Utafiti kuhusu migogoro ya viongozi wa halmashauri na mgongano wa madaraka unaosababisha kushuka kwa shughuli za maendeleo

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,580
17,685
1.Summary

Katika ngazi ya wilaya, kuna viongozi wanne wazito. Mkuu wa wilaya, mkurugenzi na mwenyekiti wa halmashauri na Mbunge. Na mara nyingi Kumekuwa na Mikanganyiko ya kutofautisha nafasi hizi na umuhimu wa kila mmoja katika nafasi yake.

Daima swali linakuwa ni nani kati yao mwenye mamlaka makubwa na nani anawajibika kwa nani? Je, hawa wanafanya kazi vipi bila migongano? Je, hawa wanaimarisha serikali za mitaa? Je, wananchi wanafahamu tofauti na umuhimu wa kila mmoja? Je, wao wanafahamu nafasi zao na wajibu zao bila kuingilia mwingine?

2.Tatizo Liko Hapa

Kumekuwa na Migongani mingi sana ya kimajukumu au ya kikazi kati ya viongozi hao ,Tumeona wakuu wa wilaya wengi (sitawataja japo Migongano yao mingi imeonekana mitandaoni) Na hadharani waziri mkuu akiwa"Demote" wakurugenzi kwa kutowajibika ipasavyo na ambao Wamekuwa migongano wao kwa wao Kuwaonya ili wasifanye hivyo.

Tutapitia majukumu yao mmoja mmoja tuone shida iko wapi

A.MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI

Kwa mujibu wa Katiba ibara ya 146 (1) na (2)
“Madhumuni ya kuwapo serikali ya Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi.Na vyombo vya serikali za Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikisha wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo..........."

Majukumu na kazi za Mkurugenzi zimegawanyika katika makundi makuu manne:-kisheria, kiutawala, kifedha na ni katibu.

1.Majukumu na kazi za kisheria

(i)Ni Msimamizi na mlinzi wa usalama na amani katika eneo la Mamlaka ya Halmashauri Anao uwezo wa kumuweka mtu Ndani na kuondoa haki yake ya dhamana lakini isizidi siku 28. Na pia kumkamata mtu yoyote bila hati ya kukamata kama atavunja sheria ndogo za Halmashauri.

Na pia ana uwezo wa kumuita mtu yoyote aliye chini ya halmashauri yake kwa mahojiano hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 51(1) na (4) cha Sheria ya Mahakama za mahakimu Na. 2 ya 1984 ,Pia soma Kifungu cha 177(1) cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288.

(ii) Mkurugenzi anatakiwa chini ya Sheria ya Uthamini wa Mali zilizoko Mjini (Urban Authorities Rating Act) ya mwaka 1983 iwapo mwenye mali akikataa kulipa kodi anayodaiwa katika muda wa siku kumi na nne, kutoa waranti kwa “Court Broker” akimtaka akamate mali binafsi za huyo mhusika zenye thamani ya kodi anayodaiwa.

Japo Kifungu hiki cha sheria kimepunguzwa nguvu baada ya serikali kuu kuamua kukusanya kodi ,ushuru na tozo mbalimbali kwenye Halimashauri kwa kutumia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mwaka 2016.

(iii) Mkurugenzi Ndiye mtia saini nyaraka mbalimbali za Halmashauri,mikataba,na miradi mbalimbali ya maji afya na barabara na pia mikataba yote ikiwemo ya wafanyakazi wa Halmashauri chini ya Kifungu cha 200 Sura 287 na kifungu 117 cha Sura 288.

2.Majukumu na kazi za kiutawala

(i)Mkurugenzi wa Halimashauri ana wajibu wa Kupokea na kusikiliza matatizo ,changamoto na au malalamiko ya wananchi kwenye Halmashauri husika na anawajibu wa kuzitafutia majibu ya kina changamoto hizo ama kwa kufanya moja kwa moja au kwa kuwaagiza wasaidizi wake.

(ii) Mkurugenzi ana wajibu wa Kuwa Afisa Uhusiano na Msemaji Mkuu wa maamuzi ya Halmashauri, yaani Mkurugenzi ndiye msemaji Mkuu wa maamuzi na maazimio ya Halmashauri na iwapo atapotosha maazimio hayo ni yeye atakayechukuliwa hatua, kwa hiyo ni muhimu yeye mwenyewe kutoa taarifa katika vyombo vya habari au kwenye mikutano ya kiutendaji pamoja na maelekezo kwa watendaji wa Halimashauri.

