Mkutano wa Mwakyembe na Hoja za Mgongano wa Maslahi

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Mkutano na waandishi wa habari umeanza takribani dakika 20 zilizopita.

Rostam kawatuma Manyerere, Ballile na Sarah Mosi.

BONYEZA "PLAY" KUSIKILIZA ALICHOKIONGEA

[mp3]http://jambovideos.com/mahojiano/mwakyembe_180309.mp3[/mp3]
 
Last edited by a moderator:
Duh hapo sasa zengwe juu ya zengwe wanakomana wenyewe kwa wenyewe.....ngoja tusubili ataongea nini lakini kuna dalili za kukanusha na kuikana hii kampuni ya umeme wa upepo.
 
Mkutano na waandishi wa habari umeanza takribani dakika 20 zilizopita.

Rostam kawatuma Manyerere, Ballile na Sarah Mosi.

Tutaendelea kuwafahamisha kinachoendelea

Manyerere si aliondoka kwa RA tangu zamani, inawekana ana wakilisha media nyingine lakini si za RA
 
Tuache ushabiki lete news anapinga yaliyosemwa na zile documents au anakubaliana nazo. Je hakukuwa na conflict of interest katika maamuzi na uchunguzi uliofanywa na kama ni hivyo sidhani in the future Dowans au Mwakyembe company zipewe umuhimu wowote wa tenda kama wako hivyo kuweka imani kwa wananchi
 
Tuache ushabiki lete news anapinga yaliyosemwa na zile documents au anakubaliana nazo. Je hakukuwa na conflict of interest katika maamuzi na uchunguzi uliofanywa na kama ni hivyo sidhani in the future Dowans au Mwakyembe company zipewe umuhimu wowote wa tenda kama wako hivyo kuweka imani kwa wananchi
Kwanza ni hivi:

Anasema mambo aloyasema Bungeni hakumaanisha kampuni hii.

Anasema watu wameshindwa hoja ndani ya Bunge na magazeti kama Tazama yanaanza kumwandama.

Anasema magazeti haya yanaamua kuwadanganya wananchi kupotea katika ukweli wa habari yenyewe.

Anasema kitendo cha kuandika "Mwakyembe katika Tuhuma Nzito" ni kukuza mambo tu. Anasema issues ambazo zingeweza kumalizikia Bungeni zinaanza kumaliziwa kwenye magazeti tu. Anasema ya Bunge yabaki Bungeni.

Ameulizwa "Kampuni hii imeanza Uzalishaji?"

Anajibu "Imepata kiwanja cha kwanza kule Singida" na anawashukuru sana raia wa Singida kuwakubalia. Haijaanza uzalishaji wa Umeme
 
No wonder Rostam anatuchezea. Wasomi mahiri, waandishi magwiji, wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa wenye majina wote wakitoka wanalia ROstam, Rostam, Rostam. Inaudhi na pia inakera. Kwangu mimi Rostam ni mbunge tu Igunga, sasa kama kila mtu akitoka anasema Rostam hiki Rostam kile Rostam huku. Jamani wanasiasa na waandishi maarufu huo ni upuuzi na kumjenga mtu bure. Kwa sababu kama Rostam ana nguvu za kuwaumiza wenzie anazitoa wapi-CCM, kama anapesa za kuwaliza na kuwaweka viongozi anazitoa wapi-CCM (ambao ndiyo wanatuibia BoT, PPF, NSSF, nk), kama Rostam ana kiburi anakitoa wapi-CCM (kwa rafiki yake JK). Kwa hiyo kwangu haiingii akilini kila siku kulalamika Rostam, Rostam wakati tunajua mbaya ni CCM. Kingine Mwakyembe kama Rostam anakuchafua ni kwamba CCM ya mafisadi inakuchafua. Kwa hiyo badala ya kulalamikalalamika hama Chama au Anzisheni Chama kingine sisi tutawaunga mkono tu. Hiyo itasaidia kuondoal jinamizi Rostam kwenye ndoto zenu for good. Lakini najua hamna ubavu wa kuhama wala kuanzisha vyama kwa sababu na nyie hamko kwa ajili ya wananchi na pia mnajua mtashughulikiwa kama nyie wenyewe (CCM) mlivyowashughulikia wenzenu waliojaribu kuhama (mfano Njelu Kasaka). Kwa hiyo tumechoka na hizo nyimbo zenu ambazo hazina kibwagizo kama hamtafanya kitendo cha kijasiri sasa.
 
Mwakyembe anadai Alishaondoka kwenye kampuni hiyo na wanaopinga wafuatilie updates za Brela za 2006/07.

Manyerere bado yupo Habari Corporation (alirudi)
 
Looh! ningelikuwa mshauri wa Dr. ningemwambia don't mention Rostam, hiyo kazi weka siku nyingine.

Concentrate kwenye hoja iliyoko mbele yako na jibu mambo yote kwa ukweli kadri uwezavyo.
 
The way waandishi kadhaa wanavyouliza maswali huwezi kushindwa kuelewa dhamira zao!

Kubenea kamwuliza: Hivi Rostam ana interest katika hiyo Project ya Singida?

Mwakyembe kajibu: Mimi siwezi kuzungumzia masuala ya Rostam
 
Anasema: Katika kupambana kutetea Taifa letu tutakumbana na matatizo mengi, yeye anaijua sheria na hajasema kama atawageuzia kibao wanaomchafua. Anasema lakini zipo sheria ambazo zinawafunga watu zikikiukwa!
 
Kuna statement kaitoa akisema: "Mtu anayenuka hawezi kujisafisha kwa maji taka".

Hiyo ni baada ya kuongela magazeti flani na RA.
 
Anasema kuna watanzania wangapi ambao wanaweza ku-declare interest kwenye mambo kadhaa ati kwakuwa wamesajili kampuni tu?

Akatoa mfano: Kuna waandishi wangapi wamesajili magazeti na hawajaacha kazi kwakuwa wameanzisha magazeti?

Akauliza tena: Ingewezekana vipi afanye ku-declare interest kwa kusajili kampuni tu ati akiwa na memorandum of articles? Anasema labda itawezekana lakini si rahisi kwa sababu unakuwa huna kazi in hand.
 
Anasema: "Sina mkataba na Bunge. Nina profession yangu na natamani mambo mengi kama mtanzania."

Anasema kuna projects nyingi ambazo ameziona zimeandaliwa ili ziwe read story za kumchafua Mwakyembe.

Anasema kuna magazeti yanayoandika "Sasa Umoja wa Mataifa unamuunga mkono dhidi ya Mwakyembe". Anasema Profession ya uandishi wa habari imeingiliwa!
 
Back
Top Bottom