Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, zuia watumishi chini yako kusumbua raia maskini wasio na Leseni

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,155
22,655
Twende haraka kwenye mada,

Taarifa zilizotufikia Kutoka vyanzo vya kuaminika zinadai kuwa Hali ni Tete mitaani,

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ameanzisha operation ya kuwasaka wote wasio na Leseni Hadi nyakati za usiku.

Ikumbukwe kuwa ,wapo wafanyabiashara wa kipato Cha chini wasio na uwezo wa kulipa lessen ya 80,000/= Hadi 150,000/= Kwa mwaka, wafanyabiashara hao, ni wale wauza chips, wenye vibanda vya kuchoma CD, mabanda ya vinyozi ,mabanda ya mama ntilie, mabanda ya mbogambogank nk nk.

Wafanyabiashara hao WADOGO walikuwa wakilipia 20,000 enzi za Magu bila usumbufu na hawakusumbuliwa na TRA Wala Jiji wakati Ule.

Sasa 20,000 haitambuliki, Jiji wanakamata watu, na ikiwa huna pesa ya fine 150,000/= ni lupango na JELA moja Kwa moja miezi 6.

Vyanzo hivyo vinadai, operation sasa Iko moto wilaya ya Ilemela.

Tafadhalini, Kusanyeni 20,000/= Kwa Wafanyabiashara wadogo kama enzi ya Magu inatosha. Hali ni ngumu.

Ni hayo tu. Karibuni.🙏
 
Yaani imekuwa mchezo wa paka na Panya, kama kipindi kile Cha Kodi ya KICHWA.

Hii Si sawa.
 
Ni kanda ya ziwa karibu maeneo yote . wakurugenzi wote wanataarifa hizo kukusanya mapato ya ndani
Sasa gia wanayotumia ni kubwa mno, wapunguze.

Chanzo hicho kinadai, yaani wanakuja wamejipanga, Hadi Wana hakimu, na askari mwenye silaha,

Ukikosa faini ya 150, 000/= unahukimiwa JELA miezi SITA hapo hapo.

Na mbaya zaidi, ukiwakimbia mchana, usiku pia wanakuja Kwa kuvizia.

Hii ni kinyume Cha SHERIA, kuwindana usiku kama vile anatafutwa jambazi!!
 
Rudisheni Kodi ya matching guys, 20,000/= ni pesa nyingi sana mtakusanya kuliko kulazimisha kukamua maziwa Kwa ng'ombe aliyekaukiwa.
 
Mitaa ninayokaa Mimi nahisi bado hawajafika.
Hadi mabanda ya nyanya , mama ntilie, wanakamata, wakati SHERIA inataka Leseni inakatwa Kwa mfanyabiashara mwenye pango lisilohamishika.

Wangechukua Ile 20,000/= Ile ni pesa nyingi sana wameacha kukusanya bila sababu ya msingi.
 
Twende haraka kwenye mada,

Taarifa zilizotufikia Kutoka vyanzo vya kuaminika zinadai kuwa Hali ni Tete mitaani,

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ameanzisha operation ya kuwasaka wote wasio na Leseni Hadi nyakati za usiku.

Ikumbukwe kuwa ,wapo wafanyabiashara wa kipato Cha chini wasio na uwezo wa kulipa lessen ya 80,000/= Hadi 150,000/= Kwa mwaka, wafanyabiashara hao, ni wale wauza chips, wenye vibanda vya kuchoma CD, mabanda ya vinyozi ,mabanda ya mama ntilie, mabanda ya mbogambogank nk nk.

Wafanyabiashara hao WADOGO walikuwa wakilipia 20,000 enzi za Magu bila usumbufu na hawakusumbuliwa na TRA Wala Jiji wakati Ule.

Sasa 20,000 haitambuliki, Jiji wanakamata watu, na ikiwa huna pesa ya fine 150,000/= ni lupango na JELA moja Kwa moja miezi 6.

Vyanzo hivyo vinadai, operation sasa Iko moto wilaya ya Ilemela.

Tafadhalini, Kusanyeni 20,000/= Kwa Wafanyabiashara wadogo kama enzi ya Magu inatosha. Hali ni ngumu.

Ni hayo tu. Karibuni.
Suala la leseni si lilihamishiwa Wizara ya Viwanda na Biashara!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ilitangazwa kabisa kwenye media na Waziri wa Viwanda na Biashara kuwa sasa masuala ya leseni yanahama TAMISEMI.
Labda kama TAMISEMI wamebaki kuwa wakala wa ukusanyaji mapato ya leseni!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Nijuavyo Hadi sasa, Mkurugenzi ndo mkusanya pesa ya Leseni za biashara,

Labda tuwekee taarifa hiyo hapa.
 
Mkuu ilitangazwa kabisa kwenye media na Waziri wa Viwanda na Biashara kuwa sasa masuala ya leseni yanahama TAMISEMI.
Labda kama TAMISEMI wamebaki kuwa wakala wa ukusanyaji mapato ya leseni!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Uko sawa,

Kuna makundi mawili A na B.

Kundi A ni Wizara ya viwanda, kundi B ndo halmashauri na Jiji inakusanya

Kundi A ni Leseni za Import na expot licence nk nk.

Kundi B, ni Lesseni za maduka madogo, biashara za ndani, makampuni ya ndani, huduma nk nk
 
Ila tupende kulipia leseni. Kama kubwa tuseme. Tutaendeleaje kila mtu akikwepa kulipia?
Watanzania wanapenda kulipa Kodi ila ikiwa kubwa ndo mtihani.

Vitambulisho vya matching guys mbona viligombaniwa?

Yaani mama mwenye Banda la kuuza mbogamboga anaambiwa alipe 100,000 ya lesseni, hapo TRA Bado kwann asijifiche?
 
Nilitaka kujua ikiwa ujumbe umemfikia mkurugenzi wa Jiji la Mwanza au la, tupige hatua zaidi.
 
Back
Top Bottom