(iii) Mkurugenzi ndiye Msimamizi Mkuu wa shughuli zote za Halmashauri hivyo anatakiwa kusimamia na kuratibu Idara zote za Halmashauri na kuratibu utekelezaji wa majukumu na kazi za Halmashauri. Katika kufanikisha haya anatakiwa kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Idara zote za Halmashauri.

Kusimamia na kudhibiti masuala yote ya Watumishi wa Halmashauri ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kinidhamu kwa wakati na kwa mujibu wa sheria, Kubuni sera na mipango ya Maendeleo ya Halmashauri na Kusimamia na kutekeleza sera, mipango na maamuzi ya Halmashauri na kuhakikisha kazi za Halmashauri, hasa zile za msingi na za lazima, zinatekelezwa kwa mujibu wa Sera na Sheria.

3.Majukumu na kazi za ukatibu

(i) Mkurugenzi wa Halimashauri kwa mujibu wa Sheria ni Katibu wa Mikutano ya Halmashauri "Baraza za Madiwani"na ana majukumu ya Kutayarisha ajenda ya mikutano ya Baraza/Kamati akimshirikisha Mwenyekiti/Meya wa Halmashauri au Mwenyekiti wa Kamati, kutoa taarifa ya mikutano ya Halmashauri na ya Kamati kulingana na Kanuni za Kudumu za Halmashauri, anawajibika Kutoa au kutuma mihutasari na nyaraka mbalimbali kwa Madiwani na kwa Mkuu wa Mkoa na Wilaya kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Halimashauri
kwa mujibu wa sheria (Sheria Na. 7 na 8 za 1982 Vifungu 68 na na chini ya Kanuni ya 16(1) ya Kanuni za Maadili ya Madiwani za mwaka 2000.


4.Majukumu na kazi za kifedha

(i)Kwa mujibu wa Kifungu cha 33(4) cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290 kinamtaja Mkurugenzi wa Halmashauri kuwa Afisa Masuuli (Accounting Officer). Kisheria kazi ya Afisa Mhasibu ni kuhakikisha yeye binafsi kuwa fedha za umma zilizo katika fungu lake zinakusanywa kikamilifu, zinatunzwa kwa usalama na matumizi ya fedha yanafanywa kwa njia halali na kwa mujibu wa bajeti ya Halmashauri.

B.MKUU WA WILAYA

(i) Kumweka mtu kizuizini kwa muda wa saa 48 mfululizo iwapo atashukiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu na Amani (Sheria ya tawala za mikoa Na 19/1997).

(ii) Kufungisha ndoa za serikali (Law of Marriage Act No 5/1971).

(iii) Kuwa mwenyekiti wa Kamati mbalimbali zitakazoundwa Wilayani.

(iv) Kuhudhuria vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kama mjumbe.

(v)Kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi.

(vi) Kumsaidia Mkuu wa Mkoa katika kuzisimamia Halmashauri za Wilaya na kuhakikisha kuwa zinatoa huduma nzuri kwa wananchi na kwa ufanisi.

(Vii) Kuziwekea Halmashauri za Wilaya mazingira mazuri na kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yake kulingana na sera za serikali.

(viii) Kutekeleza majukumu yote atakayopewa kisheria au kukasimiwa na Mkuu waMkoa.
Na zingine nyingi.

C.MWENYEKITI WA HALMSHAURI

(i) Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri ni Kiongozi Mkuu wa Halmashauri mwenye dhamana ya kisiasa. Dhamana hii humfanya kuwa kioo ndani na nje ya Halmashaui yake.

(ii) Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri ni Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani na Kamati ya Kudumu ya Fedha na Mipango/Utawala.

(iii) Kwa mujibu wa Kifungu Na. 193 (2) cha Sheria Na. 7 ya 1982 na Kifungu Na. 108 (2) cha Sheria Na. 8 ya 1982, Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri ni mtia lakiri/mhuri katika nyaraka zote rasmi za Halmashauri.

(iv) Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri analo jukumu maalum la kudhibiti na kuongoza mikutano ya Baraza la Madiwani ili liweze kufanya maamuzi yenye maslahi kwa wananchi wote wa Halmashauri.

Katika kutimiza jukumu hili Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri anatakiwa kutenda haki kwa Madiwani wote bila kujali itikadi za Kisiasa, Jinsia, Dini, Rangi au Kabila na wakati wote awe mtulivu, imara na asiyeonyesha udhaifu wakati wa kuendesha vikao.

(v) Ili kutimiza wajibu wake wa Uongozi ipasavyo, Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri anatakiwa kupewa Ofisi na Halmashauri ambayo ataitumia kukutana na wananchi wote wenye shida, kero na maoni ya kuboresha utendaji wa Halmashauri mara mbili kwa wiki. Ratiba ya siku hizi mbili lazima iwe wazi na ifahamike kwa wananchi wote.

