani story teller, naomba nianze kwa mastory ya ilikuwaje nikaibukia Burundi na kwa wasiopenda mastori, una weza ku jump kwenye mada kuu ya uzi huu.

Mjue Mhe. Salma Kikwete kwa karibu zaidi na kwa undani zaidi, Mhe. Salma Kikwete, kwanza ni mwanamke, ili sio mwanamke tuu kama mwanamke wa kawaida, bali ni mwanamke wa shoka haswa!, ni mke kwa mumewe, Dr. Jakaya Kikwete, ni mama wa familia yake, ni pia ni former 1st Lady na ni Mkurugenzi wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo Wama, na kwa sasa ni mwanasiasa na mbunge wa jimbo la Nchinga akiwa ni mmoja wa wanawake wachache wa shoka ambao ni majembe ya ukweli kwa kuwa mbunge wa jimbo.

Zijue hoja zake 10 alizozishusha kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Viongozi Wanawake wa Afrika ambao ni wake wa viongozi wakuu wa Afrika uliofanyika jijini Bujumbura Burundi hivi karibuni

Kwenye hoja zake 10, Mama Salma Kikwete alianza na Rais Samia na kumaliza na Rais Samia. Andamama nami kwenye makala hii, sio tuu kuzijua hoja zake bali pia kuzisikia kwa masikio yako mwenyewe kwa kumsikiliza huku ukimtazama na kumshuhudia kwa macho yako mwenyewe ila hapa ni kwa wenye bundle

Hii hoja ya 11 ni ya ziada, baada ya mahojiano na hizo hoja 10, nikamuuliza kama ana la kuongezo, ndipo akashuka na hoja kubwa zaidi na muhimu zaidi kuliko zote!, ni hoja ya upendo kwa majirani, mpende jirani yako kama ndugu yako.
Hoja hizi 10 za Mama Salma Kikwete, zimekuwa documented kwenye kipindi maalum cha TV, ambacho kitakujia hivi karibuni na kutangazwa kwenye vituo 6 vya TV, ITV, TBC, Star TV, Channel Ten, Clouds TV na Azam TV.

Ukiwa karibu na waridi lazima unukie!, mtu kukaa bennet na rais wa nchi kwa miaka 10, unakuwa na presidential qualities, ambazo unazipata kwa assimilation, mtu kama huyu akiwa groomed kidogo tuu, Tanzania tunaweza kujikuta tunampata Hilary Clinton wetu in near future!.

Nawatakia utazamaji mwema wa hoja hizi.

Natanguliza Shukrani

Paskali.

Umefanya kazi ambayo hujatumwa......
 
Umefanya kazi ambayo hujatumwa......
Mkuu airmax , kwanza karibu jf, kufuatia ugeni wako humu, na wewe kuwa ni mtumwa hivyo unadhani kila mtu ni mtumwa!, baadhi yetu humu sio watumwa, na mimi siku zote mimi sio mtumwa, huwa situmwi hivyo ni kawaida yangu kufanya kazi bila kutumwa, hivyo hongera, umepatia sana!.
P
 
Back
Top Bottom