Aidha, Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri kama atataka kutembelea Halmashauri yake katika harakati za kuhimiza maendeleo, atalazimika kufanya kazi hiyo katika siku hizo mbili tu zilizoruhusiwa na sio vinginevyo.

HAPO TUMEONA KILA MMOJA NA MAJUKUMU YAKE, SASA SHIDA INAANZIA WAPI?

Baada ya kupitia malalamiko ya kila mmoja haya ni baadhi yaliyoonekana;

Wakurugenzi wengi wanalalamika kuingiliwa majukumu na wakuu wa wilaya ambao Wao hutaka kuingilia madaraka ya uamuzi katika Halmashauri ambayo yako chini ya mkurugenzi na kutaka kutawala kila kitu pamoja na wakuu wa idara ambao wako chini ya mkurugenzi.

Badala ya kutaka ruhusa kutoka kwa mkurugenzi, wao hutaka report moja kwa moja na kuwa na amri moja kwa moja na wakuu wa idara ambayo huleta mkanganyiko kuhusu mamlaka ya mkurugenzi katika halmashauri.

ikumbukwe kuwa wote hawa ni wateuzi wa Rais, sasa hapo shida nyingine inapokuja kwa mkurugenzi na mkuu wa wilaya kukutana na pingamizi kubwa kutoka kwa meya ambaye yeye anajinasibu kuwa ni mkuu kuliko wao na yeye kateuliwa na wananchi na sio Uongozi uliopo madarakani.

Pia viongozi Mawaziri wanachangia migogoro hii Kuna waziri nilimsikia akimwambia mkuu wa wilaya Akusanye Taarifa kutoka kwa wakuu wa idara nafikiri sio sahihi.

NINI KIFANYIKE. (MY TAKE)

Sio kila kitu kiwekwe au atupiwe Rais kufanya nafikiri Mfumo mzuri ni kurekebisha baadhi ya sheria za kiutawala ili kuweka Utawala katika Mfumo wa MUUNDO WA UONGOZI AMBAO HAUTAWEZA KURUHUSU migogoro Halmashauri hata kidgo.

1. Wakurugenzi wabaki kuwa Wateule wa Raisi na wafanye majukumu yale yale kama sheria inavyotaka ili kupunguza urasimu na uharibifu wa Rasilimali.

2. Cheo cha mkuu wa wilaya Nafikiri kimekaa sana kisiasa na pengine ndo kinachangia mgongano huu wa kimaslahi na napendekeza Kingeondolewa na wilaya ikabaki chini ya mkurugenzi.

3. Cheo cha mkuu Wa mkoa kama msimamiaji Mkuu wa rasilimali ningependekeza kuwa Asiye Mteuzi wa raisi Iki afanye kazi kwa bidii awe ni mtu wa kuchaguliwa na wananchi
Ntaelezea Baadae.

4. Cheo cha Mkuu wa Kanda au Gavana (ZONAL COMMISIONER) Cheo hiki kitakuwa kinagwanywa kikanda yaani kati ya kanda ambayo itakuwa ni mikoa kuanzia miwili na kuendelea kila kanda iwe na mkuu wake ambaye yeye atashughulikia Maendeleo ya Kanda yake ikiwa ni Pamoja na kushughulika na Wakuu wa mikoa na wakuu wa mikoa kushughukika na wakurugenzi na wakurugenz kushughulika na wakuu wa idara nk.

5. Mawaziri wasitokane na Wabunge waaliopo madarakani ili kuepusha kofia mbili ambazo zitapelekea kushindwa ama kupemdelea majukumu.

Jinsi ya kuchagua wakuu wa mkoa (RC)na Mkuu wa kanda (ZC)

Sasa baada ya kufanyika kwa Uchaguzi mkuu Bunge lipatikana pamoja na speaker wa Bunge, Waziri mkuu atatangaza nafasi za kazi kwa Umma wote wenye sifa atakazoainisha na watu wataapply na maombi hao yata jadiliwa na bunge na hatimae kutapatikana kila kanda watu wawili na kila mkoa watu waili na ndipo majina hayo yatapelekwa mkoani kwa ajili ya kupigiwa kura na hivyo ndo atapatikana mikoani na kandani.

Nina uhakika kwamba uongozi ukiwa hivi Hakutakuwa na Migogoro.

Ni Mtazamo na wala usijenge chuki "Afande Sele".
 
Back
Top Bottom